Mapendekezo kutatua tatizo la Dollar Tanzania

Elimu bora
 
Dhahabu unazo ila ununua. Hiyo migodi waliyobinafsisha ina faida gani?
Tanzania ingekuwa ina chimba dhahabu yenyewe na kuuza, dollar zingekuwa nje nje
Hivyo hivyo kwa gesi ya Mtwara, Almasi, na Tanzanite.
 
[emoji122][emoji122][emoji122] mifumo kubadili pesa now ni migumu
 
1) Tuzalishe zaidi na tuuze nje
2) Tupunguze kununua nje hata vitu vinavyoweza tengenezwa nchini
3) Elimu itolewe watu wapende vitu vya Tanzania.
4) Makampuni ya huduma ya nje yafanyayo kazi hapa nchini yawe na account za dollar hapa hapa na yalipiwe kwenye account hizo.
5) Kuwe na uratibu wa makini wa namna ya kuanzisha na kutekeleza miradi inayotegemea materials toka nje ya nchi. Miradi hii isianzishwe kiholela.
6) Kuanzishwe matumizi ya sarafu ya nchi husika kule tunakonunua vitu kwa wingi. Kama Rupiah = India, Yuan=China, n.k. badala ya matumizi ya dollar.
 
lazima tupate viongozi wenye maono na uwezo wa kuongoza.Kiongozi wa nchi kusema tutafute Mchawi kwa nini Asia wanaendelea kuliko sisi it means juu tumepwaya sana......gap ya import na export inazidi kutanuka sana na itaendelea kutanuka na uwezo wetu wa kucontrol ni mdogo sana.
 
Wawatafute manguli wa Forex kama 100 HV
Kila mmoja wampe mtaji wa Dolla 100000 wapambane
Ndani ya mwezi hatukosi 10M USD,mdogo mdogo tunaongeza reserve yetu
 
Hiyo ya utalii na dhahabu zimekaa poa ongezea na mazao ambayo nchi inaweza kuyauza nje ni vema serikal ikaongeza nguvu kusapot wazawa mfano ngozi,pemba korosho nk,kuhusu madini serikali kupitia bunge watunge sheria rasilimali zote za nchi ziuzwe nchini wanunuzi waje wanunulie uku sio unachimba madini unajaza kwny ndege yanaenda kuuzwa nje wewe unabaki kusema hatuna tunachouza nje while mwenzako mwarabu anauza mafuta kwa dola wewe unashindwa nn kwny madin?
 
Mawazo bado ni ya bure kwa viongozi wetu badala ya kushinda kudanganya watu kuhusu Dollar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…