Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Maonyesho ya 127 ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa ya China yanayojulikana kama Canton Fair yamefunguliwa rasmi tarehe 15.
Hii ni mara ya kwanza kwa maonyesho haya kufanyika kwa njia ya mtandao
Wafanyabiashara na wateja kutoka China na nchi za nje wanaweza kufanya biashara kutoka nyumbani
Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni “kunufaishana mtandaoni kwa watu wote”
Makampuni ya China na ya nchi za nje yanaweza kuonyesha bidhaa mpya kwa kutumia teknolojia ya kidijitali
Maonyesho hayo yanayapatia makampuni ya China na ya nje fursa mpya za kibiashara za kunufaishana
Maonyesho hayo yamevutia makampuni elfu 25 ya China
Na yana maeneo 50 yanayoonesha aina 16 za bidhaa.
Bidhaa zote zitaonyeshwa mtandaoni kuanzia tarehe 15 hadi 24 mwezi Juni
Makampuni yanayoshiriki yataonyesha bidhaa zao kwa picha, video na 3D.
Ili kuonyesha taswira ya chapa zao kwa njia mbalimbali.
Sifa nyingine ya maonyesho hayo ni kutoa huduma za kutangaza bidhaa kupitia matangazo ya moja kwa moja.
Na kutakuwa na studio ya matangazo ya moja kwa moja ya saa 24 kwa kila kampuni.