Mapenzi bila pesa magumu

Raia mpya

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2022
Posts
673
Reaction score
1,915
Ndugu zangu wa kiume hivi ni kwangu mimi tu au na nyinyi inawakuta manaa dah nina mpenzi japo sina uhakika kama ni wangu kweli ila nisipompa pesa naona kabisa uchangamfu wake kwangu unapungua kabisa, hata simu kupiga haoigi anakuwa busy na sababu kibao na sio huyu tu ni demu wapili napata yupo hivi hivi bila pesa nakuwa sina tofauti na mtu aliye single😀
Sasa nawauliza ni huyu wangu au hata nyinyi mademu zenu ni hivyo hivyo?
 
Pesa inogeshe penzi lililosimama tayari, ila zisitumike kumvutia mwanamke awe na wewe
Nataka nijue ni kwamba wote wapo hivi au vip kuna rafiki yangu aliwahi kunambia mapenzi sio pesa na bla bla kibao na akatokea mfano mchumba wake kuwa anampenda japo hana pesa, hiyo ilikuwa 2020 , sasa nimekutana nae 2023 mwishoni kumuliza shemeji hajambo naona nae kubadilisha msimamo mapenz ni pesa
Kiufupi kakimbiwa😀
 
Sio pesa tu, kuwajibika kwa mwanaume ndio msingi wa mahusiano au ndoa. Ukishindwa kufanya hicho ujue hayo si mahusiano tena. Mapenzi waachie wenye pesa usije kupata msongo wa mawazo kisa kitu ambacho ukijipata kitakutafuta chenyewe.
 
Sio pesa tu, kuwajibika kwa mwanaume ndio msingi wa mahusiano au ndoa. Ukishindwa kufanya hicho ujue hayo si mahusiano tena. Mapenzi waachie wenye pesa usije kupata msongo wa mawazo kisa kitu ambacho ukijipata kitakutafuta chenyewe.
Uwajibikaji ukiacha tendo iasilimia kubwa inaangukia kwenye pesa,maana kila kitu hapo lazima uwe na hela
 
Hapo hakuna mapenzi

Tuseme kuna manzi amekukubali kwa sababu una pesa

Je, akija mwenye kibunda zaidi yako akamtongoza akikuacha utalalamika au utakubaliana na msemo kuwa mapenzi ni pesa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…