Aiseeee...
Ndio maana ukipewa mkono wewe jikaushe au jifanye mikono yako michafu, au gonga ngumi...
Ila mkuu kuna mambo mengi sana tu, handles za milango, milango, mabomba kwenye daladala, chenji, milango ya magari, kuokota okota vitu hovyo barabarani, hela tunazopokea na kutoa, matunda kula bila kuosha, PC kwenye internet cafes, lock za milango ya choo, ukiomba pen ya mtu, upandapo kwenye boda lazima utashika mabomba au chochote, ...the list is endless...
Unaweza hata kuwa kichaa kipi ushike kipi usishike, ndio maana kuna watu kunawa mikono kwao ni jadi na kawaida, kila wakati na kila muda...
End of the day mie naona ni kudra za mwenyezi mungu kutuokoa na magonjwa...
Hii thread imenikumbusha tena umuhimu wa kunawa mikono kila wakati, na kuepuka kushika shika watu au vitu..