Mapenzi kazini ni sawa na kujifunga bomu kichwani!

Mapenzi kazini ni sawa na kujifunga bomu kichwani!

Never ever attempt kuwa na mpenzi kazini (business, ofisini n.k)....... UTAJUTA KWA NINI ULIANZISHA MAHUSIANO HAYO.......
 

Attachments

Mapenzi kazini ni sumu na haitakiwi imagine unaweza kuwa PS wa boss na mkawa katika malav davi inatokea wageni wa kike wakiingia unanuna Presha inapanda presha inashuka na kazi inakushinda
mahusiano hayo si mazuri hata kidogo ..mnakosa uhuru ,pia utendaji wa kazi unaweza kuwa sio mzuri ...kula nanasi kunahitaji nafasi
Sawa sawa kabisa!
 
Kuwa na mpenzi kazini ni ukosefu wa maadili. Na, katika nchi nyingi, hilo kosa linatosha kabisa kukufukuzisha kazi (clinton na Lewinsky). Hapa kwetu Bongo hayo ni mengi sana, kazi haziendi, PS akitumwa na Maofisa wa chini haendi kisa Boss ni mpenzi wake na ole wako umfuatefuate, utapewa uahamisho kwenda lindi. Kazi kweli kweli
 
kweli kabisa mkuu, hivi vitu bwana ni hatari sana, sasa utakuta wengine hawafanyi kazi kisa bosi ni mpenzi wake, kuwajibika kunakuwa hakupo kabisa na si unajua tena human nature ni wavivu mpaka tudriiviwe if no force just to relax, na upande wapili tena mkigombana balaa kuna kufukuzwa kazi, kuonewa, kunyanyaswa. so bwana wakati mwingine tujizuie na mapenzi kazini.
 
Inawezekana takwimu zinaonyesha kuwa si jambo jema kuwa na mwenza kazinii, lakini kuna Wanaume ninaowajua ni viwembe na hawangaalii makunyanzi kwenye kazi
 
haswa!!!!!!!! afu tena kushinda na mtu all the time aaah, unakinai kabisaaa!!! siwezi hata kutumia neno 'hun nimekumis'... mda wote tuko pamoja!

Boring!! plus hayo nlo yakoti hapo ya FL!!

hahaha hapo utaanzia wapi kusema nimekumiss
 
Jamani ukitaka kujua ubaya wa mapenzi, anzisha mahusiano ofisini maana ni sawa na kujifunga bomu kichwani ukisubiri likulipukie wakati wowote!

Mahusiano kazini yasipoathiri utendaji wako (kama vile kutoa upendeleo maalum kwa mpenzi, kutumia muda wa kazi kwa ajili ya mambo binafsi na mpenzi nk) na kukusababishia matatizo kazini, basi mahusiano yakivunjika pia ni balaa jingine, visa, visasi, chuki vinatawala na kufanya mazingira ya kazi kuwa magumu.

Tuchukue tahadhari...

Ni kweli,uzinzi(mapenzi) kazini ni sumu,lakini kusema kweli hii imewatokea wengi,si kwa kupenda bali inakuja km maleria....yaani siku hizi wadada wanamitego we acha tu.Ps mjanja akimtaka bosi wake,hachomoki kabisa,na anajua bosi akiingia king tu,ka ps ndo kameula.Ndo unamkuta Ps anamtukana mpaka msaidizi wa bosi wake.

Serikali imetoa mpaka waraka wa mavazi,lakini haufatwi kabisa,mavazi yanayovaliwa makazini ni chanzo pia cha uzinzi kazini.
 
Ni kweli,uzinzi(mapenzi) kazini ni sumu,lakini kusema kweli hii imewatokea wengi,si kwa kupenda bali inakuja km maleria....yaani siku hizi wadada wanamitego we acha tu.Ps mjanja akimtaka bosi wake,hachomoki kabisa,na anajua bosi akiingia king tu,ka ps ndo kameula.Ndo unamkuta Ps anamtukana mpaka msaidizi wa bosi wake.

Serikali imetoa mpaka waraka wa mavazi,lakini haufatwi kabisa,mavazi yanayovaliwa makazini ni chanzo pia cha uzinzi kazini.

Mmh mavazi gani hayo yanavaliwa ofisi za serikali yanayosababisha tamaa za ngono? Ni kama yale yanayovaliwa wakati wa majira ya joto nchi za magharibi nini? watanzania waishio DC wanayaita mavazi ya "majungu!" sidhani kama kwa utamaduni wetu mtu anaweza kwenda na kivazi cha majungu ofisini...
 
ni sawa lakini kama ndo mbuyu wako ufanyeje,mana mapenzi hayaangalii.ila kama ni mtu ambaye unamtamani tu utimize haja zako mi nasema utajiaribia kazi.na mkuu pale juu atakua yuko sawa
 
Back
Top Bottom