Maoni yangu: Usiingie mkenge wa router za 5G za mitandao ya simu

Maoni yangu: Usiingie mkenge wa router za 5G za mitandao ya simu

Mimi ni mtumiaji wa 5G router zote Airtel,voda na Tigo.

Ukweli katika hizi router 3 mitandao ya ukweli ambayo naweza mshauri mtu atumie ni miwili tu.

Airtel na Vodacom.

Tigo ni wezi sio unlimited wanakupa unlimited kwa speed uliyolipia kisha wakiona unakamua kweli kweli bando kwa limit walokuekea wanashusha speed up to 0.1kb/sec.

Hii speed itakua hovyo mpaka saa 6 usiku ikibadilika siku wana reset wanakuoa tena speed yako. Ukiendelea kupakua matonge unabugia ukifikisha limit yao wanakata tena mpk kesho yake.

Dont go for tigo...kama unaipenda pesa yako. Kwa mnaotaka LIMITED PACKAGe speed yao iko njema.

Airtel

Hawa ni pure unlimited hawana janja janja unaserereka utakavyo ila tu router yao ili i perform vizuri hakikisha haipati joto, ikipata joto ikichemka inaathiri speed kwakua ofisini kuna AC huwa naitega sehemu ambapo najua itapgwa barid haswa naiongezea na fan inakua baridi muda wote.

Ina perform vizuri sana na zaidi ninachoipendea airtel ni power bank hao ya router inayokupa uwezo wakuzurura na router yako kwa begi anywhere.

Go for airtel,na recommend.

Vodacom

HAwa wako poa sana tena wana pure unlimited ila na wao router yao hakikisha isipate joto ila kuna muda notification light inawaka tu red ujue isha heat unachotakiwa ni kui zima na kutulia dk 1 unaiwasha tena unaendelea kuserereka.

Voda wako njema hawana shida go for it... wana router yao ya NOKIA tamu sana kali mnoo..

Faida ya voda kwenye malipo mwezi ukiisha huduma inaendelea hawakati huduma unaweza usilipe hata miezi mi 3.

Ila Airtel na Tigo mwisho wa mwezi ukifika huduma inazima kama umeme wa tanesco.

Airtel ukifanya malipo inawaka on spot.. tigo mpka uwasiliane nao sjui nn ki ufupi TIGO NI HOVYO.
Voda wao nao ukisubiri wakuzimie ukifanya malipo lazima upge simu wakuwashie ila airtel ni ukishajiunga tu unasererekA..

VODA na TIGO kipengele kwenye kuwashiwa huduma utapga wee hadi ukome.
Mimi hawa wote nawaona wezi tu,; ngoja niendelee kutumia Halotel modem kwa vifurushi visivyokuwa na ukomo
 
Hii itakulazimu ununue line tatu zote ziwe registered for unlimited data service. Wasiwasi wangu ni kwamba, hili linawezekana? Maana wanasema ili wakuunganishie line inabidi uende na router yako waiconnect kwa kutumia IMEI number ya router yako na simCard. Sijui limekaaje hili kitaalamu wataalamu msaada
Just use prepaid model of payment
 
Kuwa na router za kampuni zote hizo ni mzigo. Kwanini usiwe na router moja universal na ukawa una badili simcards? 🤔
Nina ofisi zaidi ya 3 kila ofisi ina router 1..

Hizi ni maalumu kwa ajili ya kazi ofisini sio kwamba router 3 kwa matumizi sehemu 1 hapana.

Ofisi niliopo mimi ndio natumia Router inayo perform vizuri, ofisi zingine nimewaekea router hizo zingine.
 
Wewe walipa kiasi gani per site?
Kwa matumizi ya ofisi the cheapest ni ttcl na wapo vizuri. Hata hao wengine hununua bandwidth,marine fiber optic cable(EASSY&SEACOM) inayohodhiwa na ttcl!
For mobile broadband I recommend Halotel wapo hadi vijijini!
 
Hamna asiependa cheapest service shida ni upatikanaji wa TTCL nenda ofisi zao wambie unahitaji huduma uone kona kona zake.. sio rahisi kama ilivyo kwa hawa wengine.
 
Hamna asiependa cheapest service shida ni upatikanaji wa TTCL nenda ofisi zao wambie unahitaji huduma uone kona kona zake.. sio rahisi kama ilivyo kwa hawa wengine.
Kuwa na backup ni Sawa. Lakini Fanya application ya ttcl itafika muda watakuunganisha tu
 
Kuwa na backup ni Sawa. Lakini Fanya application ya ttcl itafika muda watakuunganisha tu
Time consuming.. watu hela tuzitafute kwa shida na kupata huduma ya kulipia napo utafute kwa shida.

ingekua ni free ningehangaika ila kama ni pesa tu, acha tutumie kinachopatikana kwa urahisi Mkuu.

MJini Muda Ni PESA.
 
Back
Top Bottom