Daaah hatari Sana mpaka mabango,Huyu jamaa anahitaji ushauri wa kisaikolojia Wala sio kutumia nguvu.Ukiona mpaka ameandika hivyo kwenye bajaji ujue ameshindwa kuliweka moyoni Tena amevurugwa kwelikweli wataalamu wa saikolojia kazi kwenu sasa.Hivi kwa nini baadhi ya wazazi mnapenda kuingilia mahusiano ya watoto wenu? Chanzo Cha ndoa nyingi baadhi kuvunjika huwa ni wazazi,Yani wanandoa mkikosana tu kidogo mkipeleka kesi kwa wazazi hutoa maamuzi ya kuachana.je kuachana ndio solution? Unamuacha mke wako au mume wako eti kwa sababu wazazi wamesema achaneni ebu usikilize moyo wako unaamua Nini kusuka au kunyoa.Unampa mkeo au mme taraka kwa sababu ya maamuzi ya wazazi? Why.Ndoa ni kuvumiliana unapewa cheti mapema mtihani unafuata,yaani humo ndani ya taasisi ni milima na mabonde.