SoC02 Mapenzi ndoa mpaka kifo

SoC02 Mapenzi ndoa mpaka kifo

Stories of Change - 2022 Competition

Lilly max

New Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
1
Reaction score
0
Idadi ya vifo, majeruhi na athari hasi mbalimbali zitokanazo na mahusiano mapenzi na ndoa imekuwa ikiongezeka siku hadi siku. Vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti idadi kubwa ya athari hasi zitokanazo na mapenzi ndoa pamoja na mahusiano. Utasikia huyu kamuua mkewe kisa wivu wa wapenzi, au huyu kamjeruhi mchumba kisa wivu wa mapenzi. Miezi kadhaa iliyopita taarifa za binti wa miaka 27 aliyeuwawa na mume wake kwa risasi huko jijini mwanza zilienea kila kona ya nchi na baadae mume wake huyo kujiua kwa risasi.

Pia habari za dada kumchoma kwa moto mchumba wake kisa wivu wa mapenzi jijini dar es salaam maeneo ya mbezi. Huko Arusha pia yupo mwanaume mmoja aliyejinyonga kisa ugomvi kati yake mkewe. Hivi majuzi taarifa za binti Winfrida Michael wa chuo kikuu Mt John huko dodoma wa miaka 24 aliyekatishwa ndoto zake za maisha kwa kuchomwa kisu na mpenzi wake Julius Gervas kisa wivu wa mapenzi.

Mwanamke mmoja aitwae Magdalena Exaud huko singida amesimulia ukatili aliokuwa akifanyiwana mume wake na kupelekea kuoza mkono kutokana na kung`watwa na mume wake huyo. Magdalena anasimulia anasema alikuwa akipigwa na mume wake huyo mpaka anapoteza fahamu pamoja na ukatili mwingine mwingi, pamoja na kuwapa chakula chenye sumu watoto wao hali iliyopelekea kupoteza maisha ya mwanae mmoja.

Rehema Robert mwanasaikolojia wa mahusiano na ndoa anaelezea kuwa ongezeko nkiubwa la vifo mauaji na athari hasi katika mahusiano na ndoa yanachangiwa na sababu kadha wa kadha iikiwemo kuingia kwenye mahusiano kwa sababau ya kitu fulani, upendo kuisha, msongo wa mawazo uliopitiliza ,visasi na kupoza hasira, madhara yatokanayo na malezi, ugumu wa maisha, mitandao ya kijamii na stadi za maisha. Mwanasaikolojia huyu Rehema Robert anaendelea na kusema kuwa malezi ya watoto yana athari kubwa sana katika maisha ya baadae ya mtoto huyo yaani utu uzima wake.


Mwanasaikolojia Fred Sigmond alitoa nadharia yake akisema mtoto au mtu mzima anaposhuhudia tukio au kitu fulani ile kumbukumbu huhufadhiwa katika eneo la kuhifadhia kumbukumbu kwa maisha yake yote.hii hupelekea ukatili huu katika mahusiano na ndoa kutofikia kikomo kwani mtoto akiona mama au baba akifanyiwa ukatili na yeye atakuja kufanya kwa mke au mumewe akiona ni sawa kutokana na malezi aliyoyaona.

Wanafilosofia Carl Marx na Abraham Master wanaelezea nadharia ya kibinadamu (human perspectives) isemayo kuwa, ‘’Tabia ya mtu inategemea mazingira anayokaa mtu na watu anaoishi nao’’ na kwamba mwalimu wa kwanza wa mtoto au jamii ni mazingira anayoishi pamoja na watu anaohusiana nao.

Mfano mzuri ni uhalisia nilioupitia mimi mwenyewe enzi za utoto wangu. Baada ya mama yetu kufariki nilikwenda kuishi na dada yangu mkubwa. Dada alikuwa ameolewa na mume wake alikuwa akimfanyia ukatili mara kwa mara. Mara kadhaa alikuwa akimpiga vipigo vikali hali ilitopelekea kupata ulemavu wa kusikia. Siku moja usiku nilimshuhudia shemeji yangu akimkata dada na kisu akitaka kuutenganisha mkono wake na mwili. Tukio hilo liliacha picha kwenye akili yangu, hali ambayo imepelekea kuwa muoga kupitiliza na kuwa mtu wa kujihami kila wakati.

Hisia hizi zimenifanya kutokuwa na imani na wanaume na kuona wanaume wote ni wakatili.

INAUMIZA SANA

Suluhisho
Suluhisho la ukatili wote huu unaoendelea kwenye mahusiano na ndoa nyingi hapa nchini umeleta athari kubwa sana kwenye jamii ikiwemo kuvunjika kwa ndoa nyingi sana kwani kwa mujibu wa shirika la usajili wa vizazi talaka na vifo limebaini kuwa Zaidi ya ndoa mia tatu huvunjika kila mwez kwa jiji la dar es saalam pekee, Ukatili huu pia hupelekea ongezeko kubwa la watoto wa mtaani na tatizo la akili au ugonjwa akili.

Ni nini suluhu la haya yote yanayoendelea kwenye jamii kuhusu ukatili katika mahusiano au ndoa. Kwanza kabisa jamii inapaswa kurudi katika Imani na kuwa na hofu ya mungu kwenye kila jambo ambalo tunalifanya hii itapunguza ukatili na mauaji mengi katika mahusiano na ndoa, Viongozi wa dini pia wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo hivi ambavyo vimekithiri katika jamii katika siku hizi za karibuni.

Pili malezi ya watoto wetu yanapaswa kuangaliwa kwa umakini kwani watoto wanajifunza kutoka kwa wazazi wao hivyo yafaa kutengeneza kizazi nkilicho bora kitakachokua taifa bora la baadae. Kama watoto wetu wataendelea kushuhudia ukatili huu ukiendele kwenye jamii basi tutakuwa tunazalisha vizazi na vizazi vinavyosujudu na kuuabudu ukatili katika mahusiano na ndoa.

Pia wanajamii yawapasa kukubali kuongea kuhusu matatizo yanayowasumbua hii itapunguza msongo wa mawazo na sonona ambazo zinawakabili, pia kuongea na wasaidizi wa saikolojia na magonjwa ya akili ili kupatiwa njia au tiba za kuondokana na sonona na matatizo ya akili. Tiba ya saikolojia na akili ni tiba kama tiba za magonjwa mengine na inatibiwa kama magonjwa mengine, Hivyo jamii yapaswa kuwa na tamaduni za kpima afya ya akili kila baada ya muda fulani.
Mwishoni kabisa jamii yafaa ijue mapenzi ni furaha Amani na upendo na sio vurugu, vifo majeraha ama ukatili. Kama unampenda utamlinda
 
Upvote 0
Back
Top Bottom