Sasa we unadhani kwann wanaume wanalalamika hapa?!
Hebu tumia hata figo kufikiria. Hapa tunaongelea swala la kuoneana huruma na sio nani atoe..... Hata kama vitabu vya MUNGU vimeandika kuwa mwanaume atakuwa provider kwa mwanamke maishani mwake ila kuna dosari za kimaisha huwa zinatokea na ndipo hapo hekima na busara hutumika.
Wewe binti unakipato unaishi na mwanaume ambaye unampenda na yeye anakupenda ila ndio hali si nzuri kwake. Ajira ngumu, amekwama, kidogo alichopata kianaishia kwenye bili ya kumeme, maji, chakula na nauli anazotumia kwenye mihangaiko, akipata kidogo anakununulia hata vocha ndipo uwezo wake unaishia hapo.
Wewe una uwezo wa kulipa kodi ya nyumba, una uwezo wa kusapoti gharama zingine na akiba ipo, unakwama wapi kumsaidia mwenzako?!
Hapo ndipo tunapaongelea.... Kwamba unasema upo katika mapenzi, unajiita mwanamke wa fulani halafu akikwama wewe haupo serious nae unaishia kusema kauli za kimbea kuwa mwanaume atatafuta kwa jasho kwan yeye kakwambia hatafuti, kwan kukosa ni dhambi kusema wewe umuone yeye hayupo serious na maisha....?!