Akiongea kwenye kipindi
cha Hoja ya Mwalimu Lwaitama kilichorushwa na SIBUKA TV leo Ijumaa
06-09-2013,Dr Lwaitema amesema kuwa wabunge wa vyama vya upinzani
wanajaribu kuizuia CCM kuhodhi Bunge la katiba."CCM inao wabunge zaidi
ya robo tatu kwenye Bunge la muungano,lakini tatizo lipo kwenye Bunge la
wawakilishi,CCM hawafikii robo tatu ya wajumbe, kwahiyo, CCM wanataka
watumie nafasi aliyopewa Raisi kuteua wajumbe 166,kuziba pengo
hilo,wamepitisha apelekewe majina tisa kwa kila asasi halafu yeye
atateua mmoja anayemtaka ambaye lazima akubaliane na ajenda za CCM"
amesisitiza Dr Lwaitama.
Ameongeza kuwa,yapo mapendekezo mengi ya kamati ya Warioba ambayo
wananchi wameyafurahia sana lakini CCM hawayaafiki kabisa.Baadhi ya
mambo ambayo Dr Lwaitama amesema CCM hawataki kabisa yawemo kwenye
katiba mpya ni;
- CCM hawataki serikali tatu,wanataka serikali mbili.
- CCM inataka mawaziri waendelee kuwa wabunge.
- CCM haitaki wabunge wanawake wachaguliwe,wanataka viti maalum
viendelee ili wawaweke ndugu zao.
- CCM haitaki haki za binadamu ziingizwe kwenye katiba mpya.
- CCM inataka majaji waendelee kuteuliwa na Raisi.
- CCM hawataki madaraka ya Raisi yapunguzwe.
- CCM haitaki maadili ya viongozi yawemo kwenye katiba mpya. n.k.
Wapinzani wanajua kuwa kama Bunge la katiba litatawaliwa na wana CCM,
mambo yote yaliyotajwa hapo juu na mengine wasiyoyapenda wana CCM
yataondolewa kwenye rasimu ya katiba,na hivyo ndoto ya watanzania kupata
katiba mpya itakuwa imeyeyuka kabisa. Katiba haitakuwa mpya
tena,itakuwa ileile ya zamani kwenye jalada jipya,itakuwa sawa na kuweka
divai ya zamani kwenye chupa mpya. Ndio maana wapinzani walitaka idadi
ya wajumbe wasio wabunge iwe 400 na wachaguliwe na asasi husika sio
Raisi.Wapinzani wamekubali kudhalilika ili kuwafumbua macho watanzania
kuwa yale yote yaliyofanywa na kamati ya Warioba na kupendwa na wananchi
yapo hatarini kutoweka.
Ndugu wana JF, hivi kweli kwa mswada uliopitishwa leo unaweza kuua ndoto
zetu za kupata katiba mpya? Je, pendekezo lililopitishwa kuwa vipengele
vya katiba vinaweza kupitishwa na wingi wa wajumbe bila kujali wanatoka
wapi inaweza kuwa ni mbinu ya CCM kuhakikisha mambo hayo saba hayaingii
kwenye katiba mpya? NAWASILISHA