Mapenzi kamali. Leo nimepigwa tukio sijuhi nimueleweje

Mapenzi kamali. Leo nimepigwa tukio sijuhi nimueleweje

Tafuta pesa upunguze malalamiko.
Halafu ukumbuke kurudisha laki 6 ya watu sio yako hiyo.
Huyo mwanamke kashakutamkia anatoa penzi kwa jamaa japo sio mapenzi ya kweli ila anatmbwa kwa sababu ya pesa.
Hiyo itoshe kukuonesha kuwa hakuheshimu na hauna thamani yoyote na wewe sii chochote kwake ndio maana anaweza kufanya chochote anachotaka.
 
Wewe sema tu unataka hiyo pesa acha kuzunguka mara hivi mara vile.

Kama shida ni line yako mtumie pesa yake ubaki na line yako, wewe pesa yake ya nini?

Yani kumsajilia tu line unaona unastahili pesa alizoweka humo? We wala hufai kuwa mume wa huyo dada.
Kitonga...
 
Nilimsajilia line kwa jina langu, sasa nimegundua ananificha mwanaume mwingine... je, msamaha wake ni wa kweli?
Mwili wa Uzi:



Naomba msaada wa mawazo ya kweli kutoka kwa watu waliotulia na waliowahi kupitia maisha haya.

Niko kwenye mahusiano na dada mmoja ambaye nimekuwa naye kwa muda sasa. Kipindi fulani aliniomba nimsajilie line ya simu kwa jina langu kwa ajili ya kuhifadhi pesa lakini moyo ukawa unasita ni kama miaka 2 hv sasa week zilizo pita nikawa nime sajili ni ka mwambia line iko tayal lakin alikua bado ajaichukua , kwa sababu alisema anapata changamoto kwenye line zake. Nilimwamini, nikamsajilia line hiyo — na akaiweka pesa zaidi ya laki sita nk .Tsh 600,000.

Mpaka sasa line hiyo bado ipo kwenye simu yangu kwa sababu baada ya kutofautiana sikuweza kumpa. Sijaitumia hata shilingi, ila sasa najikuta nashindwa kuelewa kama niitumie, nimpatie au niifungie kwa usalama wangu wa kisheria na heshima yangu binafsi.

Leo amenitembelea nyumbani. Akiwa ananionyesha meseji kwenye simu yake, niliona jina la mwanaume mmoja kwenye inbox. Sikutilia maanani sana hadi aliponiomba simu yake, nikamkabidhi. Cha kushangaza, akaifuta haraka meseji ile ile niliyoiona.

Nilipomuuliza, mwanzo alikanusha. Baadaye akasema huyo jamaa ni mteja anayeleta pesa nyingi dukani kwao. Kwakua ananunua vitu vya paka hadi laki tatu 3 paka laki 4 Akasema jamaa huyo alikuwa anamfuata kimapenzi, lakini alikataa mara nyingi hadi akamkubalia ili amkamue hela— lakini anadai walikuwa hawapo kwenye mahusiano ya kweli

Nikaomba namba ya huyo mwanaume ili nijiridhishe lakini akakataa akisema ataniharibia biashara ya nyumbani kwao.

Kinachonisumbua zaidi ni kwamba:

✅ Mimi ndiye mwanaume wa kwanza kwake kimapenzi na kihisia.
✅ Nilimheshimu, nikampa nafasi ya maisha yenye heshima — hadi nikamfungulia line ya pesa kwa jina langu mwenyewe.
❌ Lakini sasa uaminifu umeanza kuwa na doa, na moyo wangu umechanganyikiwa.

Baada ya haya, alianza kupiga simu zaidi ya mara tano. Nilipopokea, akaanza kuniomba msamaha kwa uchungu. Anasema hajawahi kunichezea, ila alijikuta kwenye presha ya huyo mwanaume.

Lakini akili yangu inanieleza: msamaha wake ni wa kweli au ni wa kuokoa sura tu?
Na kuhusu hiyo line — je, nimuachie au nibaki nayo kwa usalama wangu?

Naomba mawazo ya wakuu — ya ukweli kabisa.
Nimejitahidi kuwa mkweli kwa upande wangu, bila kuongeza wala kupunguza.

Ahsanteni sana kwa ushauri wenu.
Naomba michango yenye tija na sio kubeza ilo tukio tu na solve vipi maana ana piga simu sikupokea baada ya apo anaomba msamah
Kama kila ukikumbuka alikaa hivi na ukaweza kupotezea , basi msamehe tu
IMG-20250604-WA0006.jpg
 
---

Kwa usalama wako, fanya haya mawili
1. Rudisha pesa zake.
2. Futa usajiri wa hiyo namba. Kama anaihitaji, anaweza kuisajili upya kwa jina lake mwenyewe.
Pesa yake nitairudisha .
 
Mrudishie pesa yake, suala la kumrudia ama la utaangalia moyo wako kama unamudu vishindo vyake.
 
Sijamjibu hadi sasa – moyo una maumivu mengi kuliko maneno.
Je, naendelea naye kwa masharti gani?
Au ndiyo mwisho wake kwa heshima?
Maana anatuma sms nyingì akiomba turudiane kweli
Je, nipelekwe na moyo au akili?
Je, samahani linaondoa hila ya makusudi?
Je, ni sahihi kurudisha mtu kwa kulia badala ya kubadilika?
Wakuu nipo tayari kusoma mawazo kwa ukweli bila kupendelewa. Hii ni roho ya mwanaume aliyewekeza moyo na uaminifu halafu anaambiwa ‘nilikuwa namkamua hela.’

Naomba ushauri kwa busara flani hivi
 
Sijamjibu hadi sasa – moyo una maumivu mengi kuliko maneno.
Je, naendelea naye kwa masharti gani?
Au ndiyo mwisho wake kwa heshima?
Maana anatuma sms nyingì akiomba turudiane kweli

Je, samahani linaondoa hila ya makusudi?
Je, ni sahihi kurudisha mtu kwa kulia badala ya kubadilika?
Wakuu nipo tayari kusoma mawazo kwa ukweli bila kupendelewa. Hii ni roho ya mwanaume aliyewekeza moyo na uaminifu halafu anaambiwa ‘nilikuwa namkamua hela.’

Naomba ushauri kwa busara flani hivi
Unaweza dormant zone relationship!!?

Mwanamke Alisha ku cheat huwezi Tena kumrudisha kwenye upya wake!

Mwambie aendelee na huyo jamaa na wewe ucheki maisha mengine!!!

Mbona Mimi nili move on na Sina shobo nae Tena !!?we unashindwa Nini man!!?
 
Back
Top Bottom