Uko mji/eneo gani?Habari,
Kwa muda sasa tangu nimehitimu chuo Kikuu nimekuwa na ndoto ya kuanzisha na kumiliki shule ya Awali na Msingi japo kuwa tangu nimalize chuo mwaka 2018 sijafanikiwa kupata ajira hivyo nimekuwa nikijiajiri mwenyewe kupitia kituo Cha Masomo ya ziada ( Tuition Center) na Chekechea.
Je Kuna mtu yeyeto ambaye ana ndoto kama yangu, au ameshaanza anaweza kushea hapa safari yake !?
- Aliwezaje kupata mtaji wa kuanzia
- Aliwezaje kukusanya pesa ya kununua eneo, kujenga, samani, gari la shule N.K??
- Nimejaribu kufatilia mahitaji ya eneo kuanzisha shule ni ekari 3, na kwa maeneo niliyopo heka Moja naweza pata kwa 20M sasa namna ya kukusanya hiyo pesa ndio changamoto kwangu au nitumiale mkakati gani kuweza kuipataUko mji/eneo gani?
Kwa vile una Tution center tayari, umeshapiga hatua moja mbele
Kwasasa unachotakiwa kufanya ni kuwa na focus
Kwenye hiyo center yako, fanya marekebisho madogo madogo yatakayowezesha ku accomodate watoto wadogo (miaka 3+) kisha pageuze kuwa Day care.
Ukifanya vizuri kwenye Day care, watoto hao hao ndio watakuanzishia Nursary na kuendelea.
Shule nyingi zinaanzia sehemu ya kukodi, ukishakaa vizuri utanunua eneo