Ijumaa hii Shangahi inafungua milango yake tena kwa Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji ya China, ( CIIE).
Ikiwa sasa ni mwaka wake wa nne, maenesho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kwa bidhaa za dunia kupata soko nchini China na pia wafanyabiashara kukutana na kubadilishana.
Kama mwaka uliopita, mwaonesho ya mwaka huu yana vitengo 6 vikuu ambavyo bidhaa za chakula na kilimo, magari, vifaa vya jumla, bidhaa za matumizi kwa jumla, vifaa vya matibabu na bidhaa za afya na huduma.
Ikiwa na eneo la maonyesho la zaidi ya mita za mraba 366,000, CIIE ya mwaka huu yatakuwa na karibu biashara 3,000 kutoka nchi na kanda 127, zote zikiwa juu kuliko yale ya mwaka jana.
Rais Xi Jinping wa China tarehe jana jioni amehutubia ufunguzi wa Maonyesho hayo kwa njia ya video, na kusisitiza kuwa China italinda hali yenye pande nyingi bila kuyumbayumba, kunufaika pamoja fursa za soko na dunia nzima, kuhimiza kufungua mlango kwa kiwango cha juu na kulinda kithabiti maslahi ya pamoja ya dunia.
Rais Xi amesema, mawingu ya janga la COVID-19 hayajaondolewa, mustakabali wa ufufukaji wa uchumi duniani unakabiliana na changamoto nyingi, watu wa nchi mbalimbali wanahitaji zaidi kushirikiana na kusaidiana, ili kukabiliana na taabu zilizopo sasa.
Maonesho haya yanafanyika wakati sasa dunia ikiibuka kutoka kwa athari za janga la Covid-19 ambalo limeathiri vibaya uchumi na biashara nyingi duniani.
Mbele ya hafla hii muhumu China imekuwa ikikaribisha makampuni ya biashara kutoka Afrika kushiriki ili kutafuta fursa za biashara katika soko la ndani.
Mwezi Aprili naibu mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya CIIE ,aliongoza mkutano wa mtandaoni kutoa ufahamu kwa nchi za Afrika ambazo zinashiriki.
Alisema maonyesho hayo ni muhimu katika kukuza biashara kati ya China na Afrika
Zaidi ya makampuni 450 kutoka karibu mataifa 50 ya Afrika yalijiunga na maonyesho hayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, yakionyesha bidhaa kama vile kahawa ya Kenya, chai ya Afrika Kusini na asali ya Zambia, ambayo ni maarufu miongoni mwa wachina.
Bidhaa za kilimo kutoka kwa waonyeshaji wa Afrika Kusini, kwa mfano, zilipata oda zenye thamani ya dola milioni 210 katika maonyesho ya mwaka jana, kulingana na Zhao Zhongyi ambaye ni waziri mshauri wa ofisi ya kiuchumi na kibiashara ya Ubalozi wa China nchini Afrika Kusini.
Mauzo ya bidhaa za kilimo na nyinginezo kutoka Afrika kwenda kwenye soko la China yameendelea kukua na hivyo kusaidia kusawazisha urari wa biashara.
Taakwimu za Wizara ya Biashara ya China zinaonyesha kuwa Biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kwa asilimia 40.5 katika miezi saba ya kwanza ya 2021, na kufikia rekodi ya juu ya dola bilioni 139.1.
Na Biashara ya China na Kenya ilipata ukuaji wa hadi asilimia 7.2 mwaka 2020.
Naibu waziri wa biashara wa China Qian Keming anasema bidhaa za Afrika zimeendelea kutambulika zaidi katika soko la China, huku uagizaji kutoka Afrika ukiongezeka kwa asilimia 46.3 hadi dola bilioni 59.3 katika kipindi cha Januari-Julai.
Aidha, uagizaji wa mazao ya kilimo kama vile mpira, pamba na kahawa uliongezeka maradufu katika kipindi kama hicho mwaka jana.
Na wakati huohuo Uwekezaji wa Moja kwa Moha wa kiviwanda barani Afrika ulifikia dola bilioni 2.07 kupita viwango vya kabla ya COVID-19 mwaka 2019.
Na thamani ya kandarasi ya miradi mipya iliyotiwa saini na makampuni ya Kichina barani Afrika iliongezeka kwa asilimia 8.2 na 7.8. katika kipindi cha Januari-Julai 2021.
Na ili kusaidia nchi zaidi za Afrika kupata masoko ya bidhaa zao nchini China kupitia maonyesho hayo serikali ya mashirika ya kifedha ya pande mbili yatashirikiana ili kuwezesha nchi zaidi kuendelea kushiriki.
Mkuu wa kitengo cha biashara ya kimataifa kwenye benki ya ICBC ya China Liu Rui anasema benki hiyo itashirikiana na ile ya Standard ya Afrika Kusini kusaidia makampuni zaidi ya Kiafrika kuingia katika soko la China, kupitia shughuli zinazohusiana na maonesho hayo.