Maoni yangu kuhusu suluhisho la kudumu la kero za Muungano uliopo

Maoni yangu kuhusu suluhisho la kudumu la kero za Muungano uliopo

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,730
Reaction score
2,230
Tunapoikumbuka Aprili 26, ya mwaka 1964, tujikite zaidi katika kuepukana au kumaliza kabisa zinazoitwa kero za Muungano kwa kufanya mojawapo ya yafuatayo:

Mosi, tuwe na nchi moja na serikali moja, yaani Muungano kamili (complete union). Tuachane kabisa na Muungano huu wa kubanana, kufinyana, kupunjana na kulaumiana.

Pili, Tanganyika na Zanzibar ziwe nchi kamili zenye mamlaka kamili na kubakia majirani wema wa kihistoria na kindugu.

Hili ndilo suluhisho bora na la kudumu la Muungano huu usioisha kero.
 
Inawezekana vipi kuwa na nchi moja na serikali moja halafu pia kuwa na Zanzibar na Tanganyika kama nchi kamili zenye mamlaka yake?

Hiko kitu hakiwezekani kutokea.

Suluhisho la Muungano ni wananchi kupiga kura ya maoni kama wanautaka huu Muungano au la na kama wanautaka uwe wa muundo gani. Serikali moja au tatu?

Huu Muungano uliopo sasa hivi ni fake uliamriwa na viongozi bila wananchi kushirikishwa.
 
Samahani, nimesahihisha kwa kuandika "mojawapo ya yafuatayo"
 
Back
Top Bottom