Nakumbuka sana ulivyokuwa unamsifia Magu na sera zake za porini za covid. Uliwazodoa sana CHADEMA walipokuwa wanasisitiza standard measures ambazo umezigusia. Nini kimebadilika mkuu? Si ingefaa sera za nyingi ziendelee?
Hata Magu alipowazodoa wanaovaa Barakoa na kutamba kwamba yeye na wasaidizi wake, mkaona ni poa tu. Vipi tena?
Nilimsifia Magufuli kwa mambo matatu [kuhusu corona].
1. Consistency [bila kujali matokeo].
2. Kutenda kama alivyokuwa akisema.
3. Kutokuwafungia watu ndani [‘rockdown’].
CHADEMA, Zitto, na wenzao niliwazodoa kwa kutokuyatenda waliyokuwa wanayahubiri hususan mitandaoni.
Hao jamaa zako walikuwa wanachonga madomo yao ili wajipatie pointi za kisiasa tu.
Tundu Lissu alirudi nchini kavaa barakoa. Baada ya kutoka tu uwanja wa ndege akaivua na kuitupilia mbali hiyo barakoa!
Uongo?
Tokea hapo, akiwa Tanzania sikumwona tena akiwa amevaa barakoa wala kuzingatia tahadhari zingine kama kuepuka misongamano.
Alizurura nchi nzima akipiga kampeni zake za urais bila kuvaa barakoa! Hakuepuka misongamano. Alishikana mikono na watu.
Waone hapa Tundu Lissu, Zitto Kabwe, na huyo aitwaye au ajiitaye Shangazi [Fatma Karume] wakiwa kwenye mkutano wa ACT.
Hakuna cha barakoa. Hakuna kuachiana nafasi. Hakuna kutokushikana mikono. Hakuna kutokukumbatiana.
Hao ndo watu waliokuwa mstari wa mbele kumnanga Rais Magufuli kwa kuipuuzia corona ilhali wao wenyewe hawachukui hata hizo tahadhari za msingi za kujikinga.
Sasa nije kwa huyu Rais Samia.
Keshasema kuwa keshaunda sijui ni kamati ile au sijui ni tume na alituambia ishaanza kufanya kazi.
Kama anakubali kuwa corona ipo kiasi mpaka cha kuiundia tume, inakuwaje sasa yeye mwenyewe kama kiongozi wa nchi asionyeshe mfano kwa matendo katika walau uzingatiaji wa zile tahadhari tu za msingi kama kuvaa barakoa na kuepuka misongamano na mirundikano ya watu?
Wewe huoni kama matendo yake hayaendani na maneno yake kama ilivyokuwa kwa hao rafiki zako wa CHADEMA?
Kwa mara kwanza mimi nimemwona kavaa barakoa alipoenda Uganda ile majuzi. Aliporudi akaitupilia mbali na sijamwona tena akiwa kaivaa.
Nimeona sehemu kuwa ataenda Kenya hivi karibuni. Akiwa huko nadhani ataivaa tena.
Mpende Magufuli au umchukie, jambo ambalo huwezi kusema ni maneno yake hayakuendana na matendo yake, ni hili la corona.
Rais Samia na hao rafiki zako wa CHADEMA, matendo yao na maneno yao kuhusu corona, hayaendani!
NB: Kuhusu Magufuli kuwazodoa waliokuwa wanavaa barakoa, ukweli ni kwamba nilisema, na siyo mara moja, kwamba anakosea. He was mask-shaming people. I called him out on it numerous times. Fact.
Don’t half-step when you come at me. Come correct, lest I’ll leave you in the dirt.