Mapato ya uwanja wa Benjamini Mkapa ndiyo kikwazo kikubwa kwa mapacha wa Kariakoo kujenga uwanja wao

Mapato ya uwanja wa Benjamini Mkapa ndiyo kikwazo kikubwa kwa mapacha wa Kariakoo kujenga uwanja wao

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Huwa zinaibuka kelele na kampeni za ujenzi wa uwanja/mashabiki kuchangia timu zao ili zijenge uwanja lakini mwisho wa siku kimya.

Huo ni mchezo mchafu unaochezwa na viongozi wa wa klabu hizi mbili (Simba na Yanga) kwa lengo la kuwakamua mashabiki wao kidogo walichonacho.

Siasa za kariakoo huwa zinachezwa na watu wachache kwa manufaa ya kunufaisha mifuko yao, kwani wanachokifanya wanakijua na wanajua kabisa halambee ya kuchangia uwanja ili timu zao zijenge uwanja ni hadithi za sungura na fisi tu kwani ni kitu ambacho hakiwezekani.

Uwanja wa mkapa unaingiza pesa nyingi kupitia timu hizi mbili (Simba sc na Yanga Sc) kwa akili ya kawaida tu Wala haihitaji akili ya kwenda shule unadhani Simba na Yanga wakiwa na uwanja wao kwa mkapa mapato yatatokea wapi??

Ndiyo maana Eng Hers alisema "tutajenga uwanja mdogo kwa mechi kubwa tutazipeleta kwa Mkapa"
Kwa kauli hii unaona kabisa ni maelekezo ya wasimamizi wa uwanja wa mkapa nao wanataka kula kupitia uwanja wao.

My take Simba sc na Yanga Sc siyo kwamba wanashindwa kujenga uwanja Ila kikwazo ni mkapa studium Hilo halina kipingamizi.

Nawasilisha hoja.
 
Kujenga uwanja wa maana ni at least 20B, huo ni wa watu 7000 - 10,000/-

Je mapato ya hizo team yanatosha? Yanga mwaka jana hakuweza hata kidhi bajet yake mwenyewe ikabidi akope 5B, huu mwaka kaongeza bajet sijui atakopa kiasi gani zaidi,

Kuhusu Uwanja wa Benjamin usijipe matumaini, match pekee yenye pesa ni Simba Vs yanga Vs Azam,
Hizo mech nyingine hata mashabiki buku hawafiki na ndo mana hata hao Yanga na Simba wanaona uvivu kujenga uwanja wakati watu hawaend uwanjani,
Wakiweza pata average ya mashabiki japo 7k per match am sure watajenga uwanja wao
 
Back
Top Bottom