Mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali kuhusu nini kibadilike katika Mfumo wa Elimu ya Tanzania kupitia Twitterspace ya Jamiiforums

Ijulikane lugha moja ya kufundishia eng/kisw
Sababu elimu ni kutoa ujinga bas kila anaepata nafas ya kusoma asome hadi chuo kikuu
 

Wadau mbalimbali wa elimu wamekuwa wakilalamikia mfumo wa sasa wa Elimu ya Tanzania...
Hakuna haja ya kulimbikiza masomo ya miaka minne uje uifanyie mtihani mmoja (yaani masomo ya kidato cha kwanza hadi cha nne, kwa mtihani mmoja wa kidato cha nne), ni kuwabebesha mzigo watu na kuwafanya wakariri zaidi kuliko kusoma kwa kuelewa, mfumo mzuri ni kama utumikao vyuoni (kila kidato kiwe na mtihani wake, kisha unaweka pembeni, unaendelea ulipoishia), hapa tutazalisha waelewa wengi wenye tija kwa taifa katika kuleta maendeleo ya taifa.
 
Mfumo uwe hivi:

Serikali itambue rasmi lugha ya English kama lugha ya Taifa sambamba na Kiswahili.

Ama sivyo itambue rasmi kama lugha ya biashara ndani na kimataifa.

English inasaidia kuweka tabaka kubwa sana katika vizazi vya nchi hii kuanzia ngazi ya Daycare hadi Vyuo Vikuu.

Ndio maana Taifa lina mitihani ya aina mbili: Swahili medium & English medium.

Elimu Msingi: Darasa la 1 hadi 6.

Hakuna haja ya kuwa na Drs la 7 sababu uwepo wa Nursery umesaidia sana kufanya Darasa la 1 kama unnecessary.

Elimu Secondary: Form 1 hadi 4 (O & A level)

Uwepo wa English medium umefanya Form 1 & 2 kuwa kama sio necessary sana.

Hivyo madude ya F.5 na 6 yahamishiwe F.3 na F.4 ili kuondoa kabisa A level.

Ukosefu wa ajira umefanya msingi na secondary kukosa sababu ya kutumia muda mwingi wa watoto.

Hakuna sababu ya kidato cha 5 & 6. Mtu anasoma PCB akiwa A level halafu anakwenda kusoma Accountancy Degree haina mantiki yeyote.

Kimsingi A level haina logic kwenye ulimwengu wa sasa.

Then, elimu ya masuala ya fedha na biashara iwe necessary kuanzia drs la 4 hadi secondary.

Note: Sizungumzii ujasiriamali bali nazungumzia FEDHA & BIASHARA.

Entrepreneurship is wrongly interpreted kwa sababu wengi hawajui hasa what does it really means.

Kama unajua fedha na biashara automatically unajua entrepreneurship. Kujua entrepreneurship sio guarantee ya kujua fedha na biashara.

Mkazo utolewe zaidi kwenye professional degrees / Diplomas.

Kila baada ya miaka 3 kumaliza Degrees ama Diplomas kuwepo na mitihani ya ku continue learning kwa graduates.

Mfano: Kama umesoma let say Civil Engineering then after 3 years ama within 3 years kuwepo na specific exams za kuwafanya graduates waendelee kuwa up to dates....

Kwa Engineering Bodi ya Makandaradi wanaweza kusimamia hili.

Kwa madaktari Bodi ya Madaktari inaweza kuundwa specifically for exams kama zilivyo NECTA na NBAA na PSPTB

Mfano kwa uhasibu Bodi ya Uhasibu wanaweza kupewa jukumu la kusimamia hili.

Lengo ni kufanya graduates waendelee kuwa active na updated na masuala ya taaluma zao.

Yaani Continuing Learning Education iwepo kwa all graduates.

Issue za masters degree na phD ni mbwembwe tu hazina ishu yeyote; ni kama ilivyo kidato cha 6 tu haina ishu yeyote. Ishu ni Kidato cha 4 & Bachelor Degrees then Continue Learning Education (vyovyote mtakavyoita)

Na kusiwepo na gharama kwa wale jobless.

Mkifuata huu ushauri wangu mtazalisha Taifa lenye wasomi very relevant kwenye ujenzi wa Taifa hili.

Ila najua hamtazingatia coz hampo mitaani so hamjui chochote halisi kuhusu mitaa. Mpo kwenye viyoyozi na magari full tinted hamjui chochote huku site.

NB: Mnaweza kufanya Copy & Paste kuchukua mfumo wa nchi unaokubalika zaidi Duniani na kuhamishia kwetu. I recommend that as well coz hatujawahi kuwa na anything new kila kitu tuna copy na ku paste tu kibingwa. Na mostly tuna copy vibaya maana huwa hatufanyi updates
 
Tujifunze ujuzi, tuachane na taaluma haitusaidii ila ujuzi utatusaidia kujenga taifa, kuna wahitimu wengi wasio na ujuzi hata chembe, ila wana notisi na vyeti
Tukijifunza ujuzi bado tutahitaji taaluma, lazima tusome vyote. Mfano huwezi kuwa profesa kwa ujuzi tu lazima kichwa kijae theory za kuweza kufafanua vitu ndio utaweza kufundisha wasomi ngazi za huko juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…