#COVID19 Mapambano dhidi ya COVID-19: Rais Samia anayo dhamira ya kweli? Kinachoendelea India kinatisha

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Hivi ni kweli kabisa Rais Samia ana nia ya kweli ya kupambana na COVID-19?

Sijui kama na nyie mnafuatilia yanayoendelea huko India sasa hivi!

Akina Narendra Modi walikuwa huko West Bengal wanapiga kampeni za kisiasa utadhani hamna kesho. Ona sasa kilivyoumana.

Sasa kweli hiyo kamati aliyoiunda Rais Samia ili imshauri kuhusu corona ndo imemwambia kwamba ni sawa tu watu kwenda na kurundikana hapo uwanja wa Kirumba namna hiyo?

Ona hata hapo walipokaa hao viongozi! Hakuna social distancing. Hakuna barakoa. Hakuna tahadhari yoyote ile ya maana.

Hahahaaaaa…..what is this?

 
Mkuu naungana na wewe kuhusu hili,Mama kama hajijali basi ajue yeye Raia namba moja, jambo lolote kuhusu yeye ni lenye maslahi mapana kwa Taifa.

Hivi hawaoni wazee wanampa ishara, wote wanavaa barakoa kwenye shughuli au anataka mpaka wamwambie kwa mdomo aseme wanawashwa.
 
Kila mtu alimuona Mpango alivyokuwa anakohoa siku ile amefanya press conference baada ya kutoka hospital; huyu bwana aliponea chupu chupu lakini hata baada ya kupona corona bado havai barakoa wala hakai mbali na wenzie to social distance!! Hii ni hatari sana hasa kwa viongozi wenzie anaokutana nao kila siku!! Try to social distance, hata hao walinzi wa Rais pia wajitahidi kukaa mbali ,sometimes wanaonekana kuwa karibu sana na Rais na haijulikani wanakolala!!!
 
Sasa kamati ya Samia ya nini?
Ni katika utaratibu ule ule tuliouzoea, mama amekuwa mbobevu wa NGOs. Anawafurahisha wale wenye platform ya kusikika kwa manufaa ya wapiga dili.

Nani mwingine umemsikia anazungumzia korona au vifo vya korona tangu awepo yeye.

Tuliambiwa ile Marathon ya Kili itajibu, tukatishiwa kuwa baada ya maziko ya Mwamba tutaelewa sayansi ya barakoa, mechi za simba na yangu, Mkapa ilijaa yote tukaambiwa tutaokota kama kumbi kumbi.

Leo wooote kimya.
 
Covid 19 Tz ni mafua tu. Usihofu mkuu, sisi huku hata kukumbuka hiyo hatukumbuki. Maisha yanaendelea. Sasahivi wafanyakazi wanasubiri maneno kutoka kwa mama (hotuba).

Kazi Iendelee
 
Mkuu inawezekana kamati haijapata majibu.
 
Rais Samia alisema keshaunda kamati ya corona!

Hiyo kamati ndo imemshauri haya mambo ya mikusanyiko ya watu wengi hivi iendelee?

She is not serious about!

Naona alisema kaunda hiyo kamati kuwaridhisha tu baadhi ya watu.

Maana haiingii akilini kabisa…
 
Covid 19 Tz ni mafua tu. Usihofu mkuu, sisi huku hata kukumbuka hiyo hatukumbuki. Maisha yanaendelea. Sasahivi wafanyakazi wanasubiri maneno kutoka kwa mama (hotuba).

Kazi Iendelee
Oh yeah?

Kwa hiyo corona si changamoto za upumuaji tena?
 
Tutumie chanjo za AstraZeneca sisi tunaotaka chanjo.
 
Kila taifa lipo duniani kwa sababu. Sio kila kinachowakuta wengine kitukute na sisi, Mungu wetu yupo hai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…