Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa sawa kabisa!Mapenzi kazini ni sumu na haitakiwi imagine unaweza kuwa PS wa boss na mkawa katika malav davi inatokea wageni wa kike wakiingia unanuna Presha inapanda presha inashuka na kazi inakushinda
mahusiano hayo si mazuri hata kidogo ..mnakosa uhuru ,pia utendaji wa kazi unaweza kuwa sio mzuri ...kula nanasi kunahitaji nafasi
haswa!!!!!!!! afu tena kushinda na mtu all the time aaah, unakinai kabisaaa!!! siwezi hata kutumia neno 'hun nimekumis'... mda wote tuko pamoja!
Boring!! plus hayo nlo yakoti hapo ya FL!!
Jamani ukitaka kujua ubaya wa mapenzi, anzisha mahusiano ofisini maana ni sawa na kujifunga bomu kichwani ukisubiri likulipukie wakati wowote!
Mahusiano kazini yasipoathiri utendaji wako (kama vile kutoa upendeleo maalum kwa mpenzi, kutumia muda wa kazi kwa ajili ya mambo binafsi na mpenzi nk) na kukusababishia matatizo kazini, basi mahusiano yakivunjika pia ni balaa jingine, visa, visasi, chuki vinatawala na kufanya mazingira ya kazi kuwa magumu.
Tuchukue tahadhari...
Ni kweli,uzinzi(mapenzi) kazini ni sumu,lakini kusema kweli hii imewatokea wengi,si kwa kupenda bali inakuja km maleria....yaani siku hizi wadada wanamitego we acha tu.Ps mjanja akimtaka bosi wake,hachomoki kabisa,na anajua bosi akiingia king tu,ka ps ndo kameula.Ndo unamkuta Ps anamtukana mpaka msaidizi wa bosi wake.
Serikali imetoa mpaka waraka wa mavazi,lakini haufatwi kabisa,mavazi yanayovaliwa makazini ni chanzo pia cha uzinzi kazini.