Maono: Tuepuke siasa za vyama katika makao makuu ya nchi Dodoma

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Kuna wakati nakuwa sina uhakika sana na dhamira ya nchi hii kuhamia Dodoma ila ngoja nichukulie kuwa dhamira hii ni ya kweli na itadumu.

Taifa la Marekani walifanya kitu kimoja unique sana wakati wa muundo wa Katiba yao. Katika majimbo yao yote 50, waliipa mji wao mkuu Washington DC utaratibu tofauti wa kiutawala na kiuongozi.

Hii ni katika kuutambua kama mji mkuu wa Marekani na walifanya hivyo kuepuka siku zijazo mtu au chama kujiona kuwa kwa kumiliki idadi kubwa zaidi ya wapiga kura wa mji ule au utawala wa mji basi wao ndiyo wanastahili kuwa watawala wa Marekani. Nadhani walifanya hivyo pia ili isitokee mtu au chama kitakachotaka kucontrol shughuli za wanasiasa wengine wakiwa mji mkuu katika majukumu yao ya kikazi.

Sitaenda kwenye details sana ila ningeomba kama ungependa chukua muda uangalie mfumo wa utawala wa Marekani na kwa jinsi mji wao mkuu wa Washington DC ulivyo tofauti kiutawala na kisiasa.

Waanzilishi wa taifa lile la Marekani pamoja na mapungufu yao ila walibarikiwa sana uwezo wa kuona mbali nchi yao inahitaji nini kwa miaka mingi ijayo. Hata pale walipokuwa wamepungukiwa kitu, masuluhisho ya mapungufu yao kwa kiasi kikubwa unayakuta humo humo ndani ya Katiba yao waliyoiandika wao wenyewe.

Binafsi shambulio la Tundu Lissu linaniumiza mpaka leo siyo tu kwa mazingira yanayozunguka utokeaje wake au kwa jinsi vyombo vyetu vya dola vilivyoshindwa kulishughulikia baada ya, lakini pia kwa sababu ya eneo na mji lilipotokea, mji mkuu wa nchi.

Juzi nimeangalia clip moja ya Mwenyekiti wa Baraza la Wazazi CCM, "somebody" Malecela, akitoa maneno ya kejeli na vitisho kuhusu CHADEMA na kwa mara nyingine, dhidi ya Tundu Lissu na akahusisha vitisho hivyo na mji wa Dodoma akitamba kuwa ni ngome ya CCM.

Haya ni maono yangu na nimeyapata kwa kutafakari jinsi Wamarekani walivyofanya katika muundo wao wa uongozi. Ikiwezekana huko mbele tutakapostaarabika katika siasa zetu, tusisahau kuangalia uwezekano wa kuufanya mji mkuu wa Dodoma free of "nasty politics" na kuna njia nyingi za kufanikisha hilo.

Tuendelee kubadilishana mawazo ila tusisahau kuweka utaifa mbele kwanza.
 
CCM wakizidiwa hoja ni mwendo wa vitisho tu na kulialia kwamba wanatukanwa
 
Back
Top Bottom