Mapato ya Mjusi Wetu

Mapato ya Mjusi Wetu

Wasije kutuletea mjusi feki, si wanasema wanamrefurbish
 
Wasije kutuletea mjusi feki, si wanasema wanamrefurbish
Ninavyoelewa huwezi kupata kiunzi bila sehemu za feki, maana vipande havikuwepo vyote. Vilikaa ardhini si pamoja, bali vilitawanywa. Wakati ule walikusanya waliyoweza kupata (na kutambua). -- Pili kwa maonyesho walitoa sasa vipande kadhaa na kuvibadilisha plastiki kwa sababu ya uzito. Maana yale yanayopatikana si mifupa hali halisi, ni mawe yenye umbo la mifupa. Jisomee kuhusu visukuku. Kwa hiyo vipande ni vizito, ni vya kale, na hapa waliona tatizo la kubeba uzito wa vipande vya juu. Ninavyosoma, kiunzo chote kilikuwa tayari mara mbili hatarini ya kuporomoka (urefu wa mita 13 au 14). Hapo waliondoa sasa sehemu dhaifu na kuweka mifano ya plastiki badala yake.

Kama wangerudisha tu vipande vya original, kumbe! Hapa kazi tu!
 
kaka sijui unapinga nini? Nilijibu hoja lako "Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!.. kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, .. if at all any preservative treatment is required to keep it.. part of the money (tourism fees) collected would be used".
Hapa nasema 1) Ndiyo kutunza mifupa ya kale ni kazi kubwa na ghali, 2) tusiwaze maonyesho yake yataleta faida ya kifedha kutokana na kiingilio maana gharama za kutunza ni kubwa kuliko kila kila kiingilio..


Kwa hiyo anayetaka kuirudisha mifupa aseme jinsi atakavyolipa gharama (Kwanza kujenga ukumbi, pamoja na tekinolojia ya AC, usalama na taa, pili kufunza wataalamu wa fani husika, tatu kugharamia uendeshaji endelevu wa makumbusho mapya.)

Nigeria wanapanga sasa kuchukua hizo sanamu ndogo za bronzi zilizoibiwa na Waingereza mjini Benin. Kwa kazi hiyo wametenga mamilioni kujenga makumbusho mapya. Wakiamua kutumia milioni kutoka pesa ya mafuta yao, sawa, (hata kama bado watu wengi sana pale wako maskini na bila huduma - chanzo cha BokoHaram). Na Ujerumani waliamua kuwapa bronzi kutoka Benini zilizonunuliwa na makumbusho ya Ujerumani.
Kwa hiyo sidhani Wajerumani watagoma kurudisha mifupa ya dinosauri. Ila ukiangalia maelezo ya ile kamati ya bunge (video), hawasemi wanataka mifupa, wanasema wanataka asilimia ya mapato. View attachment 1769752

Ambayo naona ni ajabu kidogo ukitaka sehemu ya mapato ya biashara inayoleta hasara. Hao wa pale kama ni wajanja wangejibu je mnataka 50% za hasara ya maonyesho?
Hawatasema, lakini je ingekuwa busara kurudisha mifupa hapa TZ sasa, wakati hakuna mahali pa kuwekea, hakuna wataalamu wanaoweza kuiunganisha na kusimamisha na hakuna pesa ya kuendesha?

Mifupa hii itendewe kama mwendokasi?


Mimi hata sikuelewi ndugu yangu.

1----Hoja ni hii: Hiyo mifupa ni mali ya nani???

2--- kama inawaingizia hasara hao wajerumani katika utunzaji kwanini wanaing'ang'ania???--- sio uwendawazimu kuendesha kitu kinachokupa hasara???--- kama hujui ni MZUNGU mwehu afanyaye biashara inayomuingizia hasara, hakuna mzungu anayefanya biashara kichaa.

Hiyo mifupa ni mali yetu, hata kama tutaichukua na kujenga "a sealed glass show case filled with helium gas in which to put the fossils" inatosha tu, watu wanaweza kuiangalia kupitia hiyo Show case na wakalipa kiasi kidogo cha fee kuliko kushikilia stereotypes kwamba "HATUWEZI" kuitunza,----sasa tutaweza nini?? au ndio ule msemo kwamba watu weusi tumekuja kujaza dunia tu??!!.

Ngoja nikukumbushe; Ugunduzi wa chuma miaka mia kadhaa iliyopita ndio ulichochea industrial revolution huko Ulaya, leo hii karne ya 21 Chuma kimejaa Liganga na Mchuchuma (Trillions of tones) tumeshindwa kukiyeyusha na kuunda mataruma ya SGR sababu eti hatuwezi !!! eti ni bora mataruma yatoke Turkey na wao wafaidi kiuchumi!!😨😨--- msitake tuwaamini wale wanaosema; Mtu mweusi weusi haupo kwenye ngozi yake tu bali hata kwenye ubongo wake pia ni kweusi.
 
Kuna mtu anauliza swali eti kabla mjusi kuchukuliwa tulikuwa tunapata sh ngapi?, Eti Huyo hakuwa na ndugu? Kuna mtaalamu yeyote anayewatafuta ndugu zake? Au hadi mzungu aje, atafute, abebe tuanze harakati za kudai?
 
Kuna mtu anauliza swali eti kabla mjusi kuchukuliwa tulikuwa tunapata sh ngapi?, Eti Huyo hakuwa na ndugu? Kuna mtaalamu yeyote anayewatafuta ndugu zake? Au hadi mzungu aje, atafute, abebe tuanze harakati za kudai?
Nimeona mkurugenzi wa makumbusho ya Berlin alipendekeza kufanya kazi ya pamoja; hao walete vifaa vya kisasa (ground radar) na Tanzania watalaamu wao, waende pamoja Lindi-Tendaguru na kutafuta pamoja. Maana tangu siku za Mwingereza miaka ya 1920s (15 baada ya ugunduzi wa mifupa iliyopo Berlin) hakuna aliyetafuta pale tena. Yule mkurugenzi aliandika, eti mjusi wa Berlin alikuwa kijana tu, angeshangaa sana kama wakubwa wasingepatikana pala Tendaguru . . .
Nadhani kwa njia hiyo alitaka kuepukana na majadiliano ya kurudisha mifupa hiyo, ila sijui kama ni hoja baya.... Watu wa hapa wapate tekinolojia ya kisasa waangalie wenyewe. Maana hata huko Usongwe mayai ya dinosauri yalipatikana (nadhani walikuwa wazungu walioyakuta..)
 

''WABUNGE Kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameanzisha kamati maalum ya kuhakikisha sehemu ya mapato ya utalii yanayotokana na mabaki ya mjusi mkubwa aliyeko katika jumba la makumbusho Mjini Berlin nchini Ujerumani yanarejeshwa hapa nchini. Mjusi huyo anatambulika kwa jina la DINOSAUR ambaye mabaki yake yalivumbuliwa zaidi ya miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi. Tangu kugunduliwa kwa mabaki hayo na hata kusafirishwa hadi mjini Berlin nchini Ujerumani hakuna kiasi chochote cha mapato kilichowahi kurejeshwa hapa nchini ikiwa ni faida inayotokana na utalii wa mjusi huyo hali iliwalazimu wabunge hao wakiongozwa na mwenyekiti Riziki Lulida kuanzisha kamati hiyo itakayopambania maslahi ya Mjusi huyo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu. MAPAMBANO haya yanaungwa mkono na wabunge mbalimbali kutoka katika majimbo ya Tanzania Bara na upande wa Pili wa Zanzibar kwa maslahi mapana ya Taifa. Kwa upande wa Serikali kupitia kwa Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi amewathibitishia wabunge hawa kuwa serikali itashirikiana nao ili kuhakikisha kuwa taifa linaanza kunufaika kupitia mabaki ya mjusi huyo.''​

bombadia zipo tumfate
 
Back
Top Bottom