Nimemzika rafiki mmoja aliyefariki Corona, alikuwa mwumini hodari sana. Nadhani kwa jumla hao
masista zaidi ya 50 Wakatoliki waliofariki Januari-Februari mwaka huu wote walisali saaana,.
Hakuna dalili hata kidogo kwamba Tanzania ina pungufu ya vifo kuliko tuseme Kenya, isipokuwa kuficha kwa data.
Kuficha data ni sawa na kufunga macho. Ukifunga macho ni rahisi kusema "Sioni kitu". Hongera!!
Madai yako Uhindi wamepiga chanjo kuliko nchi nyingine ni mfano wa kufunga macho. Hadi mwisho wa Aprili 2021 walitoa chanjo milioni 155 hivi (154,989,635; takriban mil. 25 kati yao walipokea zote mbili, wengine mara ya kwanza tu) ambayo ni idadi kubwa LAKINI
si kubwa ukilinganisha na idadi ya watu wao. Maana
wote ni BILIONI 1.3, hivyo ni asilimia ndogo. Je unaweza kukadiria mwenyewe? (nikuambie siri: 11% jumla,
chini ya 2% waliokamilika) .
Halafu barakoa? Wana mamilioni wenye umaskini mkali hawana barakoa.
Nchi iliyofaulu kuliko zote ni China. Kwa nini? Kwa sababu wanasali? Hapana,
wanatisha Wakristo na kuhubiri atheism. Wamefaulu kwa sababu ya kuchukua hatua kali za kidikteta na kutisha watu kila mahali, pamoja na nidhamu ya ajabu.
Usipotaka police state ya kiatheisti una chaguo:
- ama kufunga macho na kudai eti huoni kitu
- au kuchukua tahadhari, kubana shughuli kadhaa zisizokwamisha uchumi (kufunga vilabu, kuweka mipaka ya mikutano), halafu chanjo, chanjo, chanjo