Mapenzi jamani mapenzi, huu mchezo utaniua bure!

Mapenzi jamani mapenzi, huu mchezo utaniua bure!

Curtis De Mi Amor

Senior Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
136
Reaction score
514
Unayempenda hakupendi! Unampa hela bado hakupendi. Leo yupo kwangu kesho kwako. Hivi babu zetu waliweza survive vipi? Unahudumia nayeye anamhudumia mwingine. Unamjaza mimba ukimuuzi anasema siyo yako.

Yaani ilimradi tuu yakutese wee, uteseke haswa. Ukisema ukae single basi lazima kuna kimtu kitajileta alimradi kaje kakutese. Sijui ni pepo gani la siri lipo hapa katikati.

Mnaweza mkapendana kweli ile ya dhati, ila from nowhere litatokea jitu lakuja kuharibu kabisa penzi lenu. Huu mchezo unaumiza kichwa ndio maana watu huishia kuuwa, kuuliwa na kujiua.

Moyo tulia, nakwambia moyo wangu tulia tena upunguze wenge la mapenzi sitaki presha na ujana huu.
 
Mcheki mwamba 👇
Screenshot_20220904-173733.jpg
 
Labda huna nyota ya kupendwa mkuu,chukua muda ujitafakari kwanza.

Tatizo la watu Mara nyingi hupenda kuongea the negative side ya wenza wao kwa lengo la kutuaminishi sisi kwamba wenza wao ndio wakosaji.
Huyo mpenzi wako akipewa nafasi ya kuongea bila Shaka lazima ataexpose the negative side of you.Hapa Duniani Hakuna mtu aliyekamilika.

Chukua muda wako ujitafakari kwanza ujue una mapungufu gani ambayo yanakufanya ushindwe kudumu kwenye mahusiano.
 
Back
Top Bottom