Kwa ujumla ni kitu kizuri kwa Kenya, ila kumbuka kwamba hiyo ni robo tatu moja tu kati ya nne, inategemeana na robo tatu zingine ili kupata wastani ambao ndio utakua ni ukuaji wa uchumi wa mwaka mzima, katika hiyo robo tatu ambayo Kenya uchumi umekua kwa 6%, Rwanda umekua kwa 10%, lakini wanategemea uchumi wa Rwanda kukua kwa 7% mwaka 2018 kwa ujumla.
Kama ambavyo David Ndii anavyosema kila Mara, Uchumi wa Kenya upo very "Volatile" kutokana na makosa yaliyofanywa na waanzilishi wa Taifa la Kenya. Walipaswa kuanza kujenga misingi imara ya nchi ili kuweka mazingira mazuri ya Uchumi endelevu. Nchi haiwezi kuwa endekevi kama hakuna Umoja na mshikamano wa kitaifa"(Social cohesion), Umoja, upendo na Amani, haki na Usawa, vikiwepo hivi ndio vinazalisha UTU.
Nyerere alitumia muda mrefu sana kujenga misingi imara ya Tanzania, aliamini kwamba, bila kujenga Taifa lenye kujali UTU zaidi kuliko kujali KITU, haitowezekana kujenga Uchumi endekevu. Hili linajidhihirisha sana huko Kenya, huu ukuaji wa uchumi wa Kenya sio endelevu kwasababu kila baada ya miaka mitano lazima unashuka kutokana na athari za uchaguzi.
Sent using
Jamii Forums mobile app