Mapambano dhidi ya Ufisadi - wapi tunafanya makosa?

Mapambano dhidi ya Ufisadi - wapi tunafanya makosa?

Ivi tunashindwa kusema kuwa rushwa inatokana na ujinga (ignorance)? kama wewe hujui sheria, polisi hataacha kukusimanga? Kama wewe hujui matumizi ya pesa za umma, wabunge, BOT, rais nk hawataacha kuziiba? Kama wewe hujui kodi katika biashara yako, TRA hawataacha kukusimanga?
Mkapa alikuwa na motto ya 'Ukweli na Uwazi', lakini sidhani kama aliweza kuitimiza. Tukiweza kuondoa ujinga, tutaweza kuishi ndani ya ukweli na uwazi hivyo kupunguza rushwa kwa asilimia kubwa. La kusikitisha hata baba wa taifa baada ya kutaja ujinga kuwa adui wetu, alitumia huo huo ujinga kututawala na hivyo kuuendeleza.
 
1. A Critique of the History of Combating Corruption in Tanzania

- It is ironical that the 1967-1985 period was the period of emergency and wide spread corruption. A critical analysis of the reasons for this will show that corruption rose not because of the certain economic developments negatively affecting the performance of the economy, but rather because selfishness of the leaders took advantage of the suffering of the people. Those with power and influence, rather than living simply so that others might simply live exploited to the full the situation. For that reason it was too late for the government in 1982 to declare war on corruption and other forms of bribery. Also the manner of combating corruption was charged with political emotions and ideological apartheid. It is true that number of corruption cases decreased on the average (Maliyamkon & Bagachwa 1990); but this actually drove underground the practice, and so the spirit was still alive!


Does this by any chance link to the death of Sokoine?
 
'Ukweli na Uwazi', lakini sidhani kama aliweza kuitimiza. Tukiweza kuondoa ujinga, tutaweza kuishi ndani ya ukweli na uwazi hivyo kupunguza rushwa kwa asilimia kubwa. La kusikitisha hata baba wa taifa baada ya kutaja ujinga kuwa adui wetu, alitumia huo huo ujinga kututawala na hivyo kuuendeleza.

Mtoto, Umegusia kitu muhimu sana.
Ukweli humweka mtu huru kuhoji....... kujitetea.
Uwazi humfanya mtu kujua nini kinaendela.... humfanya mtu ashindwe kufanya vitu ambavyo havikubaliki.
Rushwa huchangiwa na ujinga kama ulivyosema na pia mambo kufanywa kwa kificho.
Corruption= Accountability- Transparecy +Discretion
( C= A-T+D)
Yaani kunapokosekana Uwajibikaji na Uwazi na kukawepo na hali ya mtu kutumia madaraka apendavyo hapo kunakuwepo na rushwa.
 
=Mkandara;537491]Field Masrshall Es,
Unaweza wadanganya wengine lakini sii mimi mkuu wangu...
Unajua kinachotufanya tuwe NDIVYO TULIVYO ni kutokana na kutozungumzia chimbuko la matatizo yetu badala yake tunazungumzia matatizo yenyewe na kuvuta hisia zetu..Na unaweza kuweka majina yoyote yale ila cha msingi ni hoja yenyewe inalenga wapi..
- Tunachojaribu hapa ni kuelimishana kwa kujumlisha maoni tofauti, kwangu chimbuko la ishu ya rushwa ni sisi wananchi wenyewe wa Tanzania sio viongozi au chama kama wengi tunavyodai, na nimeweka mifano yangu kwamba hili ni taifa lenye wananchi wa ajabu sana na sababu nikaziweka.

Tunakusoma..
Wewe na mtu mwingine yeyote yule anajua fika kwamba Ditopile kapewa dhamana sii kwa sababu ni Muislaam ila kwa sababu ni mtu wenu CCM. hata angekuwa Mkristu au Baniani maadam ni mshikaji wa JK na mwenye wadhifa ndani ya chama hicho asingeweza kukaa ndani..Iwe Mwadosya, Kingunge, Masha au Lowassa.. wote hawa wanapewa kinga na chama chako..That's the bottom line.
- Nimesema sisi wananchi wa Tanzania ni ajabu sana na hatuna mfano dunia nzima, na mfano mmojawapo ni kwamba Marehemu Ditopile aliua kwa kutumia Bastola, mbele ya public na tena kwa makusudi mazima, lakini akaachiwa kwa dhamana, Mtikila akaamua kutaka kumshitaki ili arudishwe rumande, wakatokea wananchi flani siwajui dini wala zao wala kabila zao, wakadai kwamba Mtikila asiingilie dini ya Ditopile, kwa sababu kitendo chake cha kutaka kufuata sheria kinaingilia dini ya Ditopile, How? Labda unisaidie mkuu, sasa ninasema hivi hivi wananchi wa namna hii unawasaidiaje kuondokana na rushwa? au uongozi mbovu pamoja na ufisadi?

- Hii ndio tafsiri yangu na sio maneno mengi uliyoyaweka hapo juu, I have nothing to do with.


Sasa unapozungumzia waislaam ambao walisimama for Ditopile kumbuka hata aliyeuawa ni Muislaam. Wapo waislaam na Wakristu waliopingana/waliounga mkono na dhamana ile. Hakimu aliyetoa dhamana sii Muislaam wala Prosecutor wake na haikuwa sababu hata kidogo.. Hivyo kitu cha kulaumu kwa pamoja ni mfumo mzima wa sheria nchini ambapo tunawaona viongozi hasa wa CCM wakisimama juu ya sheria..
- Nimesema waliomtishia Mtikila sijui dini wala kabila zao, kwa hiyo hapa mkuu haya hayanihusu.

Katika kesi ya jinai yoyote ile wapo watu watakao kuwa upande wa pili na sii wajinga ila ndivyo sheria inavyojengwa..Till proven Guilty au sio.. hata kama alikusudia kuua ni kazi ya mahakama..
Mkuu wangu hata Mapadre hufanya maovu na kanisa likasimama kuwatetea, hii haina maana wao wajinga ila wanafuata kinga za kanisa lao kutokana na wadhifa wa mhusika. Na hadi itakapo kuwa proven ndipo kanisa humtema mtu huyo. Tumeona kina Lowassa na Rostam wote hawa wakipewa kinga na wapo watu wanamuunga mkono jambo ambalo mimi binafsi siwezi kutumia dini ya mhusika kuonyesha ujinga wa wafuasi wa dini hiyo wala haiwezi kuwa kielelezo cha haki..Ya Masha ya Nchimbi umewazungumzia wao ktk kujenga ukubwa wa matatizo tulokuwa nayo..hivyo kesi yao haihusiani na zile zilizotangulia...
- Nimesema Masha na Nchimbi, ni another joke ya sisi wananchi wa Tanzania, maana tumelia sana kwamba hatutaki viongozi wazee, tunataka vijana kama hawa ambao wame-prove kwamba ni bora wazee, lakini watch uchaguzi unakuja tutawachagua anyways, halafu tutakuja kulia lia tena kwamba rushwa ni ya viongozi na CCM, hayo mengine yote hayanihusu wala hayahusu hoja yangu mkuu.

Mkuu wangu nawaombeni sana, jaribuni sana kuondokana na swala la ku lebel watu wakati wakidai haki zao hata kama haileti maana kwako..Umezungumzia pia mahakama ya kadhi.. Ni mtazamo wako ambao binafsi sioni kosa wala ubaya wa hoja hiyo kwani hapa Wahindi Masingasinga wamepewa sheria yao kutembea na majambia yao wakati hairuhusiwi kwa mtu asiyekuwa na imani ya dini hiyo..

Nitazidi kusema kama unapingana na mahakama ya kadhi zungumzia vilivyomo ambavyo wewe hukubaliani navyo na sii kutumia jina la dini kupinga..kwani kufanya hivyo unapingana na mtazamo wa diversity..
- Kwenye hili Bob, msimamo wangu nauweka wazi kwamba wananchi wanaolilia maneno ya Kadhi leo 2009, hawawezi kabisa kulisaidia taifa lao kwa anything, nikasema hivi hata Iran wenyewe wanaojua sana hayo mambo sasa hawayataki tena, sasa sisi kulikoni? Zingekuwa sheria zetu Tanzania zinafanya kazi ipasavyo sio vibaya ku-extend uungwana kwa kikundi flani katika jamii na sheria za dini yao, lakini wewe unajua kuwa sheria zetu zimetupwa nje, wananchi wenye akili timamu na safi na wanaolijali taifa lao, watalilia sheria za jamhuri kusimamiwa na kutumika sio kudai extention ya sheria za kidini, hawa ni wananchi wasioelewa kitu ndio maana rushwa itashamiri milele na milele, that is my point.


Tupambane na Ufisadi kwa kutazama kiini chake, tusiwe na fdikra kama za viongozi wenyewe ambao hata kupambana na Maleria tu imetushinda wakati wakijua fika kwamba chanzo chake ni mbu kuzaliana ktk madimbwi ya maji yaliyosimama..walichofanya ni kuomba vyandarua na dawa nyingi sana za kutibu Maleria..Watu wanazidi kufa kwa hesabu kubwa kuliko wakati wowote uliopita!
Beside that It's all good!
- That is my point kwamba sisi wananchi ndio chanzo cha rushwa na ufisadi, sio viongozi wala chama chochote cha siasa, samahani sana kwamba hoja zangu zimakukwaza kidini yako yaani Islam, mimi wala sikufika huko na hoja zangu ziko wazi kabisa, lakini pole sana anyways!, siwezi kusema eti Waisilamu ndio wanaturudisha nyuma Tanzania, huo utakuwa ni ubaguzi wa wazi sana, I am not like that mkuu, maana marafiki zangu wengi wa karibu na wewe included ni wa kutoka dini hiyo, ya dini na rushwa hayaingiliani kabisa mkuu.

Respect.

FMEs!
 
Ivi tunashindwa kusema kuwa rushwa inatokana na ujinga (ignorance)? kama wewe hujui sheria, polisi hataacha kukusimanga? Kama wewe hujui matumizi ya pesa za umma, wabunge, BOT, rais nk hawataacha kuziiba? Kama wewe hujui kodi katika biashara yako, TRA hawataacha kukusimanga?
Mkapa alikuwa na motto ya 'Ukweli na Uwazi', lakini sidhani kama aliweza kuitimiza. Tukiweza kuondoa ujinga, tutaweza kuishi ndani ya ukweli na uwazi hivyo kupunguza rushwa kwa asilimia kubwa. La kusikitisha hata baba wa taifa baada ya kutaja ujinga kuwa adui wetu, alitumia huo huo ujinga kututawala na hivyo kuuendeleza.

- Ni ujinga ndio unatusumbua wananchi wa Tanzania, that is the word, hakuna cha kuongeza.

Respect.

FMEs!
 
Hatuwezi kupambana na ufisadi kwa kuwa

1) Sisi ni waoga, kwa ujumla wetu

2) Hakuna aliye tayari kujitoa muhanga, kufichua siri za mafisadi

3) Anayefichua siri anaonekana msaliti, hata kwa yule ambaye anawachukia mafisadi

4) Hatuna umoja wala uzalendo wa kukubali kwamba hii ni nchi yetu, na kwamba mafisadi hawana nafasi ya kuendelea kuimaliza nchi hii

5) Hatujaamka kifikra, na kuanza kuhoji: Nani kafanya nini, kwa ajili ya nani, kwa ruksa/ridhaa ya nani?

6) Tunaogopa mabadiliko, tumezoea shida tulizonazo, tunadhani mabadiliko yatatupeleka pabaya...

Ni hayo tu.

Ufisadi utadumu, mpaka pale ambapo tutaona uchungu wa kuibiwa, na kuamua kuufanyia kazi!

Madini yanachotwa, pesa zinahamishwa, mali asili zinaporwa, bado tuko kimya? Kwenye halmashauri, ushuru unaotozwa mitaani unaishia mifukoni mwa wachache. Bado tuko kimya?

Niseme nini mpaka mnielewe? Ufisadi si wale wanaoiba BOT na kwenye mashirika makubwa, ufisadi upo hata kwenye ofisi za Wenyeviti wa Mitaa! Kwenye sekta binafsi usiseme!

Yaishe, kwa leo, lakini siogopi, ntasema tu!

Wenye kujua uchafu wa mafisadi, uanikeni, hatutaki majina yenu, tunataka DATA!
 
Mimi tofauti na wengine wengi naliona tatizo la rushwa kama mavuno ya zao lililopandwa na CCM, likapaliliwa na kuvunwa na CCM. Hivi sasa hayo mavuno yamehifadhiwa kwenye maghala ya CCM na hugawiwa kwa wananchi kama vile chakula cha msaada nyakati za njaa. Mwananchi analazimika kupokea huo msaada kwa sababu vinginevyo ni kufa tu na CCM kwa upande wake wanautumia huo msaada kama silaha ya kuwabana na kuwafunga wananchi.

Kwa nini nasema hivi - ni kwa sababu itikadi ya kisiasa iliruhusiwa kutawala nyanja zote za maisha. Hungeweza kufanikiwa kwa lolote iwe kazi, biashara au shughuli yoyote ya kijamii bila kuwa na kadi ya CCM. Ajira serikalini hadi kwenye mashirika ya umma ilitegemea ulikuwa mkereketwa hata kama hukubaliani na itikadi hiyo. Matokeo yake unafiki ulishamiri kwa kiwango cha kutisha na haikuwa tena rahisi kwa mwananchi hata kufikiria maisha nje ya CCM.

Unafiki ulizaa ukondoo na vyote viwili vikawa kama rutuba kwa maisha ya udanganyifu na ujanja ujanja. Bidii na ufanisi ziliwekwa kando na njia za mkato za kujitayarisha zikarindima na hivyo milango ya rushwa ikawa imefunguliwa. Waomba uongozi ilibidi watoe takrima na wanaotafuta huduma wahakikishe wametoa kitu kidogo. Siyo polisi, muuguzi, karani, dereva n.k. - gonjwa halikuchagua na taifa likajikuta limezama kwenye dimbwi la rushwa.

Kiwango cha rushwa Tanzania kinatisha na mpaka hapo mzizi wa fitina,CCM, utakapong'olewa, juhudi zozote za kuutokomeza ni vigumu kufanikiwa. Hatuwezi kutegemea watu wale wale, uongozi ule ule na nguvu zile zile zituletee matokeo tofauti - hapana, itakuwa ni ujinga mkubwa na tutakuwa tunajidanganya kama tulivyofanya kwa miaka 48. Ni mabadiliko tu yatakayotukwamua - uongozi mpya, fikra mpya na mikakati mipya. Wakati ni sasa.
 
Kiwango cha rushwa Tanzania kinatisha na mpaka hapo mzizi wa fitina,CCM, utakapong'olewa, juhudi zozote za kuutokomeza ni vigumu kufanikiwa. Hatuwezi kutegemea watu wale wale, uongozi ule ule na nguvu zile zile zituletee matokeo tofauti - hapana, itakuwa ni ujinga mkubwa na tutakuwa tunajidanganya kama tulivyofanya kwa miaka 48. Ni mabadiliko tu yatakayotukwamua - uongozi mpya, fikra mpya na mikakati mipya. Wakati ni sasa.
Nani ataung'oa? We're not risk takers Mag3.
 
Heshima mbele wakuu,

Naomba kukaribishwa.

Kwa mawazo yangu ufisadi nchini tanzania hauwezi kwisha kwa sababu taasisi kama Takukuru, DPP, AG etc zote viongozi wake wanateuliwa na Rais na pia wanaripoti kwa Rais, Asa je kama ikitokea swahiba wa Rais au Rais mwenyewe ana hatia unategemea kutakuwa na haki hapo?.

Ukisoma katiba utagundua tuna mapungufu makubwa ya usimamizi wa sheria na haki.. Kwa mfano Uk, PM wao mbali ya kuwa Head of state lakini kuna vyombo huru vinavyosimamia utendaji wake.. Ni the same kwa USA, Pakisatn, Iran kuna supreme leader... n.k.. Nadhani katibayetu Tanzania inampa rais majukumu makubwa kiasi kwamba ni rahisi kwake kuingilia utendaji taasisi nyingine huru.

Pili tumeingiza siasa mno ktk kila proffessional.. Ukiangalia utendaji wa idara na taasisi zote za Umma zinaendeshwa kwa kuangalia matakwa ya kisiasa badala ya proffessionalism ya kiongozi husika.. Kwa Mfano, engeneers badala ya kukaa chini wafanye kazi zao za innovations wanaburuzwa na wanasiasa wakidhi matakwa ya kisiasa, ni the same kwa accountants wetu, financial auditors..lol.. Kikubwa ni kuamua kwa pamoja kama nchi na kufanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele na rasilimali tulizo nazo.

Mwisho, Sisi tulio na nafasi ya kupata news na kuchambua masuala mbali mbali ya kitaifa, iwe kupitia magazeti, internet, radio na tv, tusiwalaumu watanzania kuwa hawako tayari kubadilika..

Tujiulize swali muhimu, Je asilimia ngapi ya Watanzania wana access of informations zinazohusu taifa lao?

The majority wanasikiliza Radio ya Taifa, RFA na wachache TBC1, je hivi vyombo vipo huru kuwapelekea watanzania habari hasa hasa zile zinazoonyesha mapungufu ya kiutendaji na mikataba mibovu ya serikali ya tanzania? Ukimwambia leo hii mtu wa mapanda vijijini anatakiwa adai barabara ya lami anaweza asikuelewe unaongelea nini wakati yeye anajua kuna malori ya mizigo yatamsafirisha kwenda sumbawanga? Ukiangalia Lugha za wabunge wetu na uchambuzi wao wa bajeti the majority ya watz huwa hawaelewi kipi kinaongelewa..

Naomba wabunge au vyama vya siasa vitafsiri vifungu vichache vyenye umuhimu kwa lugha rahisi kabisa na report zipelekwe mpaka vijijini watu wajue mapungufu ya viongozi wao waliopo madarakani sas.. Vinginevyo itakuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa labda tupindue nchi na ni kitu hakiwezekani kwa jeshi letu.

Nashauri self awareness education ndio msingi wa mabdiliko ya ukweli.. Wananchi wapewe elimu ya bure ya mambo ya tanzania. Pia Jamiiforums tuwahusishe mabalozi, na mshirika ya kigeni yanayotupa misaada Tanzania wapate taarifa huku sio wasubirie taarifa za kuchonga za serikali.. Tumeshuhudia Ghana civil society ina sauti kubwa ndio maana Obama amewasifia.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Kutomtaja, kumjadili, JK kua moja kwa moja that current ndiye head of all ufisadis
 
Mjadala huu ni mzuri ingawa baadhi wanauchukulia kimzaha mzaha.

Wapi tumekosea katika mapambano dhidi ya ufisadi?

Katika kulijibu swali hili mtu kwanza hana budi kuainisha ni akina nani mafisadi. Jibu la swali hili linaweza kuwashangaza wengi. Ukweli ni kuwa kila mmoja wetu sisi watanzania ni fisadi. Kilichopo ni kuwa tunahitilafiana katika suala la viwango vya ufisadi.

Kwanini kila mmoja wetu ni fisadi chambua hoja hizi zifuatazo:

Chaguzi zetu zote katika nchi hii zimejaa rushwa. Bila fedha katika nchi hii huwezi kupata nafasi ya kuchaguliwa katika ngazi yoyote ile. Iwe ni katika CCM au CUF serikali za mitaa, CHADEMA na kadhalika. Watanzania kwa mamilioni hawafanyi kazi iwe ni vijijini au mijini. Kila mtu anataka kjuishi kwa dezo. Watanzania hatuna utashi wa kufanya mambo au maamuzi. We lack will. Kila mtu anakula (rushwa) pale alipo.

Nenda vijijini uone rushwa inavyotembezwa kwenye serikali za vijiji, kata, tarafa na kadhalika. Jioneee kile kinachotokea mahakamani. Jiji la Dar es Salaam hivi sasa ni vurugu tupu. Kila mtu anafanya atakavyo kana kwamba hakuna serikali. Madereva wanaendesha magari kwa kutanua na kuwagonga waenda kwa miguu. Hatua hazichukuliwi.

Tembea katika barabara ya UHURU (kutoka mnazi mmoja hadi shule ya uhuru) ujionee maajabu. Magari yamepaki katika maeneo ya waenda kwa miguu na kuwalazimisha waenda kwa miguu wanaotaka kununua vitu madukani watumie barabara na kujihatarisha wenyewe kutokana na msongamano mkubwa wa magari. Eneo la kisutu soko ni kila mahali hata kwenye mifereji ya maji machafu wafanyabiashara wanatandaza nyanya, vitungu na bidhaa nyingine. Pale Manzese wamachinga wamerudi kwa kasi na kutandaza bidhaa zao pembezoni mwa barabara.

Mfumo wetu wa utawala umeshindwa kufanya kazi katika kila eneo la nchi ndio maana nchi hii imejaa matatizo ya kutisha. Bunge ndiyo limekwisha.

Umesikia wabunge wetu wanazungumzia suala la watoto wa mitaani wanaoomba mitaani huku wenzao wakiwa darasani? Nyumba ya Waziri inakarabatiwa kwa shilingi bilioni moja huku watoto wa shule za misingi nyingi nchini wakiwa hawana madawati.

Pita katika mitaa ya Dar es salaam uone maelfu kwa maelfu ya watu wakiwa wamekaa vikundi vikundi wakati wa saa za kazi wakiwa hawana cha kufanya zaidi ya kupiga soga. Watanzania wanaofanya akzi kwa siku haizidi hata asilimia 10 iwe ni vijijini au mijini. Watanzania ni wapiga soga.

Mtanzania ukiwa una kazi au nafasi kidogo ndugu wanamiminika kwako utajikuta unakuwa na watu siyo chini ya kumi wanaolishwa na wewe, na wala huwezi kuwafukuza kwani hao ni ndugu zako.

Ulishawahi kufanya tathimini ya sifa za viongozi wetu kwa mfano wakuu wa wilaya? Wengi hawajui hata maana ya uongozi. Mkuu wa wilaya anamuacha dereva wa serikali na kumchukua dereva wa mitaani ambaye pengine wanafahamiana kuendesha gari la serikali. Wakuu wa wilaya wengi hawajui kazi kabisa. wamepewa nafasi hizo kwa fadhila. Nchi itaendeleaje katika hali hii. Sisi Watanzania tumelaaniwa. Tumelogwa.

Ajali zipo kila kona ya nchi kwa sababu wengi wanaoendesha mabasi hawana sifa. Vyombo vya dola viko kwenye matatizo.

Rais Mstaafu anazabwa kibao wakati vyombo vya dola vipo.

Wastaafu wa Afrika Mashariki wanalala barabarani Selander Bridge vyombo vya dola vipo na havijui kama tukio la aina hiyo litatokea.

Je, wafanyakazi kwenye nafasi nyeti serikalini kweli wanafanyiwa screening au vetting? Ni hoja inayoweza kuzua mjadala mwingine. Wale waliokuwa wakiitukana serikali baadhi sasa wako madarakani wakiwa na nyadhifa nyeti. Nchi hii inaselekea kubaya wengi pengine hatujui kuwa tunakwenda kuzimu.

Rushwa itakwishaje wakati wengi wetu hatuna 'will' ya kupigana nayo zaidi ya kulindana? Ni mtanzania gani msafi katika nchi hii kwa sasa? Asimame tumuone na ajipige kifua kuwa yeye ni msafi. Mfumo wa uongozi na utawala katika ngazi zote kuanzia kwenye familia mpaka juu kabisa haufanyi kazi kwa hiyo rushwa na ufisadi hauwezi kwisha.

POLENI WATANZANIA. HONGERENI KWA KUPIGA KELELE ZA UFISADI NA UFISADI ZISIZO NA TIJA.
 
Yote tunayoyaweka hapa sidhani kama CCM wataweza kuya-impliment, kwa maana wako deeply involved. Kwa maneno mengine, kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzie. Tunahitaji viongozi wenye macho. The longer we wait the longer it will take to save our country.
Hivi tukiwasamehe mafisadi kutakuwa na taabu? on condition waachie ngazi?
ohh...one more question: Nani ana nguvu zaidi, rais/serikali, bunge au mahakama katika mfumo uliopo Tanzania? alafu rais sio sehemu ya bunge na hapo hapo sehemu ya executive? sio tatizo lingine hili?
 
nimejaribu kuwahoji watu wawili watatu juu ya tatizo sugu la rushwa,wamenijibu shortly lakini nimeumiza sana kichwa!wanasema

CORRUPTION IS HUMAN NATURE!tunapishana ile extent
 
Heshima mbele wakuu,
Naomba kukaribishwa.
Kwa mawazo yangu ufisadi nchini tanzania hauwezi kwisha kwa sababu taasisi kama Takukuru, DPP, AG etc zote viongozi wake wanateuliwa na Rais na pia wanaripoti kwa Rais, Asa je kama ikitokea swahiba wa Rais au Rais mwenyewe ana hatia unategemea kutakuwa na haki hapo?. Ukisoma katiba utagundua tuna mapungufu makubwa ya usimamizi wa sheria na haki.. Kwa mfano Uk, PM wao mbali ya kuwa Head of state lakini kuna vyombo huru vinavyosimamia utendaji wake.. Ni the same kwa USA, Pakisatn, Iran kuna supreme leader... n.k.. Nadhani katibayetu Tanzania inampa rais majukumu makubwa kiasi kwamba ni rahisi kwake kuingilia utendaji taasisi nyingine huru.

Pili tumeingiza siasa mno ktk kila proffessional.. Ukiangalia utendaji wa idara na taasisi zote za Umma zinaendeshwa kwa kuangalia matakwa ya kisiasa badala ya proffessionalism ya kiongozi husika.. Kwa Mfano, engeneers badala ya kukaa chini wafanye kazi zao za innovations wanaburuzwa na wanasiasa wakidhi matakwa ya kisiasa, ni the same kwa accountants wetu, financial auditors..lol.. Kikubwa ni kuamua kwa pamoja kama nchi na kufanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele na rasilimali tulizonazo.

Mungu ibariki Tanzania.

Yaani unaonglea kiini cha tatizo lenyewe na mimi nakuunga mkono kwa hilo. Hapo tatizo letu wengi tunajua sana kuhusu matatizo yetu ya tanznania. Na tuna namna million moja ya kutatua tatizo moja, lakini chanzo cha tatizo ndio tunakwepa, wengi watakwambia uongozi ni ule ule wa muda kwa hivyo ubadilike waje wenye uchungu na nchi sawa but they forget this is just the secondary problem, tuna guarantee gani ya baadae kwamba hawata shikwa na tamaa kwani amna mtu anaezaliwa nayo. Ni situation tu ambayo inamfanya mtu abadilike for what he stands for especially when it comes to financial gain.

Kwa hivyo tatizo sio viongozi tu peke yake bali na sheria zenyewe aziko wazi hivyo na wala azina nguvu hivyo za kusema amna mtu mwenye uwezo wa kulindwa na sheria penye makosa. mpaka tuunde katiba zenye kutoa baadhi ya nguvu za serikali na raisi ndio ukweli tunaweza kuanza kupambana na ufisadi.

wengi humu uangalia vitu based na degree zao tu and not reasoning outside those boxes. Mfano nina 90% guarantee aliyeweka thread hii based on his explanation ni Economist so i do not expect lots of critical evaluation of the situation. she seems to look at things on scarcity of them ndio maana anaona sheria ni nyingi mbona amna mabadiliko asicho angalia je hizo sheria zinatumika vipi na zina kwama wapi.
 
nimejaribu kuwahoji watu wawili watatu juu ya tatizo sugu la rushwa,wamenijibu shortly lakini nimeumiza sana kichwa!wanasema

CORRUPTION IS HUMAN NATURE!tunapishana ile extent

mh, ulikuwa hujui hilo? Hakuna sehemu ambako hakuna rushwa. Hata China kuna Rushwa. Tatizo sisi tumefikia kiwango kisichokubalika. Unaweza kufananisha na 'inflation'. Wanauchumi wanakwambia lazima kuwe na inflation. Kitu wanafanya ni ku-maintain ile rate iwe low - labda 1%-3%.
Hapo sisi ndo tumeshindwa maana sasa rushwa imekithiri. Ni kama WOS alivyosema....we lack accountability. Hii inatokea pale mtunga sheria, msimamiaji sheria na mtoa hukumu wa sheria anapokuwa mtu mmoja - aka CCM. CCM imeshika Executive, Legislative na Judiciary branch. Nilipendekeza katika earlier post nikasema hizi organisation kama PCCB, zingekuwa chini ya bunge - angalau kusiwe na mkono wa serikali humo. Maana zinatakiwa kusimamia serikali. Wewe mtoto wako anaweza kukuhukumu hivi leo? Kwa nini zisimamiwe na bunge? Bunge lina accountability, sema kwa sasa TZ hii haipo kutokana na ununuaji wa kura. Lakini in theory, hali ndo ingetakiwa kuwa hivyo. Bunge likishindwa kazi, tunachagua wabunge wapya, through njia pekee sisi wananchi tuliyopewa kwa ajili ya kuendesha nchi - UCHAGUZI.Lakini kutokana na bunge letu na serikali kuwa kitu kimoja, basi accountability haipo.

Ukiangalia Mahakama, nayo ndio hao majudge wanachaguliwa na rais bila usimamizi wowote - another problem. Yani kwa ujumla mfumo mzima umekaa kaa tu. Na la kuongeza ni hilo la Ujinga nililogusia mapema. Watu wanauza kura. Watu hawajui haki zao, nk. Lakini at the end ni vitu viwili: ACCOUNTABILITY and TRANSPARENCY. Bila hivyo...tutaendelea kuumia.

Tuanze mchaka mchaka...alisema, alisema.....
 
Mtoto, Umegusia kitu muhimu sana.
Ukweli humweka mtu huru kuhoji....... kujitetea.
Uwazi humfanya mtu kujua nini kinaendela.... humfanya mtu ashindwe kufanya vitu ambavyo havikubaliki.
Rushwa huchangiwa na ujinga kama ulivyosema na pia mambo kufanywa kwa kificho.
Corruption= Accountability- Transparecy +Discretion
( C= A-T+D)
Yaani kunapokosekana Uwajibikaji na Uwazi na kukawepo na hali ya mtu kutumia madaraka apendavyo hapo kunakuwepo na rushwa.

Ili kosa lolote liweze kutendeka ni lazima hizi factor mbili ziweze kufanyakazi kwa pamoja.

Crime = Temptation + Opportunity

Kinachotakiwa ni kujenga mifumo itakayozuiya hizi factors mbili zisifanye kazi kwa pamoja.

if you disable Opportunity then temptation will stay ineffective and in the long run it can be eliminated. The same applies to the temptation.
 
Nilikuwa nawaza juu ya hili na kulinganisha na nchi zilizoendelea. Kitu kingine kikubwa kinachochangia ni uchumi mbovu. Kwa mfano katika nchi zilizoendelea, ukiangalia maisha ya mtu wa kawaida - yani mwenye kipato cha kawaida kama polisi, na vitu anavyoweza kupata kutokana na mshahara wake, basi hali hii inamnyima incentive ya kula rushwa. Tuchukue kitu kama kuwa na gari. Hichi kitu bongo bado ni luxury. Vingine ni kama Kwenda cinema, kwenda supermarket, nk. Ambapo huku, hivyo ni vitu vya kawaida sana hata mtu wa kipato cha chini anaweza ku-afford. Kwa hiyo, kula rushwa au element ya ufisadi itapunguzwa sana na kaka income itaendana na matumizi - uwiano wa income na expenditure. Hivyo basi Tanzania tufanyaje? Tunaweza kuanza kwa ku-improve our manufacturing industries. Yani tuwe tunatengeneza vitu vyetu, ambavyo vitakuwa katika bei nafuu, ambayo kila mtu ataweza ku-afford. Kwa mfano kiwanda cha tv, nk. Tumejijengea sifa kuwa na vitu vilivyotengenezwa nje ya nchi zaidi ya vitu vya nyumbani. Lakini kama tutaweza kujenga viwanda nchini na kuvi-support, basi hii itasaidia sana katika kupunguza ufisadi, hasa mdogo mdogo. Then slowly tutapanda ngazi na kupambana na mafisadi nyangumi na mapapa.
 
Punamilia07,
Mkuu nakukubali sana tu ktk hili isipokuwa ktk Ufisadi kinachotangulia mbele ya crime ni UTAJIRI.. hivyo crime inakuwa mojawapo ya means ya kuupata huo Utajiri..Na mara zote hata yule aliyefanikiwa kuupata Utajiri bila kupitia njia hii (crime), basi mafanikio yake hutokana na nguvu hizi mbili yaani Temptation na Opportunity.

Hivyo ni vigumu ku eliminate Crime ikiwa kila mmoja wetu atapenda kuwa tajiri na huwezi kuharamisha Utajiri kwa sababu ndiyo maendeleo yenyewe...ikiwa na maana hatuwezi kujenga mifumo inayoondoa hizi factors mbili ambazo zipo pande zote mbili laa sivyo itakuwa tunajaribu kuondoa kiini cha yote yaani pamoja na UTAJIRI..

Ndipo tunapokuta hizi siasa zetu zikigongana kwa sababu hakuna mfumo rahisi wa kuzuia crime kwa mtu mmoja mmoja au Taifa zima bila kuathiri wenye nia njema na Utajiri, isipokuwa sheria zetu ndizo zinatakiwa kukinga,kulinda na kuzia ukiukaji wa mbinu zinazotumika kupata utajiri zisije fikia kuwa ni criminal acts..
Ndio yale ya Ujamaa wa Nyerere na Azimio la Arusha, Sokoine na Wahujumu Uchumi, Mwinyi na Fagio la Chuma.. mifumo yote hii ilikuja onekana kuwa ipo kupinga Utajiri pamoja na kwamba ilielekeza nguvu zake kupambana na wahalifu. Sababu kubwa ni kwamba mbinu zote hizi zilielekeza kufuta Temptation na Opportunity, of which also eliminate means of people getting RICH..

Tatizo la nchi yetu bila shaka tumefikia mahala Crime ni SIFA. Ukiwa BoT hujawahi kuiba wewe ni mjinga, Ukiwa kiongozi hujawahi kufanya Ufisadi wewe ni mjinga kwa sababu hakuna mtu anayeweza kuwa na Utajiri kwa kupitia mshahara..Pengine inatakiwa watu tufikirie kwanza kuwa na MAISHA BORA ni muhimu kuliko Utajiri lakini pia tukubali hakuna kipimo kati ya kutafuta Maisha bora na Utajiri..na means za kupata mambo haya ndipo Uharamu na crimes unapoingia..

Somo hili latakiwa kuchukua mfano wa dini - yaani kutambua na kuepukana na haramu toka katika mambo mazuri na yaliyohalalishwa,(kuchambua mchele toka ktk Pumba) lakini pia kusisitiza kuwa pepo haipatikani kwa kuepuka mabaya tu bali ni matendo mazuri yatakayo kupeleka peponi.. - Utajiri sii haramu.

Kwa mchanganyiko wa haya yote mkuu wangu inaniuwia vigumu kuweka mstari kati ya maisha bora na Utajiri na jinsi gani utaweza muunda mfumo utakao futa temptation na Opportunity ikiwa yapo maendeleo ya mtu au jamii hutegemea factors hizo hizo..
 
Last edited:
Back
Top Bottom