Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ninavyoelewa huwezi kupata kiunzi bila sehemu za feki, maana vipande havikuwepo vyote. Vilikaa ardhini si pamoja, bali vilitawanywa. Wakati ule walikusanya waliyoweza kupata (na kutambua). -- Pili kwa maonyesho walitoa sasa vipande kadhaa na kuvibadilisha plastiki kwa sababu ya uzito. Maana yale yanayopatikana si mifupa hali halisi, ni mawe yenye umbo la mifupa. Jisomee kuhusu visukuku. Kwa hiyo vipande ni vizito, ni vya kale, na hapa waliona tatizo la kubeba uzito wa vipande vya juu. Ninavyosoma, kiunzo chote kilikuwa tayari mara mbili hatarini ya kuporomoka (urefu wa mita 13 au 14). Hapo waliondoa sasa sehemu dhaifu na kuweka mifano ya plastiki badala yake.Wasije kutuletea mjusi feki, si wanasema wanamrefurbish
kaka sijui unapinga nini? Nilijibu hoja lako "Kwani Kutunza mifupa ni kazi??!!.. kumbuka hiyo mifupa ilikuwa fossilized for thousands of years underground with natural preservative treatment, .. if at all any preservative treatment is required to keep it.. part of the money (tourism fees) collected would be used".
Hapa nasema 1) Ndiyo kutunza mifupa ya kale ni kazi kubwa na ghali, 2) tusiwaze maonyesho yake yataleta faida ya kifedha kutokana na kiingilio maana gharama za kutunza ni kubwa kuliko kila kila kiingilio..
Kwa hiyo anayetaka kuirudisha mifupa aseme jinsi atakavyolipa gharama (Kwanza kujenga ukumbi, pamoja na tekinolojia ya AC, usalama na taa, pili kufunza wataalamu wa fani husika, tatu kugharamia uendeshaji endelevu wa makumbusho mapya.)
Nigeria wanapanga sasa kuchukua hizo sanamu ndogo za bronzi zilizoibiwa na Waingereza mjini Benin. Kwa kazi hiyo wametenga mamilioni kujenga makumbusho mapya. Wakiamua kutumia milioni kutoka pesa ya mafuta yao, sawa, (hata kama bado watu wengi sana pale wako maskini na bila huduma - chanzo cha BokoHaram). Na Ujerumani waliamua kuwapa bronzi kutoka Benini zilizonunuliwa na makumbusho ya Ujerumani.
Kwa hiyo sidhani Wajerumani watagoma kurudisha mifupa ya dinosauri. Ila ukiangalia maelezo ya ile kamati ya bunge (video), hawasemi wanataka mifupa, wanasema wanataka asilimia ya mapato. View attachment 1769752
Ambayo naona ni ajabu kidogo ukitaka sehemu ya mapato ya biashara inayoleta hasara. Hao wa pale kama ni wajanja wangejibu je mnataka 50% za hasara ya maonyesho?
Hawatasema, lakini je ingekuwa busara kurudisha mifupa hapa TZ sasa, wakati hakuna mahali pa kuwekea, hakuna wataalamu wanaoweza kuiunganisha na kusimamisha na hakuna pesa ya kuendesha?
Mifupa hii itendewe kama mwendokasi?
Nimeona mkurugenzi wa makumbusho ya Berlin alipendekeza kufanya kazi ya pamoja; hao walete vifaa vya kisasa (ground radar) na Tanzania watalaamu wao, waende pamoja Lindi-Tendaguru na kutafuta pamoja. Maana tangu siku za Mwingereza miaka ya 1920s (15 baada ya ugunduzi wa mifupa iliyopo Berlin) hakuna aliyetafuta pale tena. Yule mkurugenzi aliandika, eti mjusi wa Berlin alikuwa kijana tu, angeshangaa sana kama wakubwa wasingepatikana pala Tendaguru . . .Kuna mtu anauliza swali eti kabla mjusi kuchukuliwa tulikuwa tunapata sh ngapi?, Eti Huyo hakuwa na ndugu? Kuna mtaalamu yeyote anayewatafuta ndugu zake? Au hadi mzungu aje, atafute, abebe tuanze harakati za kudai?
bombadia zipo tumfate
''WABUNGE Kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameanzisha kamati maalum ya kuhakikisha sehemu ya mapato ya utalii yanayotokana na mabaki ya mjusi mkubwa aliyeko katika jumba la makumbusho Mjini Berlin nchini Ujerumani yanarejeshwa hapa nchini. Mjusi huyo anatambulika kwa jina la DINOSAUR ambaye mabaki yake yalivumbuliwa zaidi ya miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi. Tangu kugunduliwa kwa mabaki hayo na hata kusafirishwa hadi mjini Berlin nchini Ujerumani hakuna kiasi chochote cha mapato kilichowahi kurejeshwa hapa nchini ikiwa ni faida inayotokana na utalii wa mjusi huyo hali iliwalazimu wabunge hao wakiongozwa na mwenyekiti Riziki Lulida kuanzisha kamati hiyo itakayopambania maslahi ya Mjusi huyo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu. MAPAMBANO haya yanaungwa mkono na wabunge mbalimbali kutoka katika majimbo ya Tanzania Bara na upande wa Pili wa Zanzibar kwa maslahi mapana ya Taifa. Kwa upande wa Serikali kupitia kwa Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi amewathibitishia wabunge hawa kuwa serikali itashirikiana nao ili kuhakikisha kuwa taifa linaanza kunufaika kupitia mabaki ya mjusi huyo.''