Mapato ya Mjusi Wetu

Wasije kutuletea mjusi feki, si wanasema wanamrefurbish
 
Wasije kutuletea mjusi feki, si wanasema wanamrefurbish
Ninavyoelewa huwezi kupata kiunzi bila sehemu za feki, maana vipande havikuwepo vyote. Vilikaa ardhini si pamoja, bali vilitawanywa. Wakati ule walikusanya waliyoweza kupata (na kutambua). -- Pili kwa maonyesho walitoa sasa vipande kadhaa na kuvibadilisha plastiki kwa sababu ya uzito. Maana yale yanayopatikana si mifupa hali halisi, ni mawe yenye umbo la mifupa. Jisomee kuhusu visukuku. Kwa hiyo vipande ni vizito, ni vya kale, na hapa waliona tatizo la kubeba uzito wa vipande vya juu. Ninavyosoma, kiunzo chote kilikuwa tayari mara mbili hatarini ya kuporomoka (urefu wa mita 13 au 14). Hapo waliondoa sasa sehemu dhaifu na kuweka mifano ya plastiki badala yake.

Kama wangerudisha tu vipande vya original, kumbe! Hapa kazi tu!
 


Mimi hata sikuelewi ndugu yangu.

1----Hoja ni hii: Hiyo mifupa ni mali ya nani???

2--- kama inawaingizia hasara hao wajerumani katika utunzaji kwanini wanaing'ang'ania???--- sio uwendawazimu kuendesha kitu kinachokupa hasara???--- kama hujui ni MZUNGU mwehu afanyaye biashara inayomuingizia hasara, hakuna mzungu anayefanya biashara kichaa.

Hiyo mifupa ni mali yetu, hata kama tutaichukua na kujenga "a sealed glass show case filled with helium gas in which to put the fossils" inatosha tu, watu wanaweza kuiangalia kupitia hiyo Show case na wakalipa kiasi kidogo cha fee kuliko kushikilia stereotypes kwamba "HATUWEZI" kuitunza,----sasa tutaweza nini?? au ndio ule msemo kwamba watu weusi tumekuja kujaza dunia tu??!!.

Ngoja nikukumbushe; Ugunduzi wa chuma miaka mia kadhaa iliyopita ndio ulichochea industrial revolution huko Ulaya, leo hii karne ya 21 Chuma kimejaa Liganga na Mchuchuma (Trillions of tones) tumeshindwa kukiyeyusha na kuunda mataruma ya SGR sababu eti hatuwezi !!! eti ni bora mataruma yatoke Turkey na wao wafaidi kiuchumi!!😨😨--- msitake tuwaamini wale wanaosema; Mtu mweusi weusi haupo kwenye ngozi yake tu bali hata kwenye ubongo wake pia ni kweusi.
 
Kuna mtu anauliza swali eti kabla mjusi kuchukuliwa tulikuwa tunapata sh ngapi?, Eti Huyo hakuwa na ndugu? Kuna mtaalamu yeyote anayewatafuta ndugu zake? Au hadi mzungu aje, atafute, abebe tuanze harakati za kudai?
 
Kuna mtu anauliza swali eti kabla mjusi kuchukuliwa tulikuwa tunapata sh ngapi?, Eti Huyo hakuwa na ndugu? Kuna mtaalamu yeyote anayewatafuta ndugu zake? Au hadi mzungu aje, atafute, abebe tuanze harakati za kudai?
Nimeona mkurugenzi wa makumbusho ya Berlin alipendekeza kufanya kazi ya pamoja; hao walete vifaa vya kisasa (ground radar) na Tanzania watalaamu wao, waende pamoja Lindi-Tendaguru na kutafuta pamoja. Maana tangu siku za Mwingereza miaka ya 1920s (15 baada ya ugunduzi wa mifupa iliyopo Berlin) hakuna aliyetafuta pale tena. Yule mkurugenzi aliandika, eti mjusi wa Berlin alikuwa kijana tu, angeshangaa sana kama wakubwa wasingepatikana pala Tendaguru . . .
Nadhani kwa njia hiyo alitaka kuepukana na majadiliano ya kurudisha mifupa hiyo, ila sijui kama ni hoja baya.... Watu wa hapa wapate tekinolojia ya kisasa waangalie wenyewe. Maana hata huko Usongwe mayai ya dinosauri yalipatikana (nadhani walikuwa wazungu walioyakuta..)
 
bombadia zipo tumfate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…