Mapendekezo ya China yaendana na “Mkataba wa Zama Zijazo” wa Umoja wa Mataifa

Mapendekezo ya China yaendana na “Mkataba wa Zama Zijazo” wa Umoja wa Mataifa

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
无标题.jpg

Mkutano wa Kilele wa Zama Zijazo wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulipitisha “Mkataba wa Zama zijazo”, ambao unaelezea muhtasari wa maendeleo ya siku zijazo duniani. Lengo la Mkataba huo ni kuboresha mfumo wa usimamizi wa dunia, na kustawisha utaratibu wa pande nyingi, ili kukabiliana vizuri na changamoto mbalimbali zinazokabili binadamu katika zama mpya. Mkataba unaendana sana na mapendekezo mengi ya China.

“Mkataba wa Zama Zijazo” unatoa picha bora ya siku zijazo, ambapo dunia itaepuka matumizi mabaya ya silaha hatari, na kuwa na amani na utulivu zaidi, utaratibu wa pande nyingi utafuatwa zaidi katika mambo ya kimataifa, na nchi zinazoendelea zitakuwa na sauti zaidi katika mashirika ya kimataifa ya fedha, dunia itapata nishati mpya na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, dunia itatekeleza ushirikiano wa kidijitali na kuwa na usalama wa mtandaoni.

Katika miaka mingi iliyopita, China siku zote imekuwa inaunga mkono Umoja wa Mataifa kufanya kazi zaidi katika mambo ya kimataifa. Wakati mkutano huo wa Umoja wa Mataifa ulipofanyika, misimamo na mapendekezo ya China yamefuatiliwa, na busara nyingi za China zimewekwa kwenye “Mkataba wa Zama Zijazo” uliopitishwa kwenye mkutano huo.

Baada ya kuingia kwenye zama mpya, jumuiya ya kimataifa inakabiliwa na suala kuu la aina gani ya dunia, na namna ya kuijenga. China imetoa jibu la kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa binadamu. “Mkataba wa Zama Zijazo” unatupia macho siku zijazo, na ustawi wa binadamu wote, na kutoa maoni ya kiujenzi, ili kuhimiza pande zote kufanya juhudi kwa pamoja. Wakati huo huo, China imetetea kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu, na kutekeleza mapendekezo ya maendeleo ya dunia nzima, usalama duniani, na staarabu duniani.

Katika suala la maendeleo, “Mkataba wa Zama Zijazo” unasisitiza kutimiza maendeleo endelevu, na kutoacha nchi yoyote nyuma. Watu wa hali mbalimbali duniani wameeleza kuwa China imejizatiti kujenga majukwaa muhimu ya ushirikiano duniani, kuhimiza ushirikiano wa kivitendo kati ya nchi zinazoendelea katika nyanja mbalimbali, na kuchangia katika kuhimiza mfumo wa utawala wa kimataifa kuwa na haki na usawa zaidi.

Suala la amani na usalama huwa ni mjadala mkubwa katika vikao vya Umoja wa Mataifa. Kuhusu suala hili, China inasisitiza kwamba nchi yoyote haipaswi kuharibu usalama wa nchi nyingine ili kulinda kabisa usalama wake wenyewe, kwani kitendo hiki hakisaidii amani na usalama kweli duniani. “Mkataba wa Zama Zijazo” pia umetaja usalama wa anga ya juu, na kusisitiza nchi mbalimbali duniani zinapaswa kutumia anga za juu kwa njia ya amani. China siku zote inapinga kuendeleza uwezo wa kijeshi kwenye anga ya juu, na imeshirikiana na nchi nyingine kubwa kuanzisha sheria za kimataifa ili kuhakikisha matumizi ya amani ya anga za juu.
 
Back
Top Bottom