Mapendekezo ya CCM kuhusu kwa tume ya katiba haya hapa ....

Mapendekezo ya CCM kuhusu kwa tume ya katiba haya hapa ....

Haki sawa

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2007
Posts
4,781
Reaction score
3,210
Naomba kuwaletea baadhi ya vipengele ambavyo CCM wametoa mapendekezo yao kwenye tume ya Warioba ...makubwa yaliyopo ni kuhakikisha kuwa status quo inaendelea kuwepo kama hali ya sasa kuanzia kwenye Muungano na madaraka ya Rais .

katika kifungu 25(2)...wao wanasema kuwa kusafirisha binadamu sio kosa kisheria , hivyo lisping we maarufuku na katiba

kifungu, 62 Znz iruhusiwe kujiunga na Jumuiya za Kimataifa kama UN, FIFA .nk , kuwa ni ili kupungua kero za Muungano, ila hawataki Tanganyika iwepo

kifungu, 69 (4) kinachohusiana Rais kujinasibisha na chama chake wanasema kifutwe kwani mara nyingi Marais huwa ndio wenyeviti wa Chama .......

Kifungu, 93(2), idadi ya Mawaziri wanasema iwe 20 .......

kifungu, 94(2), kinachokatwa mgombea urais walau awe na shahada ya kwanza , wanasema kifutwe kwani sio lazima kuwa na elimu ili uwe Rais boboar kifungu,

kifungu 107 , kinachotoa fursa kwa Bunge kuithinisha mikataba mikubwa kuhusu rasilimali za taifa , wanasema kifutwe kwani hilo sio jukumu la Bunge bali la Serikali....

kifungu, 105 , wanasema wabunge wa Muungano wawe 360 na kwa suala wa 50/50 wanaume na wanawake ......where on Earth ........

kifungu, 106 (2), wabunge waendelee kulipwa mishahara hata baada ya Bunge kuvunja na kulipwa vinu a mhongo vyao .....eti mpaka Bunge jipya lipatikane......

kifungu, 122(1)(d) ...kuhusu mtu kukosa sifa ya kuendelea kuwa mbunge endpoint amepangiwa na matatizo ya akili , wanasema kifutwe kwani huo ni ugonjwa kama mwingine.

Kifungu 124, wananchi wasiwe na haki ya kuwawajibisha wabunge , hivyo kifutwe na kisiwepo

kifungu, 133(1) ,katibu wa Bunge aendelee kuteuliwa na Rais na sio kamisheni ya Bunge.....eti awe huru katika utendaji na kama atateuliwa na kamisheni ya Bunge hata kuwa huru , .....mbona Rais anateua katibu mkuu kiongozi .....kwanini huyo wanaona atakuwa huru?

Vifungu vya 224-229-234 , uteuzi wa wakuu wa vyombo vya usalama wateuliwe na Rais kama ilivyo leo.

kuhusu Muungano.
wanataka Muungano wa Serikali mbili na hoja zao ni kama ifuatavyo;
1. Kisheria , kwa kuwa hati za Muungano zimekuwa rejea ya rasimu
2. Serikali 3 zitakuwa na utata katika kusimamia na kuendesha Uchumi n hivyo kuleta mgongano
3. Tanganyika itachangia zaidi kuendesha serikali tatu kutokana na uchumi wake na hivyo kuivuruga Zanzibar .....vipi kuhusu serikali mbili........
4. Jamii imepanga na sana kwa kuoleana na kuishi pamoja .......so

haya ndio sehemu ya mapendekezo ya CCM yalivyowasilishwa na Asha Rose Migiro Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu rasmu ya katiba .
 
kweli ulevi wa madaraka ni ulevi mbaya kuliko aina yoyote ile, tazama kifungu cha 124 hapo......

Ila wakae wakijua kuwa kila jambo linamwisho wake... Huwezi kuzuia mafuriko........
 
kweli ulevi wa madaraka ni ulevi mbaya kuliko aina yoyote ile, tazama kifungu cha 124 hapo......

Ila wakae wakijua kuwa kila jambo linamwisho wake... Huwezi kuzuia mafuriko........
Wanasema kama wananchi hawataridhika na mbunge wana fursa ya kumuondoa baada ya miaka mitano ya uchaguzi, .....hii ni aibu kubwa kuwa na mlango wa kuingia ila wa kutokea haupo , ndio maana wanaendelea kuuza madawa ya kule ya ......hawataki kubugudhiwa ...
 
Mhhh!!

No wonder she was fired..................... Anabebeshwa tu zigo kama Mnyamwezi anakubali!!??
 
Vikao vya ndani vilivyojumuisha wanachama 2 mil :help:
 
Mapendekezo ndio hayo waliyowasilisha kwenye Tume , na anayetaka kubisha na ajitokeze sasa kwani huo ndio ukweli wenyewe

Haki Sawa, siyo nia yangu kubisha..

Najaribu kujiuliza hawa jamaa wanaishi dunia ipi?..wanawezaje kuwa na mawazo aina hii, hii ni katiba itakayo watumikia wao, watoto wao na wajukuu, wameshindwa kuweka UZALENDO mbele, inasikitisha
 
Haki Sawa, siyo nia yangu kubisha..

Najaribu kujiuliza hawa jamaa wanaishi dunia ipi?..wanawezaje kuwa na mawazo aina hii, hii ni katiba itakayo watumikia wao, watoto wao na wajukuu, wameshindwa kuweka UZALENDO mbele, inasikitisha
Uzalendo kwao ni msamiati mpya sana na hawaielewi hiyo lugha inaitwa Uzalendo....
 
Wanasema kama wananchi hawataridhika na mbunge wana fursa ya kumuondoa baada ya miaka mitano ya uchaguzi, .....hii ni aibu kubwa kuwa na mlango wa kuingia ila wa kutokea haupo , ndio maana wanaendelea kuuza madawa ya kule ya ......hawataki kubugudhiwa ...

Hapana wananchi lazima wapewe uwezo wa kisheria wa kuwatengua wabunge vilaza, hii lazima ipite
 
Uzalendo kwao ni msamiati mpya sana na hawaielewi hiyo lugha inaitwa Uzalendo....

Hapa Mzee wetu Warioba na tume kwa ujumla wanahitaji sala zetu ili mwenyezi mungu awaongoze vyema bila pressure kutoka vyama vya siasa.
 
Mwananchi mil 2.....walitoa maon hayo, na viongoz wao wakakaa Dodoma kuyasahihisha ili yawe bora zaidi, kumbuka ndio tuna viongozi wengi wa serikali waliotoa na kupitisha maoni haya......
May be is the reason why TZ is poor
 
Kama ni kweli basi hawa jamaa inabidi wafanyiwe uchunguzi juu ya bongo zao.

Nafikiri kifungu hiki alichangia Mwigulu Nchemba maana kwa videmu ni kiwembe jamaa yetu...

kifungu, 105 , wanasema wabunge wa Muungano wawe 360 na kwa suala wa 50/50 wanaume na wanawake ......where on Earth ........
 
Kifungu cha 122(1)d mbunge aliechaguliwa na wananchi hata kama akienda jalalani kuchakuachakua chakula kutokana na upungufu wa akili alionao wapiga kura wake waendelee kumsubili mpaka atakapo maliza.
 
Lissu , anawalipua CCM Bungeni muda huu kuhusu jinsi CCM walivyokataa kuunga mkono rasimu ya Warioba .
 
mbona wanaCCM hamkanushi, kuhusu hayo madai kama ni uongo semeni basi tuwasikie. Ila ikumbukwe kuwa nchii hii ni ya WATZ wote
 
kifungu cha 107, mikataba yote mikubwa iidhinishwe na bunge kifutwe na kubaki jukum la serikali'' kwel hawa watu ni mambumbumbu, ndo sababu nchi ipo gizan. Yaani hiki ndicho walichopanga na mwenykit wao akaridhia? nafsi yangu inaamin kuwa haya si maoni ya wananchi, bali ni ya ccm na viongoz wake, na hata maoni walokua wanakusanya ni ufisadi m2pu.
 
hiyo yote waliosaini kwa ajili ya kubadilishana waliopaswa kunyongwa haijawatosha? Nchi lazima ikombolewe. Ma... Yao...
 
Back
Top Bottom