Mapadre acheni kuudhalilisha ukatoliki (padre aomba waumini wamchangie milion 90 anunue kluger ya kutembelea

Mapadre acheni kuudhalilisha ukatoliki (padre aomba waumini wamchangie milion 90 anunue kluger ya kutembelea

Huenda wewe ndo umeanza kusikia au kuona Mimi Nina bahasha ya harambee ya kumchangia BabaParoko gari! Nipo kazini nikifika home napiga picha naiweka hapa siogopi mtu Wala nani nikifika nyumbani inapigwa picha inaweka hapa.

Kabla ya harambee WAUMINI walichangishwa Hela na kupewa Gori (kiasi Cha pesa)Kila mtu ambayo ilikuwa 45k. Akaona haitoshi wakasoti watu walio na kazi zao wakatengeneza group wasap wakaweka Gori Tena 100k Kila mtu then Harambe Kwa kuandikiwa barua kabisa na ilifanyika kigangoni.

Ukumbke nyumba tuli mjengea kubwa na ya kisasa kabisa!

Mimi ni Rc lakni Nimeshastuka kitambo naenda mwaka wa7 bila kunusa kanisani uhuni mwingi na utapeli umerudi makanisani.
Wee Kama Mimi[emoji28]
 
Hakuna huo utaratibu na padre haruhusiwi kumiliki mali binafsi. Hapo imetumika lugha ya mafumbo aliposema gari lake anamaanisha "gari la parokia" . Wakati mwingine mapadre wakiomba kuchangiwa labda kwa 'mkono wa kwaheri' au sababu fulani, hiyo pesa huwa hawaitumii kwa matumizi binafsi bali utakuta wanapeleka kutoa misaada au wanapeleka kwenye shirika fulani na huwa hawasemi inabaki mioyoni mwao. Mfano kuna padre aliandika vitabu kadhaa kwa hiyo akaomba waumini wamchangie kununua hivyo vitabu ili apate pesa kidogo, Lakini kumbe baadaye ilijulikana ile pesa yote alipeleka kuchangia kituo maalum cha rehab.
Upo sahihi
 
Hakuna huo utaratibu na padre haruhusiwi kumiliki mali binafsi. Hapo imetumika lugha ya mafumbo aliposema gari lake anamaanisha "gari la parokia" . Wakati mwingine mapadre wakiomba kuchangiwa labda kwa 'mkono wa kwaheri' au sababu fulani, hiyo pesa huwa hawaitumii kwa matumizi binafsi bali utakuta wanapeleka kutoa misaada au wanapeleka kwenye shirika fulani na huwa hawasemi inabaki mioyoni mwao. Mfano kuna padre aliandika vitabu kadhaa kwa hiyo akaomba waumini wamchangie kununua hivyo vitabu ili apate pesa kidogo, Lakini kumbe baadaye ilijulikana ile pesa yote alipeleka kuchangia kituo maalum cha rehab.
Huo ni utasho wa mtu. Utawa wao unawataka waishi kwa kiasi, ila si wote wanajifunga na nadhiri zao, binadamu ni dhaifu!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Unajua mm naenda nje ya Mada ila ntarudi mwishoni,tunajua mapadri hawatumii mikuyenge isipokuwa Kwa kukojoa si ndio?Kwann vatikani wasiweke vigezo kila atakaye upadri aasiwe,na hili litapunguza kashfa ya mapadri kunajisi alter boys.Kuhusu Toyota Kruger nahisi ni too much,kwanza kama ni safari wanagari za parokia,kuhusu misele ya hapa na pale nashauri wanunuliwe punda,viongozi kibao wa enzi hizo walipanda punda.
 
Nimeandika kwa masikitiko makubwa sana nikiwa kama muumin kindakindaki mkatoliki

Miezi miwili iliyopita nilijumuika na waumini wenzangu kwenye misa ya asubuh ndani ya kanisa katoliki lililopo maeneo ya saint carol wilayani sengerema jijini Mwanza

Mamia ya waumini tulijumuika kwenye misa hiyo,

Kitu kilichonishangaza kwenye hiyo ibada ni pale padre alipoomba waumini tumchangie pesa kiasi cha milioni 90 kwa ajili ya kununua toyota kluger ya kutembelea

Padre hakuishia hapo bali aliendelea kwa kutoa utaratibu wa namna gani pesa hiyo itapatikana

Alitoa amri kila kigango kimchangie milioni 1 na pesa nyingine alielekeza namna zitakapopatikana infact nilijiskia vibaya sana na kujiuliza hv wakatoliki kweli tumefikia hatua hii?

Leo hii tena tarehe 10 nimeudhulia misa ya asubuh kwenye kanisa lilelile padre aliongea kauli yenye ukakas sana, kwamba baba paroko amemwagiza amchukulie kiasi cha milioni moja ambacho aliwaomba waumin wamchangie akiwa kwenye ibada siku za nyuma zilizopita

Niliposkia kauli hiyo nilitoka ndani ya kanisa na kuondoka zangu

Sasa swali langu linaenda kwa wale viongozi wa juu wa kikatoliki

Kwanini mmetufanya sisi waumini wenu kama major source of income? Au mnataka tusiwe tunakuja kusali?

Haya mambo kwenye ukatoliki yameanza lini mbona mnajidhalilisha

Na hiyo kluger ya milion 90 ni kluger gan au anataka range?

Tena kaongea kabisa kwamba ameongea na wataalam wa magar wakamshaur gar nzur inayofaa kwa mazingira ya kitanzania ni kampuni ya toyota na wakamshaur anunue toyota kluger ambayo wakampatia na bei tsh milion 90 wakatoliki badiliken mnatia aibu
Mwambieni hamna pesa ila mko tayari kufunga na kumuombea miezi mitatu ili apate hiyo hela…! Maana wao hata sisi tukikosa hela huwa wanasema watatuombea hawatupi pesa! Chamsingi mwambieni mtamuombea awe na imani!
 
Kluger milioni 90? Au kuna toleo jioya silijui? Angeomba hata Rav4 basi..
Kluger ya million 90 ni toleo hili hapa kwa msioifahamu na sio ule mninga wa kisukuma old fasheni.
Screenshot_20231210-173136.png
 
Sasa utaenda kusali wapi kusiko na michango ya kununua magari? Kumbuka kuwa wamisionari waliokuwa wanafanya kazi hiyo siku hizi hawapo na hawaji afrika. Tupo kwenye zama zingine, sisi wenyewe ndio wamisionari tunajenga makanisa na kuwanunulia vyombo vya usafiri viongozi wetu wa kidini
 
Back
Top Bottom