Mapadri na mashehe wanavuta sana sigara. Je, hawajui kuwa hiyo ni dhambi mpya iliyosahaulika kuwekwa kwenye vitabu vitakatifu?

Dhambi ki teolojia sifa zake zipo mfano biblia hakuna mahala imekataza kuvuta bangi .ila sifa kuu ya dhambi huwa ni jambo lolote linalohatarisha maisha yako au ya mwenzako .sigara hufupisha maisha kama ilivyo ulaji kitimoto.kisayansi mvuta sigara anapata madhara madogo ukilinganisha na madhara anayoleta kwa kunukia sigara .kutoa moshi wa sigara hewani kutoa mkojo wenye sumu ya sigara vichakani .mfano asali ya tabora imekataliwa kuingia nchi mbalimbali kwa sababu tu kilimo cha tumbakuu kimezidi hivo nyuki wameweka sumu ya sigara kwenye asali.hivo kuvuta sigara ni kuua .ukiwa unanukia sigara ukakumbatiana n'a mama mjamzito kumsalimu tu kila siku mara 30 hiyo sumu imetosha mama huyo kuzaa taahila .
KUVUTA SIGARA NI ROHO YA SHETANI YA KUPENDA FURAHA YA MUDA BILA KUTOKUWA NA UPENDO WA AFYA YAKO NA ZAIDI AFYA YA BINADAMU WENZIO WANAOKUZUNGUKA .MADHARA YA PAFU LA SIGARA MOJA HUENDA MITA 500 SAWA NA KARIAKOO NZIMA
 
ONDOA KAMBALE, NA KUMBIKUMBI vingine vipo sawa
nguruwe, ngono na pombe umejikataza mwenyewe. Hatujakatazwa.
 
uduwanzi unakutesa. Bangi na nguruwe vinahusika vipi na upuuzi?
 
Point yangu ni kwamba sigara haijatajwa moja kwa moja na hiyo ni loop jole kwa wavutaji,inategemea na tafsirueishi zanzibar mashehe hawagusi pombe kabisa ila sigara wanavuta
Hakuna loophole kwenye mambo ya dini kwasababu dini imejengwa kwenye misingi madhubuti, halafu sio sigara tu vingi tu havijatajwa moja kwa moja ulitaka quran itaje kila kitu kimoja kimoja ni daftari la mahudhurio hilo?.

Mirungi haijatajwa directly na ni haramu, shisha kadhalika, madawa ya kulevya kadhalika na mengine mengi na yote ni haramu kwa mujibu wa kanuni za uislamu.
Hao mashekhe wanaovuta sigara wanafuata matamanio ya nafsi zao na uislamu uko mbali na matendo yao hayo.

Samahani kwa lugha kali kidogo ila sijapenda ulichokifanya kuna watu hutafuta hizi chochoro kutukana dini ya allah pasi na hoja wala ushahidi.
 
Mapadri wanatumia Pombe Kali sana, Kuna nyumba nihamia ila kabla yangu walikuwa wanaishi mapadri.....stoo kulijaa chupa za kila kilevi na Kuna sehemu palijaa vishungi vya sigara yaani utadhani ni danguro vile.........
mapadre na wao huwa wanapanga nyumba mtaani mkuu? hii ndo naisikia leo.
 
Nimewahi kuona padri moja wa kikatoliki raia wa italia akimaliza ibada ya misa takatifu anapanda gari lake kurudi parokiani huku kabugia kiko. Mwingine ni mwalimu wa kiislam wa kipindi cha dini shuleni, huyu alikuwa mkali balaa, akukuta mtoto wa kiislam ameingia kwenye kipindi cha wanafunzi wakristo anaingia hilo darasa kibabe na kutoa mkong'oto mkali kwa watoto wa kiislam. Baada ya kipindi cha dini anawasha sigara na kuanza kuvuta. Kuna viongozi wengine wa dini ni wazinzi balaa
 
Nimekuelewa mkuu tunaelimishana tu
 
Kwa kuwa na cocaïne haijaandikwa kwenye biblia n'a quran nashauri pia waitumie maana vyote vinaharibu afya
 
Kama wametuletea dini na tumezikubali kwa mikono yote hakuna kilee watatuletea tutakataa na vyoye hivyo ni kwa maslahi yao binafsi
 
Mapadri wanatumia Pombe Kali sana, Kuna nyumba nihamia ila kabla yangu walikuwa wanaishi mapadri.....stoo kulijaa chupa za kila kilevi na Kuna sehemu palijaa vishungi vya sigara yaani utadhani ni danguro vile.........
Mapadre Walikuwa wamempanga? Au unataka kutuambia nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…