Mapambano bungeni ni dhidi ya ajenda mahususi ya CCM ya kuhodhi Bunge la Katiba-Mwl Lwaitama

Mapambano bungeni ni dhidi ya ajenda mahususi ya CCM ya kuhodhi Bunge la Katiba-Mwl Lwaitama

Unajiita Geniusbrain????? Am not sure na ulicho andika hapa kama kina ugenius ndani yake its just a peace of rubbish. ...possibly ugenius wa JOGOO akisha kuwa mkubwa analala na mama yake.... nao pia ni ugenius.......shame.

Hakuna jipya kwenye haya uliyoyaeleza, tumeisha yasikia sana kwa viongozi wako. Na Lwaitama anajulikana kwa kupayuka na kutotumia udokta wake kufikiri. Hivyo hitimisho la thread uliyoileta twaweza sema ni thread ya craaaaaaaaaaaaaaaaaap.
 
Hakuna jipya kwenye haya uliyoyaeleza, tumeisha yasikia sana kwa viongozi wako. Na Lwaitama anajulikana kwa kupayuka na kutotumia udokta wake kufikiri. Hivyo hitimisho la thread uliyoileta twaweza sema ni thread ya craaaaaaaaaaaaaaaaaap.

Jina lenyewe ni ---- - GeniusBrain. Kinachotoka humo ni ---- kupita maelezo. Undhani font kubwa ndio ushawishi? Hoja yenye nguvu hata ikiwa na font size ya kawaida itafika tu. Basura!
 
Ndiyo maana MACCM HAWAPENDI WASOMI WAKWELI KABISA ILA WANAWAKUMBATIA WAPUMBAVU MF MWIGULU.
 
Kwani nani angeweza kuamini Gadafi angeondolewa madarakani?Vivyo hivyo kwa ccm.Wazungu wanasema "It is just a matter of time"
 
Mkuu umeongea pointi
Akiongea kwenye kipindi
cha Hoja ya Mwalimu Lwaitama kilichorushwa na SIBUKA TV leo Ijumaa
06-09-2013,Dr Lwaitema amesema kuwa wabunge wa vyama vya upinzani
wanajaribu kuizuia CCM kuhodhi Bunge la katiba."CCM inao wabunge zaidi
ya robo tatu kwenye Bunge la muungano,lakini tatizo lipo kwenye Bunge la
wawakilishi,CCM hawafikii robo tatu ya wajumbe, kwahiyo, CCM wanataka
watumie nafasi aliyopewa Raisi kuteua wajumbe 166,kuziba pengo
hilo,wamepitisha apelekewe majina tisa kwa kila asasi halafu yeye
atateua mmoja anayemtaka ambaye lazima akubaliane na ajenda za CCM"
amesisitiza Dr Lwaitama.


Ameongeza kuwa,yapo mapendekezo mengi ya kamati ya Warioba ambayo
wananchi wameyafurahia sana lakini CCM hawayaafiki kabisa.Baadhi ya
mambo ambayo Dr Lwaitama amesema CCM hawataki kabisa yawemo kwenye
katiba mpya ni;

  1. CCM hawataki serikali tatu,wanataka serikali mbili.
  2. CCM inataka mawaziri waendelee kuwa wabunge.
  3. CCM haitaki wabunge wanawake wachaguliwe,wanataka viti maalum
    viendelee ili wawaweke ndugu zao.
  4. CCM haitaki haki za binadamu ziingizwe kwenye katiba mpya.
  5. CCM inataka majaji waendelee kuteuliwa na Raisi.
  6. CCM hawataki madaraka ya Raisi yapunguzwe.
  7. CCM haitaki maadili ya viongozi yawemo kwenye katiba mpya. n.k.

Wapinzani wanajua kuwa kama Bunge la katiba litatawaliwa na wana CCM,
mambo yote yaliyotajwa hapo juu na mengine wasiyoyapenda wana CCM
yataondolewa kwenye rasimu ya katiba,na hivyo ndoto ya watanzania kupata
katiba mpya itakuwa imeyeyuka kabisa. Katiba haitakuwa mpya
tena,itakuwa ileile ya zamani kwenye jalada jipya,itakuwa sawa na kuweka
divai ya zamani kwenye chupa mpya. Ndio maana wapinzani walitaka idadi
ya wajumbe wasio wabunge iwe 400 na wachaguliwe na asasi husika sio
Raisi.Wapinzani wamekubali kudhalilika ili kuwafumbua macho watanzania
kuwa yale yote yaliyofanywa na kamati ya Warioba na kupendwa na wananchi
yapo hatarini kutoweka.

Ndugu wana JF, hivi kweli kwa mswada uliopitishwa leo unaweza kuua ndoto
zetu za kupata katiba mpya? Je, pendekezo lililopitishwa kuwa vipengele
vya katiba vinaweza kupitishwa na wingi wa wajumbe bila kujali wanatoka
wapi inaweza kuwa ni mbinu ya CCM kuhakikisha mambo hayo saba hayaingii
kwenye katiba mpya? NAWASILISHA
 
Hakuna jipya kwenye haya uliyoyaeleza, tumeisha yasikia sana kwa viongozi wako. Na Lwaitama anajulikana kwa kupayuka na kutotumia udokta wake kufikiri. Hivyo hitimisho la thread uliyoileta twaweza sema ni thread ya craaaaaaaaaaaaaaaaaap.

Mbowe na Sugu mnasema hawana hoja mkisingizia elimu yao ndogo, haya huyu naye hatumii udokta wake kufikiri.hatuwaelewi nyie watu
 
mbowe na sugu mnasema hawana hoja mkisingizia elimu yao ndogo, haya huyu naye hatumii udokta wake kufikiri.hatuwaelewi nyie watu

acheni upumbavu.hivi ninyi ni watanzania?kati ya hayo yaliyotajwa hapo juu,ni mtanzania gani asiyeyapenda?au mnadhani upinzani wanakubali kudhalilika kwa maslahi ya nani kama si watanzania?
 
Hakuna jipya kwenye haya uliyoyaeleza, tumeisha yasikia sana kwa viongozi wako. Na Lwaitama anajulikana kwa kupayuka na kutotumia udokta wake kufikiri. Hivyo hitimisho la thread uliyoileta twaweza sema ni thread ya craaaaaaaaaaaaaaaaaap.

haya maneno hayana msingi.mleta thread ana uhuru wa kueleza mawazo yake hata kama huyapendi ,
acha wengine wajadili maana inaonekana huna la kusema bali unataka tukusome tu.
kama huna comment kaa kimya si lazima ujibu.
 
Mimi nadhani nia ya CCM imekuwa wazi hata kabla ya mchakato wa kuandika katiba mpya haujaanza. Tukumbushane haya yafuatayo kwa ufupi:-
  • Katika mpya haikuwemo kwenye manifesto ya CCM iliyotumika kuomba kura kwa wananchi mwaka 2010;
  • Mwanasheria Mkuu wa serikali alisikika akisema hakuna haja ya kuandika Katiba mpya kwani kwa mtazamo wake hii iliyopo inakidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya nchi. Sana sana alikuwa akiongelea mabadiliko ya vipengele vichache vya katiba kuihuisha iendane na wakati;
  • Waziri wa sheria wakati huo Bi selina Kombani naye alisikika akitoa msimamo unaoshabihiana na wa mwanasheria mkuu kuwa hakuna haja ya Katiba Mpya.
  • Aliyekuja kubadilisha upepo wa mambo ni Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya muungano ambaye alitoa fursa kwa katiba mpya kuandikwa - na sikumbuki iwapo jambo hili lilijadiliwa kwenye vikao vya CCM kabla mwenyekiti wao hajatoa tamko la kuanza kwa mchakato wa katiba mpya.
  • Hata ulipotokea mgogoro baina ya wabunge wa CCM na wale wa upinzani bungeni kuhusu muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ni Mwenyekiti wa CCM ndiye aliyechukua initiatives za kukutana na wapinzani na wadau wengine na hatimaye kuurudisha muswada ule kwa marekebisho.
Hivyo ninaweza nikasema kwa usahihi kabisa kuwa wazo la katiba mpya halikuwa la CCM kama chama bali lilikuwa la Mwenyekiti wao. Kila mara bunge la Jamhuri lilipopata nafasi ya kupitisha sheria zinazohusiana na Katiba CCM wamekuwa mstari wa mbele kupoka hatamu ya mabadiliko ya Katiba ili kuingiza matakwa yao ya kichama. Hata hizi juhudi za sasa za CCM kuuteka mchakato wa bunge la Katiba ni muendelezo tu wa zile kauli za viongozi waandamizi wa serikali akiwemo mwanasheria mkuu wa serikali na waziri wa sheria wa wakati huo kuwa Tanzania hatuhitaji katiba mpya.
 
Dk anatukumbusha tu kuwa katiba mpya haikuwa ajenda ya CCM sio jana wala leo
 
Back
Top Bottom