Kuabudu ni swala binafsi uko huru kusali au kutosali.Ukiona wewe ukienda kusali utapata corona usiendeSerikali inasita kabisa kuzuia ibada zote makanisani na misikitini,sijui shida ninini, Vatican washasitisha na hadi huko Macca, sijui shida iko wapi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Misa bila nyimbo zilikuwepo tangu kabla ya Vatican II, wakati tukisali Kilatini. Kulikuwa na Misa mbili: ya kwanza haina kuimba na ifuatayo yenye kuimba. Sala ni zilezile katika Misa zote mbili. Tofauti ni kwamba katika Misa ya kwanza sala zinasaliwa tu ambapo wakati wa Misa ya Pili sala hizo hizo zinaimbwa badala ya kusaliwa tu. Kwa mfano Kyrie, Gloria, Kanuni ya Imani, Mtakatifu na Mwana Kondoo. 'Shangilio' peke yake liliweza kuchukua hata dakika tano likiimbwa wakati likisaliwa tu linachukua chini ya dakika moja. Hii inasababisha Misa ya pili kuchukua muda zaidi ya mara mbili ya ule wa Misa ya kwanza. Hata siku hizi Misa ya Jumapili ndiyo inakuwa na kuimba kwingi wakati Misa ya katikati ya wiki haina kuimba kwingi na inachukua muda mfupi tu. Kwa hiyo kusema kwamba tusali bila kuimba siyo jambo geni. Lilikuwa likitokea na linaendelea kutokea hadi sasa. Inachoagiza TEC ni kwamba kusiwepo kuimba ili kufipisha muda. Hakuna cha ajabu hapo. Nimekuwa nikifuatilia Misa za katikati ya wiki kwenye Youtube ambazo zinaendeshwa na Papa mwenyewe huko Vatican tangu wiki Takatifu, kwa kuwa imekatazwa watu kwenda kanisani nchini Italia. Misa inachukua nusu saa tu badala ya saa mbili ambazo ingechukua kama kungekuwepo na kuimba. Usipotoshe kwa kusema Misa bila kuimba ni maigizo na kumpangia Mungu namna ya kumuabudu.Yaani ibada ya kikristo bila nyimbo?
Sasa hiyo ni ibada au maigizo ya kibagani?
Kwanini wasizuie watu kutoa sadaka, maana virusi vya Corona vinaweza kukaa kwenye karatasi au chuma kwa siku kadhaa?
Waache upuuzi wa kumpangia Mungu namna ya kumuabudu, wanalazimisha watu waende makanisani kumwabudu Mungu wakati Mungu yupo popote na anaweza kuabudiwa popote.
Watu wahimizwe kuabudu majumbani mwao, maana kanisa la kweli huanzia nyumbani na huishia nyumbani.
Kusoma katekisimo na sio kusoma Biblia takatifu. Hapa ndiko watu walikopotezwa na kumridhia yule mwanamke kahaba mzinzi-Yezebeli kwa kumpa jina bikira Maria.
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo Hellen G. White unayemsema mimi simfahamu.Mkuu sio katekisimu ni badala ya kusoma biblia wao husoma PAMBAZUKO KUU!
Hapa ndipo walikopotezwa na kumridhia yule mwanamke kahaba mzinzi-Yezebeli kwa kumpa jina HELLEN G WHITE!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona barua ni ya kuomba maoniBaraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ‘TEC’ limetoa tamko kutekeleza agizo alilotoa Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Aprili 15, juu ya kujilinda na #COVID19 kwenye masuala ya ibada
TEC imeamua kusitisha mazoezi ya kwaya ili kuepuka mikusanyiko. Pia nyimbo wakati wa ibada zimesitishwa ili Ibada isitumie muda mrefu
Pia mafundisho ya dini kwa watoto na makundi mengine yamesitishwa. Mafundisho yataendelea kwa njia nyingine kama kujisomea katekisimu au njia ya mtandao
Pia kanisa litazingatia umbali wa mtu na mtu wanapokuwa ibadani, matumizi ya vinasa sauti, watanawa mikono kabla ya kuingia kanisani pia watanyunyizia dawa vifaa vya ibada
Makatekista na wanaotoa huduma wataelewesha kuhusu #CoronaVirus na watapewa vifaa vya kujikunga, kufanyia usafi na kunyunyiza
====