Uchaguzi 2020 Maono, malengo, matarajio ya Membe kuwania Urais yameisha rasmi?

Uchaguzi 2020 Maono, malengo, matarajio ya Membe kuwania Urais yameisha rasmi?

Mr Q

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
18,046
Reaction score
38,598
Ni mada ya kuuliza tu maana tangu Aguswe baada ya vile vikao swala la kugombea ama kuwania kiti cha uraisi naona kama zimeyeyuka.

Mh. Membe muda ndio huu watu wanachukua fomu za ugombea nawe kama mtu ambaye kwa namna fulani ulijipambanua kama mtu mwenye malengo ya kuwa Rais siku moja usipoteze ata nukta kachukue sasa.

Nakukumbusha kuna memba humu JF walianzisha hadi tag ya #2020twendenamembe sioni kama litakuwa jambo la busara kuwa angusha.

To other JF members do you think Mr Benard fits to replace the current presidet and become the next president?
images (11).jpeg
 
Nilisikia waliprinti fomu moja tu na printa pamoja na kifaa kilichotumika kuchapa hiyo fomu viliharibiwa kabisa

Na mlango wa ofisi ukatiwa kufuli?[sina uhakika na hili]

Tunashuhudia zanzibar idadi ikizidi kuongezeka
Daah nikajua bado form zinatolewa huko CCM ili achukue maana ndoto zake ni kua rais kupitia CCM tu.
 
Daah nikajua bado form zinatolewa huko CCM ili achukue maana ndoto zake ni kua rais kupitia CCM tu.
Sina uhakika kama nikupitia ccm tu kwa siasa zetu hizi Unaweza kuta akaibukia ACT tatizo sheria saivi nadhani zinambana mtu anayehama chama na kugombea uraisi
 
Sina uhakika kama nikupitia ccm tu kwa siasa zetu hizi Unaweza kuta akaibukia ACT tatizo sheria saivi nadhani zinambana mtu anayehama chama na kugombea uraisi
ACT atakuja kwa kazi 1 tu,kugawanya kura za Upinzani then akimaliza kazi hio atarudi zake nyumbani CCM kama wenzake Lowassa/Sumaye.
 
Pata Picha ndio Chadema Leo hii wangeprint na wao Form moja kisha akapewa mgombea wao tu.....halafu huyo Mgombea angekua The Freeman! Dah tusingelala wallah. Ila wao wote wamefyata mikia yao kama mbwa koko wa kijijini kwetu
 
Hahahahahah Ati wamefyata mkia

Saivi ukijiinua nakuleta usumbufu vumbi la kisiasa likitulia jiandae kutembelewa na taasisi zifuatazo

Takukuru wakikuhoji nyumba ulizojenga ulitoa wapi pesa
Tra wakija na takwimu za kodi ulizo kwepa na mambo mengine kama hayo.

Nani sasa anataka usumbufu kama huo kisa fomu ya uraisi?
 
Huwenda hizi ni hearsay tu tujipe muda kwasababh bado zoezi halijafungwa wengine wanaweza kuongezeka
Ndio maana akili yangu inagoma kuamini, chama chenye demokrasia komavu kama hiki wanawezaje kumnyima haki ya kugombea mwanachama mwingine? Yaani wanarudi enzi za kuchagua kivuli?
 
Ni haki ya Membe kugombea chama chochote atakacho, ila sio lazima awemgombea kwa chama chochote.anaweza kaa akatulia ili kutunza heshma yake ya kulitumikia taifa la TZ.
Ushauri mzuri ila kugombea pia sio kuharibu heshima. Ni pamoja na kuongeza CV na kuwa mmoja wa watu wanaoingia ktk historia ya taifa hili, historia itakayo somwa na kusimuliwa kizazi hata kizazi
 
Hahahahahah Ati wamefyata mkia

Saivi ukijiinua nakuleta usumbufu vumbi la kisiasa likitulia jiandae kutembelewa na taasisi zifuatazo

Takukuru wakikuhoji nyumba ulizojenga ulitoa wapi pesa
Tra wakija na takwimu za kodi ulizo kwepa na mambo mengine kama hayo.

Nani sasa anataka usumbufu kama huo kisa fomu ya uraisi?
Mpwa tuchati....
 
Nilisikia waliprinti fomu moja tu na printa pamoja na kifaa kilichotumika kuchapa hiyo fomu viliharibiwa kabisa

Na mlango wa ofisi ukatiwa kufuli?[sina uhakika na hili]

Tunashuhudia zanzibar idadi ikizidi kuongezeka
Ulisikia....... That's not a good word for a great thinker!
 
Ulisikia....... That's not a good word for a great thinker!
Ndio maana kuna mahali nimesema na ku admit kabisa [sina uhakika na hilo]
Katika nyakati hizi masikio lazima yafanye kazi kuliko kawaida
 
Back
Top Bottom