Mapambano ambayo yapo mbele yako

Mapambano ambayo yapo mbele yako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAPAMBANO AMBAYO YAPO MBELE YAKO!

Anaandika, Robert Heriel

Kabla sijaenda mbali, niseme maisha yanahitaji roho ngumu ya ustahimilivu, bila roho ngumu haya maisha yatakutoa Knockout katika hatua za awali kabisa
Labda niweke hivi;

1. Kuwa hodari na jasiri. Usiwe muoga oga, kwenye maisha huna la kupoteza, usiogope kukabiliana na matokeo. Pambana!

2. Kuwa Mr. Perfect. Amini kuwa kile unachokifanya ndio sahihi. Jiamini, Usiishi Kwa Mitazamo ya wengine.

3. Tambua kuwa kila Eneo katika maisha lina kanuni zake. Lakini isikufanye ukakariri kanuni. Iweke akili yako Flexible.

4. Pigana kufa kupona Kwa ajili ya Familia yako( mke na watoto wako). Usichelewe kuanzisha Ufalme wako(familia yako). Kadiri unavyochelewa kuanzisha familia ndivyo unavyojiwekea mazingira magumu ya kushinda, yaani unashindwa kabla hujaanza. Tumia kanuni ya Goli la mapema au ushindi unatafutwa mapema Kabisa.

5. Usipende kuhairisha mambo uliyoyapanga.

6. Jitahidi kabla wazazi wako hawajafa yaani wangali wa hai, uwafanyie Jambo Fulani ambalo watakushukuru Sana na kujivunia wewe.

7. Kabla hujafika kwenye Mia anzia kwenye sifuri. Usipende kufanya Jambo kubwa ilhali unamtaji mdogo. Anza kidogo kidogo ukiwa na roho ngumu yenye ustahimilivu.

8. Kula, kunywa, vaa vizuri. Muda ni mchache wala hautokutosha. Mipango yako yote isiathiri mambo hayo matatu.Usije sema utakula na kunywa vizuri na kuvaa vizuri nikipata pesa au kazi Fulani. Utakwama! Utakwisha!
Kula ungali unameno, kunywa ungali mdomo bado unaladha, vaa ungali mwili unahaiba nzuri. Muda sio rafiki.

9. Jitahidi kuzaa na kuleta kizazi Bora Duniani. Usiache mbegu zako hovyohovyo.

10. Mche Mungu. Lakini isikufanye ukashindwa kuishi Kwa Raha(Yale uyapendayo kuyafanya) zingatia usifanye Kwa kufuata mkumbo Bali fanya kitu Ile inayotoka moyoni. Hayo ndiyo maisha.

Mapambano ambayo lazima uyapitie
1. Pambano la kukataliwa na watu wengine.

2. Pambano la kujikataa mwenyewe.

3. Pambano la kiuchumi,

4. Pambano la kupigana na muda. Kuona muda unakuacha na huna ufanyalo.

5. Pambano la kukataliwa na Familia yako mwenyewe. Hasa Mkeo.

6. Pambano la kuukabili ukingo WA maisha yako

Silaha unazotakiwa kutumia;

1. Utulivu
2. Shukrani na kuridhika
3. Ustahimilivu na Subira
4. Timing na ambush za kiintellejensia
5. Courage na mtazamo chanya.
6. Selection na Categorization makini ya wanaokuzunguka

Nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Usikubali mtu mwengine akwambie yupi anafa kuwa mkeo na yupi hafai kuwa mkeo fata uamuzi wako. Usitegemee ndugu jamaa wawe wafariji/uwategemee kwenye maisha yako. Tafuta hela kwa njia halali usi dhulumu wala usikubali kudhulumiwa. Achana na wanafiki kaza buti tafuta mafanikio unafiki hauleti mafanikio unalete utengamano.
 
Usikubali mtu mwengine akwambie yupi anafa kuwa mkeo na yupi hafai kuwa mkeo fata uamuzi wako. Usitegemee ndugu jamaa wawe wafariji/uwategemee kwenye maisha yako. Tafuta hela kwa njia halali usi dhulumu wala usikubali kudhulumiwa. Achana na wanafiki kaza buti tafuta mafanikio unafiki hauleti mafanikio unalete utengamano.

Umeongeza finyango yenye mnofu
 
Mkuu barikiwa Sana ,,maandiko yako yamenifanya nibadili mtizamo na kuwa Mwanaume mwingine kabisa.
 
Usiogope jela tu, theres a thin line kati ya kufanikiwa na kwenda jela.
 
Mkuu kama itakupendez maelezo kidogo pale
No.4 ...Timing na ambush ya kiintelejensia.
 
Uzi mujarabu kabisa tokea sebuleni kwa shemeji yako 🤣✌
 
Back
Top Bottom