Mapendekezo yoyote ya kuboresha Tume ya Uchaguzi yatainufaisha CHADEMA zaidi dhidi ya vyama vingine

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kilichopelekea Chadema kufanya vibaya uchaguzi uliopita pengine ni kukosa Uhuru wa Kufanya Siasa, Uhuru wa kuwafikia watu, uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara, uhuru wa mikutano ya ndani, na kikubwa zaidi ni muundo mzima wa uchaguzi.

Kwahiyo baada ya uchaguzi wa 2020, Chadema wakaanza kudai Katiba Mpya but the aim was to get what they were denied for a long time, TUMEHURU.

Kwa msingi wa ā€œShoot for the moon. Even if you miss it you will land among the starsā€, hata ukikosa Katiba angalau unaweza kuambulia Tumehuru.

Endapo Chadema itapata uhuru wa kufanya mikutano yao bila kuingiliwa na vyombo vya dola, iruhusiwe kufanya program zao freely, operation kama M4C, Chadema Digital, Join The Chain nk, kwa kutumia Katiba hii hii iliyopo hakuna chama kinaweza kushindana na Chadema kwa hoja kikiwemo Chama cha Mapinduzi.
 
Hii inaitwa ukichimama nchale ukikimbia nchale.

Kwa jinsi chadema ilivyojiimarisha haiepukiki
 
Kilichopelekea Chadema kufanya vibaya uchaguzi uliopita pengine ni kukosa Uhuru wa Kufanya Siasa. Uhuru wa kuwafikia watu, uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara, uhuru wa mikutano ya ndani, na kikubwa zaidi ni muundo mzima wa uchaguzi.
Kwakuwa umetumia neno 'pengine' basi nikubaliane nawe kwa asilimia 5. Chadema haikufanya vibaya, ilifanya vizuri tena vizuri sana kuliko miaka mingine ya nyuma, ila kila kitu kilivurugwa,kwa mabavu ya watawala.

Anza na uchaguzi wa serikali za mitaa, njoo uchaguzi mkuu. Kilichotokea kilionekana mbele ya macho yetu sote - ilikuwa aibu.
 
Endapo itatokea Chadema kushika madaraka kisha kukaendelea kwa hali hii ya wafuasi wa chadema pamoja na hii mitazamo yao juu ya chama chao basi kutakuwa hakuna tofauti na wafuasi wa Ccm hivi sasa na mitazamo yao juu ya chama chao kilichoshika madaraka.
 
Ukisoma bandiko langu vizuri nimesema matokeo iliyopata Chadema yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na mchakato mbaya wa uchaguzi.
 
Ya akinamkandala[emoji1787]

Umeulizwa swali la msingi: ā€œtume huru unaijua wewe?ā€. Usidhani ni kama ile vieite ya Polepole.

Usipojibu hili swali ipasavyo basi jua ulichoandika ni dhana ya kufikirika tu katika nchi hii ya kusadikika.
 

Ndio maana KATIBA MPYA ni muhimu.

Katiba iliyopo sasa hivi inatoa mianya kwa watawala kuwa miungu watu na kuongoza kwa matakwa yao ni si kwa matakwa ya sheria.
 
Ya akinamkandala🤣
Jakaya Kikwete aliwategemea sana akina Mkandara na REDET yao. Wakamdanganya kwa tafiti zao feki za kuchonga miaka yote kumi ya utawala wake matokeo yake CCM ikachukiwa sana....
Samia naye ameanza kuifuata njia ile ile. Kufika 2025 atakuwa ameshapata jibu lake
 
Kila mwaka ccm ikawa inapigwa za uso. Hata Samia hata pona mpaka pale atakapoamua kuungana na wananchi na kuachana na vikundi vichache vya ccm
 
Chadema inajitegemea. Inaweza kusimama na wananchi tu.
 
Naipenda sana Chadema ila wale vijana kina Martine[emoji16][emoji16][emoji16] mavi ya popo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…