Mapendekezo ya mabadiliko katika vifungu vya Sheria ya Bima

Mapendekezo ya mabadiliko katika vifungu vya Sheria ya Bima

Mbute na chai

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
564
Reaction score
593
Mapendekezo haya nayatoa kwa TIRA.

Mabadiliko ninayopendekeza ni kwamba, kuwepo na rudisho (return of some proceeds) la fedha kwa mchangiaji wa bima inayoisha muda wake bila janga kutokea.

SABABU ZA MAPENDEKEZO HAYA

1. Kuepusha mianya ya rushwa.

Mmiliki wa gari yuko radhi kumshawishi askari kupokea rushwa ya tsh 5000 ili asimwandikie faini ya kuendesha gari isiyo na bima. Hii ni kwa sababu mmiliki hulipa bima kila mwaka na huku gari haipati ajali hivyo ni kama analichangia shirika la bima tu bila kupata faida ya bima hiyo. Hivyo, kukiwa na rejesho fulani la fedha baada ya muda wa bima kuisha kwa wateja ambao magari yao hayajapata majanga kutaleta hamasa kwa watu kulipia bima na serikali itapata tozo yake.

2. KUEPUSHA USUMBUFU WAKATI WA AJALI

Usumbufu ni kama kushindwa kulipa gharama za uharibifu wa gari au madhara aliyopata mtumiaji mwenza wa barabara. Hii inatokana na watu wengi kukwepa kulipia bima kutokana na hofu kuwa fedha hiyo itaenda bure.

3. KUPIGA VITA UMASKINI.
Mfano mzuri ni yule mama ambaye lori lake lilitumbukia mto wami na kupata msaada kutoka JWTZ. Kilio alichoonesha kwenye vyombo vya habari ni ushahidi tosha kuwa hakuwa na bima ya kumwezesha kufidiwa gari nyingine hivyo alirudi kwenye umaskini.

KUKIWA NA REJESHO LA ASIMILIA HATA HAMSINI WATU WENGI WATAKA BIMA YA VYOMBO VYAO VYA MOTO NA CHANGAMOTO YA VYOMBO VINGI, HASA VYA WATU BINAFSI, KUTOKUWA NA BIMA ITAPUNGUA KAMA SIYO KUISHA.

Karibuni kwa maoni kingazani.
 
Hicho ulichoandika hakipo duniani, kumbuka unaweka bima kiasi kidogo sana kuliko gharama halisi ya kitu.

Mfano bima ya nyumba yenye thamani ya tsh 100M utachangia tuseme tsh 200k kwa mwaka, sasa ikiwa hela itakuwa inarudishwa, siku kukitokea janga la hiyo nyumba kuungua, fedha ya kufidia gharama itatoka wapi?.

Bima ambayo naona inapaswa kurudishwa kwa mhusika, ni bima ya mkopo, ikitokea ukamaliza rejesho lako ilipaswa kile kiasi kilichokatwa kirejeshwe kwa mhusika.

Bima za magari, nyumba, viwanda, meli et al tuendelee kulipa maana tulipacho ni kidogo, tunachangiana kwa mwenzetu anayepatwa na majanga.

Wale wenzangu na mimi tunaoumizwa na mifumo mibovu ya fidia hususani kwa vyombo vya moto, hapo tunapaswa kuilaumu serikali kushindwa kumtetea mlaji pindi makampuni ya bima yanapompiga danadana mteja.
 
Naongezea
Kiundwe chama cha wakata bima.
Hiki kitetee wakataji wa bima pale wanapopata changamoto na mashirika ya bima kupiga danadana kulipa kwa wkt.
 
Back
Top Bottom