Kiongozi anaefaa ni Emmanuel Nchimbi.Ndugu IIT MWASISI OS,
Sehemu hii ya pili ya andiko lako inazidisha msisimko wa hadithi, lakini kiuhalisia unazidi kuchora picha ya kiongozi wa kufikirika kwenye sinema (character profile) kuliko kiongozi halisi wa kisiasa anayeweza kuongoza nchi kwenye ulimwengu wa sasa. Huu wasifu wa kijana maskini, mwenye chuki na umaskini, mkimya, mwenye IQ kubwa, anayevunja sheria kulinda wanyonge, na mwenye "Savior Complex" ni nadharia hatari sana kijamii na kisiasa kwa sababu zifuatazo:
Mosi, dhana ya "Benevolent Dictator" au Dikteta Mwema anayeendesha nchi kwa "Mkono wa Chuma" ili kuondoa urasimu ndani ya siku 365 ni mtego wa kisaikolojia. Unaposema atavunja sheria na mifumo kisa tu ana "nia njema", unasahau kuwa sheria na taratibu (hata zile unazoziita za kijinga) ndizo zinazomlinda mwananchi wa kawaida asionewe na mwenye nguvu. Kiongozi anayevunja sheria kwa kisingizio cha kuwasaidia maskini, ndiye huyo huyo atakayevunja sheria hizo hizo kuwakandamiza pindi wakimkosoa. Mkono wa chuma hauna macho, na historia inajua jinsi udikteta "wenye nia njema" unavyoishia kuwa jinamizi.
Pili, hili suala la kiongozi kuongozwa na "Chuki ya Kudumu" na "Maumivu ya Utotoni" ni hatari sana kisaikolojia (Crucible of Hardship). Kiongozi wa nchi anatakiwa kuongozwa na hekima, utulivu, na dira ya pamoja, sio na vinyongo, majeraha ya utotoni, au chuki binafsi dhidi ya mifumo. Kiongozi anayeendesha nchi kwa hasira na visasi vya utotoni, mara nyingi huishia kuona kila mtu anayemkosoa kama msaliti au adui, jambo linalofanya utawala wake kuwa wa hofu badala ya maendeleo.
Tatu, dhana ya "Savior Complex" (Utume wa Ukombozi) ambapo kiongozi anaamini ana "Wajibu wa Kiungu" na anaweza kutumia mamlaka yake hata "nje ya Katiba," ndio msingi wa tawala zote dhalimu zilizowahi kuharibu nchi mbalimbali duniani. Nchi haiondolewi umaskini kwa "Agizo la Rais ndani ya masaa 24" kama amri ya kijeshi. Uchumi wa kisasa unategemea diplomasia ya kikanda, sera za kodi zenye utulivu, masoko huru, na imani ya wawekezaji. Amri za kijeshi kwenye uchumi huwa zinasababisha bidhaa kupotea, mfumuko wa bei, na wawekezaji kukimbia—na mwisho wa siku anayeumia ni yule yule mwananchi wa chini.
Mwisho wa siku, usemi wako wa "Kutoka kwenye Chanzo, Tutarudi kwenye Chanzo" unaonyesha jinsi unavyojaribu kuvika siasa joho la kiroho ili kuhalalisha utawala wa mtu mmoja mwenye nguvu zote. Ni vyema tukakumbuka kuwa mifumo imara ya kisheria na taasisi madhubuti ndizo zinazoleta maendeleo endelevu, sio "Masihi" wa kufikirika anayetawala kwa hasira za uswahilini. Katika ulimwengu huu halisi, hata huyo dikteta mwenye "frequency" za juu atalazimika kufuata bajeti ya nchi na kulipa madeni ya nje, mambo ambayo hayaitikii amri za mkono wa chuma.
LGBTQ kuruhusiwaYote haya yatafanywa na huyo atakayekomboa nchi hii
- Militarization of the country kuondoa tatizo la ajira huko mbele nitaelezea atawezaje hili. Usaili mzito na kwa program maalumu..mamillion ya vijana
- Urudishaji wa rasilimali zilizoibwa tanzania kwanzia mafuvu zana hadi mijusi mikubwa
- Uratibu wa kila kitu cha msingi chini ya serikali
- Wizara za kistartejia baada ya kuangalia zilizopo dunia nzima na kuandaa mpango maalumu wa wizara
- Kuzuia uchafuzi wa mazingira na kuanzisha miradi mikubwa ya TARI na TSF
- Kuratibu malazi kote Tanzania amna mtu atakayelala nnje ya nyumba na ceiling
- Mwisho wa bidhaa feki Tanzania mara mia hata mitumba sio bidhaa feki hapa FCC Na kina TRA etc watawajibishwa ipasavyo
- Kuwarudishia taasisi za dini ETC maeneo yao yaliyotaifishwa 100% kuanzia mashule na kuwapa ma hospital yao 100%
- Nguvu kwa TISS kuchunguza wafadhili na wawekezaji kuzuia state capture
- Mwisho wa dawa za kulevya tz watu walewe hadi wafe ila kizazi cha kuganda barabarani ni mwisho
- LGBTQ kuruhusiwa ila sio kwa nia ya kuchafua sura ya Tanzania Abroad kwa wao kupost utumbo mitandao ya uma wahangaike na mitandao yao na privacy zao. Wenye misimamo mikali kote Tanzania either kuwapinga au kubagua watapelekwa RE EDUCATION Center
- Ulinzi shirikishi na ubalozi wa nyumba 10 kurudishwa kwa nguvu kuhakikisha takribani karibia nusu ya watanzania watakuwa shift za usiku huko mbele tutaelewa kwa undani
- Uchifu,umangi etc kurudishwa kama ceremonial kama Uganda kwa kudhibitiosha DNA za mababu kwa kufukua maiti zao 100% na sio uchifu wa mr=tu kujisimika
- Kiswahili kote Tanzania na sio kuweka mabango ya kichina kila sehemu au lugha nyingine wahangaike na maeneo yao kama china town na sio kisa wanajenga barabara uchina kila sehemu NO
- FGM kuratibiwa ki hospital na mila nyingine zitakazoonekana zinafaida
- Ofisi za serikali nyingi zitakuwa 24 hours na ulinzi wa doria nzito sana usiku
- CNI kamati maalumu ya masilahi ya taifa itaanzishwa Committee of National interest
- Large Emergence Ministry itakayounganisha mifumo yote ya dharura Tz na kuwa na namba kama 111 ambayo itakuwa raisi sana
- Mwisho wa ufisadi Tanzania Sera ya No tolerance ni chap mahakama ya jeshi na hukumu ya kifo bila kujali
- No to ndugulization ,tribalism na upendeleo wowote wa kibaguzi nchini
- Wenye miaka 100+watakuwa na upendeleo mkubwa kama kuzungushwa miti mingi na hifadhii kwa gharama za serikali na vitu vingi vitakuwa bure kwao
- Uingizwaji wa wanyama adini na wanyama ambao nchi nyingine ni Invasive kama Ngamia Australia akati wamasai wanahangaika kufa kwa mifugo kipindi cha kiangazi
- Maghala makubwa kila mikoa na wilaya ya nyama.mafuta,maji,nafaka kwa ushirikiano na TAWA,TANAPA,NCAA,TAWIRI.
- Utengenezaji wa mvua sehemu kali kwa kutumia chumvi NACL
- Serikali itatangaza Burrial crisis na kuanza kwa kuchoma maiti na kuponda mifupa na meno kwa asilimia 100 tanzania watu watakuwa na vijibakuli vya majivu hiii itapunguza magharama za mamisiba na majeneza nab ado sehemu za ardhi kuendelea kupunguzwa.incinerator zitawekwa kila kijiji wilaya na mikoa zenye uwezo hadi wakuchoma watu 100,000+ ili wakati wavita na milipuko kazi iwe kasha. Ruksa ya kutupa au kuzika maiti katikati ya bahari kama marine wanavyofannya
- Masoko Tanzania nzima kuboreshwa kwa kujengwa maghorofa ili kupambana na jua na mvua
- Mwisho wa machinga majijini na mijini Tanzania.huu ukwepaji kodi utakufa kifo kibaya
- Walimu wakali na katili watakuwa kipaumbelle kwa kupandishwa madaraja shule zitaendeshwa kwa mifumo ya jeshi bila kujali ni international wala nini asunbuhi mpaka usiku.shukle zote za primary na Olevel zitakuwa boarding
- Tanzania kuwa na dira sio tuu ya miaka 5-50 bali kuwa na hadi millennium goal za miaka 1000+ijayo hiii itafanya kiongozi yeyote asiende nje ya mstari bila ya kuwa kitukikubwa kimeingilia kama majanga
- Uratibu mzuri wa habari na fake na prank news zitakuwa labeld kabisa
- Vikosi maalumu kama Basij Gestapo SS na Secret servise kuanzishwa kwa kuendesha kazi maalumu ndani na popote ulimwenguni hapa na angani
- Uanzishaji wa vikosi maalumu kama IMF imposible mission force watakao weza fanya lolote kwa yeyote
- Kila kijiji kutakuwa na Mini Arena kwa ajini ya michezo mbalimbali yaani Mult purpose arena
- Kuratibu maeneo yote ya hospital za akili na mwishowa Sober house za mwisho kabla ya kufungwa
- Vunwa kwa miti yote mikongwe na mikubwa Tanzania isiyo ya dawa kwa ajili ya kazi mbali mbali nitakazoelezea huko juu sustainable timber.na mashamba ya kisasakwa ajili ya timber na carbon business.na supply chain nzima ya raw material in accordance to market world wide
- Tanzania kuwa donar mkubwa wa viungo vya binadamu
- Ruksa kwa mtanzania kuamua kufa kwa maamuzi.bila maumivu kwa uratibu wa serikali
- Ruksa kwa wazazi kutoa mimba endapo watagundua motto atakuwa na ulemavu wowote na hitilafu na kumfanya kuwa mzigo toka utotoni hapa duniani
- Serikali kuratibu makampuni yote ya telecommu ikiwezekana hata kuyanunua ili kuhakikisha kila kitongoji hamna issue ya kukosa mawasiliano
- Ai kufungwa kwenye AGRO Tanzania nzima na mifumo ya hali za hewa
- Kama BBC 19/2/26 kuhusu Somalia
- Mashirika mengi legelege serikalini kubinafsishwa au kuvunjwavunjwa kama tanesco
- Kazi nyigi almost zote kutoa mauaji zitarasimishwa hasa sex worker au Madada poa na Madada uroda kwa utaratibu maalum
- Maoneo ya nyikani na hifadhini kutaanzishwa tha kargest manmade sea ambazo zitawekewa Plastig Balls kuzuia evaporation of water
- Kuanzisha Tanzania Eden program ambayo wanyama wengi wa porini watauzwa kwa bei ya chini kwa watanzania wafugwe kama pet au for leisure hasa matajiri
- Kuanzisha mashamba ya chakula kwa wanyama yatakaokuwa na mifumo tofauti hata ya umwagiliaji wa helicopter na Seed balls kuendana na TARI na kuotesha mimea mingi.hasa miti ghali kama rese wood na black wood+orchidaceae
- Wanyama wengi wa porini wataanza kulelewa kwenye maeneo maalumu toka utotoni kuwafanya kuwa na tabianzuri na wanadamu.nursery na cages na kuwa na DNA na Sperm bank kubwa duniani kwa ajili yao BBC3/3/26 kuhusu cages South A na DNA kwa samba zilizosaidia kuzuia poaching
- Mashirika yote ya kudhibiti kuangaliwa kwa jicho la umakini kama TBS etc
- Tanzania kuwa kinara kwa usalama 100% msichana atakaye vaa cheni ya dhahabu ataweza tembea na miguu toka mtwara hadi kagera bila kudhurika
- PMC contactor yetu ya Tanzania kufanya kazi mbalimbali Africa na dunia
kwa atakayoyafanya hakutakuwa na upinzani na wapinzani kwa mara ya kwanza watamkubali na ku mu endowseAtaharibu uchaguzi na kujipa ushindi wa asilimia mia akiamini kwamba wananchi wote wa jamhuri ni maamuma na vilaza hivyo wanyang'anywe haki yao ya kuchagua viongozi wao lakini yeye ni jiniasi (baba wa wananchi) kwahiyo ajiweke madarakani kwa nguvu.
kuhusu mambo ya katiba mpya sikuonyeshwa maana kiongozi huyu atakuja mbeleni sanaAtaupotezea mchakato wa katiba mpya, kwasababu haamini kwenye utawala wa sheria anadhani yeye ndio sheria. Pia haamini kwenye maridhiano ya kitaifa anaamini kwenye kuendesha mambo kwa nguvu hivyo atawaonea bila hata ushahidi wale anaotofautiana nao kimawazo.
ndio atakayoyafanya huwezi kuwa na title ya baba wa wananchi alafu UBAGUE wananchi kwa misingi yeyoteLGBTQ kuruhusiwa
Duh YBWYB ndugu
yeye atakachofanya sio wimbi la utekaji na uuaji bali atafanya parcial forced disappearance ya muda kwa baadhi ya watu hasa magaidi.Yeye na timu yake ya praise and worship (wanamuabudu yeye) hawataamini wananchi wakiwakataa kwasababu wanajiona ni wazalendo kupita watu wote na wanajiita (baba wa wanachi)
Hivyo wataanza kutunga stori za uongo bila kutoa ushahidi wowote kwamba wapinzani wao ni vibaraka au mafisadi na wimbi la utekaji na uuaji litashika kasi sio mfano.
na kwambia hatafanya hivyo na Tanzania itakuwa ni nchi namba moja kwa amani duniani kiasi ambacho msichana aliyevaa cheni ya dhahabu safi atatembea toka Mtwara hadi Kagera Bila kukutana na upinzani wowoteAtaondoa wapinzani wote bungeni na kutengeneza bunge la chama kimoja kwa sababu haamini kwenye uongozi jumuishi na hataki changamoto
Amna taasisi itakuwa HURU mbwele yake maana lazima migtazamo yake na maono yake yatimizweAtafanya mambo ya kifisadi na ambayo ni kinyume na utamaduni wa nchi (rejea misimamo ya mwalimu Nyerere) kwa uwazi kabisa kama vile kujenga uwanja wa ndege kijijini kwake lakini asione kwamba ni ufisadi. Kwasababu anadhani nchi ni mali yake.
Atataka kumpelekesha mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ofisi inabidi iwe huru, ipewe meno na iachwe ifanye kazi zake vizuri kwasababu ameonyesha mapungu ya utawala wake. Atasema mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali anatumika bila kutoa ushahidi wowote.
kwa mara ya kwanza Yeye atawateka na wengine watapotea hapanaKwasababu atakuwa amevibomoa vyama vya upinzani kitaasisi. Wanasiasa wa upinzani watakuwa hawana jinsi zaidi ya kugeuka wanaharakati.
Yeye atawateka na wengine watapotea bila kufuata utaratibu wa kisheria akitumia watu wake wa propaganda kudanganya wananchi kuwa "wanaharakati ni wabaya" jambo ambalo dunia nzima inajua si kweli
huenda labdaKiongozi anaefaa ni Emmanuel Nchimbi.
Tafadhali Kijana wa Ifoza nipe changamoto kwa hicho nilichosema
LGBTQ siyo ishu ya ubaguzi ni ishu ya maadili nani huyo anadanganya watu hukoLGBTQ kuruhusiwa
Duh YBWYB ndugu
Hiyo siyo sahihi, nchi hii itakombolewa na watanzania wote kwa umoja wao sio na mtu flaniAmna taasisi itakuwa HURU mbwele yake maana lazima migtazamo yake na maono yake yatimizwe
Ndugu Mroki,Kiongozi anaefaa ni Emmanuel Nchimbi.
Tafadhali Kijana wa Ifoza nipe changamoto kwa hicho nilichosema
Hata hivyo, tukiweka mihemko pembeni na kuangalia ukweli wa mambo kiweledi na kihistoria, tuna wajibu wa kuwapima viongozi hawa kwa matendo yao ya nyuma (track record) na si kwa maneno yao ya sasa wanapokuwa nje ya mfumo mkuu wa maamuzi.Kiongozi anaefaa ni Emmanuel Nchimbi.
Tafadhali Kijana wa Ifoza nipe changamoto kwa hicho nilichosema
Duh aisee nimepata somo.Ndugu Mroki,
Shukrani kwa mchango wako. Jukwaa hili ni huru na kila mmoja wetu ana haki na uhuru kamili wa kutoa maoni yake. Kama kwa mtazamo na vigezo vyako unaona Dkt. Emmanuel Nchimbi ndiye kiongozi anayefaa, mimi ni nani wa kukupinga? Hiyo ni haki yako kidemokrasia.
Hata hivyo, tukiweka mihemko pembeni na kuangalia ukweli wa mambo kiweledi na kihistoria, tuna wajibu wa kuwapima viongozi hawa kwa matendo yao ya nyuma (track record) na si kwa maneno yao ya sasa wanapokuwa nje ya mfumo mkuu wa maamuzi.
Kihistoria na kiutendaji, kuna mashaka makubwa kama Dkt. Nchimbi ana tofauti na wanasiasa aina ya Humphrey Polepole—ambao huwa upande wa wananchi na kuonekana "watetezi wa wanyonge" pale tu wanapokuwa nje ya mamlaka au pale maslahi yao binafsi ya kisiasa yanapoguswa. Ukweli huu unathibitishwa na mambo mawili makubwa:
Mosi, tunakumbuka vyema Mei 2013 bungeni wakati Dkt. Nchimbi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Alipowekwa kitimoto na wabunge na kutakiwa kujiuzulu kutokana na changamoto za kiusalama, majibu yake yalijaa kiburi cha mamlaka na dharau kubwa kwa misingi ya uwajibikaji. Kauli yake maarufu ya kuwabeza wapinzani na wabunge kuwa "kama mnataka kufukuza mawaziri nendeni mkagombee urais mshinde" ilionyesha dhahiri dharau dhidi ya taasisi ya Bunge inayowawakilisha wananchi. Hakuwa upande wa raia, alikuwa upande wa kulinda madaraka yake.
Pili, ni utekelezaji wa "Operesheni Tokomeza Ujangili" (OTU) ya mwaka huo huo wa 2013. Chini ya usimamizi wa wizara yake, operesheni hiyo iligeuka kuwa jinamizi kwa wananchi wa kawaida—haki za binadamu zilikiukwa vibaya, raia waliteswa, walibakwa, na wengine kuuawa kwa kisingizio cha kusaka majangili. Ililazimu ripoti ya Kamati ya Bunge iliyofanywa kwa uzalendo mkubwa chini ya Mheshimiwa James Lembeli kuumbua madudu hayo, jambo lililopelekea shinikizo kubwa lililomng'oa madarakani mnamo Desemba 2013 kwa kushindwa kuwajibika mapema.
Hivyo basi, unapomzungumzia Dkt. Nchimbi kama mfano wa "Masihi" au kiongozi wa mfano kwa sasa, ni lazima ujiulize: Je, tunamhukumu kwa kauli zake za sasa akiwa kwenye majukwaa ya kisiasa, au tunampima kwa matendo yake ya dharau kwa mifumo ya uwajibikaji na ukiukwaji wa haki za raia uliotokea chini ya usimamizi wake akiwa na dhamana kubwa ya nchi?
Ukweli unabaki palepale: mifumo imara na taasisi madhubuti ndizo zitakazookoa nchi hii, si wanasiasa wanaobadilika rangi kulingana na upepo wa maslahi yao unavyoelekea.
na wewe unaweza kumchambua kiongozi. Nilishaandika makala kuhusu Tundu Lissu ingia google uchambuzi wa kijana wa Ifoza kuhusu Tundu Lissu. Soma hapa kujua kama Lissu anafaa ama la mimi nimeelezea Maisha yake Uanaharakati na siasaDuh aisee nimepata somo.
Vp kuhusu mh Tundu Lissu mchambue na huyo basi
Basi nishajua unamkubali nanina wewe unaweza kumchambua kiongozi. Nilishaandika makala kuhusu Tundu Lissu ingia google uchambuzi wa kijana wa Ifoza kuhusu Tundu Lissu. Soma hapa kujua kama Lissu anafaa ama la mimi nimeelezea Maisha yake Uanaharakati na siasa
Mimi sina upande au mtu maalum ninayemshabikia. Mtazamo wangu ni rahisi: kiongozi yeyote atakayetuhakikishia Watanzania kuwa tutaishi ndani ya nchi yetu kama wamiliki halali wa rasilimali na mustakabali wa taifa hili tunalolipenda—awe anatoka CCM au chama kingine chochote—huyo ndiye nitakayemwona anafaa.Basi nishajua unamkubali nani
Kwani Nchimbi ni mtu wa kuyumba na kununulika maana huyo ndiye niliyemtajaMimi sina upande au mtu maalum ninayemshabikia. Mtazamo wangu ni rahisi: kiongozi yeyote atakayetuhakikishia Watanzania kuwa tutaishi ndani ya nchi yetu kama wamiliki halali wa rasilimali na mustakabali wa taifa hili tunalolipenda—awe anatoka CCM au chama kingine chochote—huyo ndiye nitakayemwona anafaa.
Kuhusu Lissu, nilimtolea mfano tu ili kuonyesha utofauti wake wa kimtazamo na kiutendaji ukilinganisha na wanasiasa wengine, lakini hiyo haina maana kwamba tayari nimemthibitisha anafaa kuwa Rais. Utofauti wake mkubwa ni msimamo wake usiobadilika badilika. Ukisoma hiyo link niliyokupatia, utaona nimeeleza kwa kina matatizo na changamoto nyingi kubwa alizopitia; kama angekuwa mtu wa kuyumba au kununulika kama hao wengine uliowataja, huenda leo hii angekuwa hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Msingi wangu si mtu, bali ni msimamo na maslahi ya nchi.
Ndugu faana,