Mapendekezo: Shule ya za Sekondari Benjamin, Msingi Uhuru na Kiwanda cha Bia zihamishwe Kariakoo waachiwe wamachinga hilo eneo

Mapendekezo: Shule ya za Sekondari Benjamin, Msingi Uhuru na Kiwanda cha Bia zihamishwe Kariakoo waachiwe wamachinga hilo eneo

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2011
Posts
3,763
Reaction score
5,607
Kuanzia roundabout ya Uhuru hizo shule zote napendekaza ziondolewe zitafutiwe eneo lingine lipishe wamachinga walioratibiwa.

Kiwanda cha bia hakina sababu ya kukaa katikati ya jiji, kiamishwe kipishe wafanyabiashara.

Maeneo hayo yajengwe majengo simple ya kisasa yenye vizimba vya kimkakati ambapo wamachinga watawekwa na kuchangia kiasi rafiki.

Pia Kariakoo bado inamahekari ya maeneo yaliyowazi kuliko wengi wanavyofikiri. Tuiongezee kariakoo yote floor moja juu. Biashara zote zinafanyika chini.

Napendekeza kama lilivyojengwa daraja kubwa la treni juu zitengenezwe njia na mitaa rafiki hata kwa chuma ili watu wawe wanapandisha juu na kuendelea na biashara kwa juu. Mitaa hiyo iunganishwe na floor za juu za magorofa ambayo maduka yaliyolala yataamka. Vile vyumba vilivyogeuzwa stoo vitakuwa maduka. Lakini katika mitaa ya juu inaweza kutengenezwa vizimba maelfu kwa ajili ya wamachinga pia.

Tusifikilie kutengeneza matatizo, tufikilie kuyatatua kwa maumivu rafiki.

unadhani nini kifanyike. Karibu kwa maoni yako na wewe.

NOTE: Rais wa Singapore mzee Lee Kuan Yew aliwahi kuhamisha ikulu mjini ili kupisha wafanyabiashara, kuhamisha kiwanda na shule ili kuongeza mapato na kuwahudumua vijana wanaomaliza vyuo bila hatia ni baraka kwa taifa.
 
Kuanzia roundabout ya Uhuru hizo shule zote napendekaza ziondolewe zitafutiwe eneo lingine lipishe wamachinga walioratibiwa.

Kiwanda cha bia hakina sababu ya kukaa katikati ya jiji, kiamishwe kipishe wafanyabiashara.
Kwani machinga ni walipa kodi?

Serikali haifaidikii na pato Lao ivyo ni hasara zaidi kuliko faida
 
Magulio yaliyopangwa yaanzishwe ktk kila manispaa zilizipo ndani ya miji, hii ndiyo dawa pekee ya kuwaondoa machinga wasiopangwa mabarabarani, chinga waliopo ktk uzio wa shule, vyuo, mahospitali, sehemu au nyumba za ummaa kama maofisi, nyumba za ibada n.k
 
Biafra lipo tayari

Ova
 
Akili za CCM ndio hizi. TBL investment yao ni shilingi ngapi? Wakisimama uzalishaji kwa siku moja NI hasara ya kiasi gani?
Je wanalipa Kodi kiasi gani ukilinganisha na machinga?

Msilifanye swala la machinga mtaji was kisiasa
Kuanzia roundabout ya Uhuru hizo shule zote napendekaza ziondolewe zitafutiwe eneo lingine lipishe wamachinga walioratibiwa.

Kiwanda cha bia hakina sababu ya kukaa katikati ya jiji, kiamishwe kipishe wafanyabiashara...
 
Ndio muda wa kutumia zile open space sasa kila mtaa na kuweka temporary structures za ku-accommodate hawa chingas.
 
Shule kuhamishwa napinga; kiwanda cha bia sawa kiko mjini mno kwa sana ila sio kwa ajili ya kupata eneo la machinga! Machinga ni nature ya shughuli zao kutembeza bidhaa zao mikononi; sio permanent settlement.
 
Kwa mgeni kutoka sehemu ya mbali anaweza kuona vipaumbele vipo mbele nyuma

Machinga Kwanza

Alafu Elimu na Viwanda baadae!

Huenda akajiuliza kwa kuwa na hayo mawili chini ya Machinga yasipewe kipaumbele? huenda kwa kufanya hivyo tunsingehitaji kuhamisha kitu ili hao watu wapate nafasi (sababu wasingekuwepo)
 
Naona wengi mmezoea wale wamachinga wajinga kutoka vijijini ambao hukimbilia mijini.

Hapana, wamachinga wa leo wengi ni wasomi na ni jeshi kabisa la vijana waso na ajira rasmi.

Serikali ya CCM nayo imeingia mkenge kwa kukurupuka kutatua tatizo hili la hawa wamachinga wasomi.

Suala la wamachinga litatuliwe kisomi na kiueledi.

Hili suala ni la dharura na laingia moja kwa moja kwenye usalama wa taifa.
 
Mtoa ushauri kama huyu ndo anasababisha chinga kufukuzwa mjini.

Nami napendekeza chinga wapelekwe kilwa au chattle huko wahamishe burigi.
 
Kuanzia roundabout ya Uhuru hizo shule zote napendekaza ziondolewe zitafutiwe eneo lingine lipishe wamachinga walioratibiwa.

Kiwanda cha bia hakina sababu ya kukaa katikati ya jiji, kiamishwe kipishe wafanyabiashara.
Hivi hao Machinga mbona mnataka wapendelewe kwa lipi haswa? uchafu wao au kukwepa kodi ? maana nchi nzima imegeuka kuwa machinga hadi wamekuwa kero. Mbona soko la Congo lilipohamishwa karume tumeenda sana na hao wapumbavu wakauza huko karume wakarejea congo na msimbazi wamezuia hadi services road ni watu wazuri hao?

ts same na wale wa jangwani kwenye mafuriko nasema wapangwe na walipo kodi. Sisi tunalipishwa Zimamoto, Osha, Takataka,Kodi ya Mapato, kodi za pango na tozo juu, leseni, Ulinzi shirikishi, VAT, Payee, Daswaco,Luku yenye ewura humo, na kodi zingine wao hawalipi kitu kuchafua maeneo, kuziba mifereji, kuziba services road makelele too much alafu eti wapewe maeneo ya shule na kiwanda hivi mna akili au mapunguani? kaombeni leseni za biashara acheni issue za dhulma
 
Kwa mgeni kutoka sehemu ya mbali anaweza kuona vipaumbele vipo mbele nyuma

Machinga Kwanza

Alafu Elimu na Viwanda baadae!

Huenda akajiuliza kwa kuwa na hayo mawili chini ya Machinga yakapewa kipaumbele huenda tunsingehitaji kuhamisha kitu ili hao watu wapate nafasi (sababu wasingekuwepo)

Una akili sana
 
Mimi naona toka kituo cha Polisi Msimbazi mpaka sokoni Kariakoo nyumba kuukuu za NHC zivunjwe pajengwe mall hata floor sita wamachinga wapewe vizimba. Kwa sasa waachiwe kwa muda mpaka mradi ukamilike
 
Yaani tuhamishe shule na kiwanda kuwapisha wakwepa Kodi?

Waache kuiibia serikali mapato. Wakachukue leseni wafanye biashara rasmi serikali ipate Kodi. Over
 
Back
Top Bottom