Bemendazole
JF-Expert Member
- Nov 14, 2020
- 2,649
- 6,680
MAPENDEKEZO YA MABORESHO YA MFUMO WA UENDESHAJI WA MABASI YA MWENDO KASI
Mabasi yaendayo haraka ni mradi uliobuniwa kurahisisha huduma za usafiri kwa wakazi wa majiji makubwa yenye msongamano mkubwa wa magari na watu.
Tangu kuanzishwa kwa huduma hii kumekuwepo na changamoto za kimiundombinu pamoja na changamoto za kiuendeshaji.
Nia ya andiko hili ni kuota nafasi ya wataalam na wadau wengine wa sekta ya usafirishaji kuzingatia nama ya kuboresha huduma za usafiri wa mwendo kasi ili kumrahisishia mtumiaji wa huduma hizi pamoja na kuwasaidia watoa huduma za usafiri kwa kutumia mabasi yaendayo haraka.
Utatuzi
Wakati najaribu kuangalia ni namna gani tungeweza kuboresha utaratibu wa huduma hizi, ilibidi niangalie jinsi mabasi haya yanavyofanya kazi. Kwa sasa mabasi haya hufanya kazi kwa kuanzia point A na kuishia point B. Yote yanafanya kazi kwa kufuata mzunguko unaofanana.
Hapo ilibidi nijiulize pia, kama sayari zote zinasafiri kuelekea katika uelekeo mmoja, kwa nini kila sayari iliundwa kutembea kwenye orbiti yake?
Hapo ndipo nilipopata jibu kuwa ili kuboresha mfumo wa uendeshaji wa mabasi haya, inabidi mabasi yasafiri katika mfumo wa orbit. Yani mabasi yaanze point tofauti na kusihia point tofauti ili kupunguza umbali ambao basi moja linapaswa kusafiri, pia kuwasaidia wasafiri wanaonazia kwenye vituo vya kati kati kupata usafiri ukiwa una nafasi ya kukaa au hata kusimama.
Kupunguza umbali wa mabasi haya kusafiri kutaokoa gharama kwa kupunguza muda ambao basi litalazimika kusafiri, kupunguza gharama za mafuta, kuliwezesha basi linalosafiri safari fupi fupi kufanya mizunguko ziadi na pia kupunguza gharama za uchakavu (wear and tear).
Nilipoliangalia jiji la Dar Es Salaam kwa ujumla wake, iwapo mfumo huu wa uendeshaji utazingatiwa, kwa mwaka gharama za takribani bilioni tano zingeweza kuokolewa kama nilivyokwisha kueleza hapo juu.
Picha No 1: mfumo wa uendeshaji mabasi ya mwendo haraka kwa mfumo wa ‘orbital module
Maelezo ya picha:
Katika picha hii, utaona kuwa basi No moja litaanzia mwanzo wa safari na kuishia mwisho wa safari
Basi namba mbili litaanzia vituo vitatu baaada ya kituo cha mwanzo na litaishia vituo vitatu kabla ya kituo cha mwisho wa safari.
Mwendelezo utaendelea hivyo kwa vituo vyote:
Ili kuweka taarifa nyingi (complex information) kwenye lugha rahisi, nimechora majedwali yakionesha ni kituo gani basi litaanzi ana kituo gani basi litaishia. Vituo vyote nimevipa namba kunazia namba moja mpaka namba ishirini na moja ili kumwezesha mtoa huduma kutumia jedwali hili kwa bara bara tofauti tofauti. Namba inaweza kubadilishwa kwa kupewa jina la kituo halisi. Mfano namba moja ikasimama kuwakilisha kituo cha Kimara Mwisho na namba 16 ikasimama kuwakilisha kituo cha Gerezani.
Jedwali No 1: Mkeka wa vituo vya kupandia na kushushia abiria kwa bara bara yenye vituo 16
Wakati mabasi Namba moja hadi namba sita yanaanzia Gerezani, Basi namba saba hadi namba kumi kwa wakati huo huo yatakuwa yameanzia safari zake Kimara Mwisho hivyo kukamilisha mzunguko kwa usawa.
Madhara ya kuwa na vituo vingi vya kusimama na kupakia abiria
Kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini, kadri unavyokuwa na vituo vingi vya kupakia na kushusha abiria, mtoa huduma atalazimika kuwa na idadi kubwa ya mabasi tofauti na hapo juu ambapo yangehitajika mabasi sita yanayokwenda na mengine sita yanayorudi.
Ili kupunguza idadi ya mabasi yanayohitajika, mtoa huduama anaweza akaruka kutoa huduma kwenye vituo vilivyoko karibu karibu kama vile Fire na Jangwani ili kupunguza ulazima wa kuhitaji mabasi mengi.
Jedwali No2: Mkeka wa vituo vya kupandia na kushushia abiria kwa bara bara yenye vituo vingi (21)
Changamoto za mfumo huu wa ‘Orbital Module’
Changamoto kubwa niliyoiona kwenye mfumo huu ni namna ya mabasi marefu yanavyoweza kugeuza mara yanapofika mwisho wa safari, nikaonelea kuwa kuna mambo mawili yanaweza kufanywa.
Moja ni kuboresha maeneo ya vituo vya mwisho kwa kupanua mzingo wa bara bara ili kuruhusu mabasi yaweze kugeuza kwa urahisi au option ya pili ni kuhamishia bara bara za mwendo kasi ziwe upande wa nje na bara bara za kawaida ziwe upande wa ndani ili kutanua diameter na kuweza kuyaruhusu mabasi kugeuza kwa urahisi.
Picha No 2: Muonekano wa bara bara ya mwendo kasi na ule wa magari ya kawaida ambapo magari ya mwendo kasi yatapita kwenye upande wa nje na yale ya kawaida yatapita kwenye bara bara za ndani.
Hitimisho
Mpango huu umelenga kutatua changamoto za utoaji huduma wa mabasi yaendayo haraka ndani ya majiji makubwa, endapo utatekelezwa kama ilivyooelezewa hapa au kwa kuboresha, ni matumaini yangu utasaidia kwa kiasi kibubwa kuboresha huduma (service quality) pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji.
NB: Nime attach Chapisho hili kwa wadau kuweza kuona picha.

| 1 | Origin | 1 | 2 | 3 | 14 | 15 | 16 | Destination | |||||
| Destination | 1 | 2 | 3 | 14 | 15 | 16 | Origin | ||||||
| Mfano, basi No 1 litaanzia Gerezani, litasimama Msimbazi kupakia abiria na kushusha, litasimama Fire kupakia abiria na Kushusha kisha halitasimama sehemu yeyote mpaka litakapofika kituo cha Bucha ambapo litasimama kushusha abiria na kupakia abiria wanaoenda vituo vya mbele, tena litasimama kituo cha Korogwe kushusha abiria na kupakia abiria wanaoneda kituo cha mbele na mwisho gari litahitimisha safari kwenye kituo chake cha mwisho cha Kimara mwisho ambapo abiria wote watashuka na litageuza na kuanza safari kwa kufuata mtiririko huo huo. | |||||||||||||
| 2 | Origin | 1 | 2 | 3 | 11 | 12 | 13 | Destination | |||||
| Destination | 1 | 2 | 3 | 11 | 12 | 13 | Origin | ||||||
| Kama inavyoonekana kwenye jedwali, basi namba mbili litaanzia kwenye kituo cha Gerezani, litasimama kwenye kituo cha *Msimbazi kushusha abiria na kupakia abiria wanaokwenda kwenye vituo vinavyofuata, litasimama fire kupakia na kushusha abiria wanaokwenda kwenye vituo vinavyofuata. Baada ya hapo basi halitasimama sehemu yoyote mpaka mwisho wa safari ambapo litasimama kushusha abiria kwenye kituo cha Bucha ambapo litasimama kushusha abiria na kupakia abiria wanaoenda vituo vya mbele, tena litasimama kituo cha Korogwe kushusha abiria na kupakia abiria wanaoneda kituo cha mbele na mwisho gari litahitimisha safari kwenye kituo chake cha mwisho cha Kimara mwisho ambapo abiria wote watashuka na litageuza na kuanza safari kwa kufuata mtiririko huo huo. Mtiririko huu utaendelea kwa vituo vyote kama vilivyooneshwa kwenye jedwali. Nimetumia majina ya vituo ila sina uhakika na ushahi wa majina au mpangilio wa vituo husika. | |||||||||||||
| 3 | Origin | 1 | 2 | 3 | 8 | 9 | 10 | Destination | |||||
| Destination | 1 | 2 | 3 | 8 | 9 | 10 | Origin | ||||||
| 4 | Origin | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 | Destination | ||||
| Destination | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 | Origin | |||||
| 5 | Origin | 16 | 15 | 14 | 6 | 5 | 4 | Destination | |||||
| Destination | 16 | 15 | 14 | 6 | 5 | 4 | Origin | ||||||
| 6 | Origin | 16 | 15 | 14 | 9 | 8 | 7 | Destination | |||||
| Destination | 16 | 15 | 14 | 9 | 8 | 7 | Origin |
Wakati mabasi Namba moja hadi namba sita yanaanzia Gerezani, Basi namba saba hadi namba kumi kwa wakati huo huo yatakuwa yameanzia safari zake Kimara Mwisho hivyo kukamilisha mzunguko kwa usawa.
| 7 | Origin | 16 | 15 | 14 | 13 | 12 | 11 | 10 | Destination | ||||
| Destination | 16 | 15 | 14 | 13 | 12 | 11 | 10 | Origin | |||||
| 8 | Origin | 4 | 5 | 6 | 10 | 9 | 8 | 7 | Destination | ||||
| Destination | 4 | 5 | 6 | 10 | 9 | 8 | 7 | Origin | |||||
| 9 | Origin | 4 | 5 | 6 | 10 | 11 | 12 | 13 | Destination | ||||
| Destination | 4 | 5 | 6 | 10 | 11 | 12 | 13 | Origin | |||||
| 10 | Origin | 7 | 8 | 9 | 11 | 12 | 13 | Destination | |||||
| Destination | 7 | 8 | 9 | 11 | 12 | 13 | Origin |
Madhara ya kuwa na vituo vingi vya kusimama na kupakia abiria
Kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini, kadri unavyokuwa na vituo vingi vya kupakia na kushusha abiria, mtoa huduma atalazimika kuwa na idadi kubwa ya mabasi tofauti na hapo juu ambapo yangehitajika mabasi sita yanayokwenda na mengine sita yanayorudi.
Ili kupunguza idadi ya mabasi yanayohitajika, mtoa huduama anaweza akaruka kutoa huduma kwenye vituo vilivyoko karibu karibu kama vile Fire na Jangwani ili kupunguza ulazima wa kuhitaji mabasi mengi.
Jedwali No2: Mkeka wa vituo vya kupandia na kushushia abiria kwa bara bara yenye vituo vingi (21)
| 1 | Origin | 21 | 20 | 19 | 3 | 2 | 1 | Destination | |||||
| Destination | 21 | 20 | 19 | 3 | 2 | 1 | Origin | ||||||
| 2 | Origin | 21 | 20 | 19 | 6 | 5 | 4 | Destination | |||||
| Destination | 21 | 20 | 19 | 6 | 5 | 4 | Origin | ||||||
| 3 | Origin | 21 | 20 | 19 | 12 | 11 | 10 | Destination | |||||
| Destination | 21 | 20 | 19 | 12 | 11 | 10 | Origin | ||||||
| 4 | Origin | 21 | 20 | 19 | 15 | 14 | 13 | Destination | |||||
| Destination | 21 | 20 | 19 | 15 | 14 | 13 | Origin | ||||||
| 5 | Origin | 21 | 20 | 19 | 18 | 17 | 16 | Destination | |||||
| Destination | 21 | 20 | 19 | 18 | 17 | 16 | Origin | ||||||
| 6 | Origin | 21 | 20 | 19 | 9 | 8 | 7 | Destination | |||||
| Destination | 21 | 20 | 19 | 9 | 8 | 7 | Origin | ||||||
| 7 | Origin | 6 | 5 | 4 | 3 | 2 | 1 | Destination | |||||
| Destination | 6 | 5 | 4 | 3 | 2 | 1 | Origin | ||||||
| 8 | Origin | 9 | 8 | 7 | 3 | 2 | 1 | Destination | |||||
| Destination | 9 | 8 | 7 | 3 | 2 | 1 | Origin | ||||||
| 9 | Origin | 12 | 11 | 10 | 3 | 2 | 1 | Destination | |||||
| Destination | 12 | 11 | 10 | 3 | 2 | 1 | Origin | ||||||
| 10 | Origin | 15 | 14 | 13 | 3 | 2 | 1 | Destination | |||||
| Destination | 15 | 14 | 13 | 3 | 2 | 1 | Origin | ||||||
| 11 | Origin | 18 | 17 | 16 | 3 | 2 | 1 | Destination | |||||
| Destination | 18 | 17 | 16 | 3 | 2 | 1 | Origin | ||||||
| 12 | Origin | 15 | 14 | 13 | 9 | 8 | 7 | Destination | |||||
| Destination | 15 | 14 | 13 | 9 | 8 | 7 | Origin | ||||||
| 13 | Origin | 12 | 11 | 10 | 9 | 8 | 7 | Destination | |||||
| Destination | 12 | 11 | 10 | 9 | 8 | 7 | Origin | ||||||
| 14 | Origin | 18 | 17 | 16 | 9 | 8 | 7 | Destination | |||||
| Destination | 18 | 17 | 16 | 9 | 8 | 7 | Origin | ||||||
| 15 | Origin | 9 | 8 | 7 | 6 | 5 | 4 | Destination | |||||
| Destination | 9 | 8 | 7 | 6 | 5 | 4 | Origin | ||||||
| 16 | Origin | 12 | 11 | 10 | 6 | 5 | 4 | Destination | |||||
| Destination | 12 | 11 | 10 | 6 | 5 | 4 | Origin | ||||||
| 17 | Origin | 18 | 17 | 16 | 6 | 5 | 4 | Destination | |||||
| Destination | 18 | 17 | 16 | 6 | 5 | 4 | Origin | ||||||
| 18 | Origin | 15 | 14 | 13 | 6 | 5 | 4 | Destination | |||||
| Destination | 15 | 14 | 13 | 6 | 5 | 4 | Origin |

Upvote
1