Mapenzi ni 2 way traffic, stop being bitter

Mapenzi ni 2 way traffic, stop being bitter

Kwa kweli mimi kuliko kuwa kwenye mahusiano kama hayo ni bora nibaki single hadi nakufa! African men demand a lot from their women more than they can give!
Unajiharibu ujue.....?!

No body will fix you.... Fix yourself before its too late......


We unasusa mapenzi..... Mapenzi ni chakula cha moyo na akili, ukisusa utaumia wewe mpenzi....... Imagine unasusa wenzako unaona wanaolewa wanakwenda kuanza maisha ya ndoa wewe unabakia kulalamika na kuongea kauli za hasira..... Pole sana.
 
Kwel ule msemo kwamba ikiwa mshahara wako ni 100K na mkeo nae ni 100k nyumban jumla mna 100k alikuwa anaongelea wanawake wa hivi
Mwanamke akiwa na laki mbili na mimi laki tano, hapo ndani tuna laki saba ukijumlisha na ile laki mbili nitakopa kwa mshikaji wangu...

Kimsingi ni kulishana matango pori maisha hatlyataki fujo....
 
Ndipo zilipoishia kuwaza! But on a serious note tafuta hela mtu wangu yaani mimegundua wewe ni kati ya wanaume ambao huwa wanapigia sana chapuo habari za mwanaume na mwanamke kuhudumiana kiuchumi!

Tofauti tu ni kwamba wanaume wenzio wengi huwa wanapigia chapuo kuhudumiana katika nyanja zote na siyo kiuchumi tu ila wewe unataka mhudumiane kiuchumi tu kwingine kote mwanamke apambane na hali yake! Tena huwa unajifanya kuuchukia na kuupinga vikali huu mfumo wa 50/50 ila eti kwenye pesa unataka mwanamke naye awajibike kutoa pesa sawa na mwanaume duuh!
Punguza jazba hii mada ni laini inatakiwa kujadiliwa kwa utulivu....
 
Sasa hapo utakuwa unaenda kinyume na huo msemo wako wa mapenzi ni two way traffic! Kwa sababu wanaume wengi wa kiafrika huwa mnataka wanawake ndiyo wajitoe zaidi kwenye mahusiano kwa kisingizio cha mapenzi ilihali ninyi hamuwezi kufanya hivyo!

Hata mimi naweza kukuambia tu kirahisi "it's so easy if you really love a woman" hata kama mwanamke wako ni pasua kichwa! Sidhani kama utakubali yaani ninyi wanaume wa kiafrika hamuwezi kuwafanyia wanawake zenu yale ambayo mngetaka wao wawafanyie!
Mahitaji yanatofauti ila both wanaume kwa wanawake wanajitoa sana.... Kuwa mpole.... Maisha hayataki fujo
 
Nitafute hela mara ngapi mrembo?
Nitafute hela mara ngapi mrembo maana basically nina kila kitu ambacho kijana wa kileo anapaswa kuwa nacho. Everything that you wish your man could have!

Ishu ni itikadi tu sababu huwezi lazimisha niishi katika itikadi ambazo zinaku favor wewe eti sababu wanaume wengine wapo hivyo siishi ili kuimpress watu, atleast that makes me a bit different.

Pia, siabudu hio dini ya lazima kumpa mwanamke kila kitu just to feed my ego but niko katika imani ya mwanamke kujitegemea ili kuleta balance katika maisha yetu. Thats why utaona niko Contrary na wanawake wengi wenye kimelea cha uvivu wa fikra.

Wanawake ambao wanadhani kuwa mahusiano ni bed of roses ama sehemu ya kupumzikiana. Mie sina huo ujinga.
Preach on brother
 
Duniani hapa vitu vyote vinaendeshwa au vinajiendesha kulingana na kanuni za asili...

Kuna kanuni kadha wa kadha lakini nitaziainisha mbili tu kulingana na muktadha wa mada yako...

Moja, mwanamke anapaswa kuwa chini ya himaya ya mwanaume (wabeijing msicomment)...

Sasa kila kilicho chini ya himaya ya mtu yoyote, mwenye wajibu wa kukitunza kitu hicho ni mwenye himaya...

Hivyo ndio maana mwanaume amekuwa akiwajibika kumtunza mwanamke...

Mbili, mwanamke hapaswi kufanya kazi ama shughuli yenye kutumia nguvu, maarifa yake kwa nia ya kuingiza kipato binafsi...

Kutokana na kanuni namba moja, mwanamke anapaswa kuwa ni msaidizi wa mwanaume ili kuhakikisha mwanaume hachoki, fadhaika, pata wakati mgumu katika kutaabika kwake kutafutia familia yake kipato...(unaweza mithalinisha na mahusiano yaliyopo baina ya mtambo unotembea kufua nishati "car engine" na kilainisha mtambo "oil")

NB: Kanuni hizi zinawahusu mwanaume na mwanamke walio wenza katika unganiko linalotambulikana.
Daaaah. We jamaa upo? Long time
 
Sasa wewe si ndie unayumba mama. Ishu ilioko mezani huijibu unazalisha maswali yasio na mpango. Kuna mwenzio aliomba aeleweshwe straight akawa na jibu. We unaranda randa!

Can you stand for your man financially without feeling bad about it?
Atakubadilishia swali ngoja aje
 
Mwanamme lazma atoe kwa mke but also mke lazma atoe kwa mume at times! Hii vita huwa kubwa sana kwa wanawake wanaojihesabia haki kama vilema katika mahusiano.

Hizo zama zilishapita, kidume unafanya kazi unaingiza hela mke anakupiga spoku miaka nenda rudi, siku kazi ikiisha all you got for us ni masimango tu kama vile hatukufanya kitu katika maisha yenu.

Mie niko against hili, na ndio msingi wa ku stick katika itikadi yangu. Mwanamke awe na self-reliance but pia with giving spirit. Sio mwanamke mchoyo na mbinafsi tu haya ndio huwa manyanyasaji.
Wengi wa namna hiyo ya wenye ulemavu wa akili ya ndoa huwa wanatoka familia masikini anakuja kwa malengo ya kuchuma tu na kuondoka......
 
Hii mada imekuwa na ubishi mkali sana ambao hauna muafaka. League ndefu sana hii inaweza gonga miaka miwili
 
Wengi wa namna hiyo ya wenye ulemavu wa akili ya ndoa huwa wanatoka familia masikini anakuja kwa malengo ya kuchuma tu na kuondoka......
Hio tabia lazima ibadilike na kama haitoshi basi kila mtu a exercise uhuru wa kuchagua. I'll stick to my philosophy!

Anaeona hawezi kujitoa basi aende kwa Mo au Bhakressa akachume tu.
 
Ww naona hujaelewa mada ipoje,na kama umeelewa basi ni mmoja ya wanawake waliotajwa kwenye hiyo mada maana kinachozungumzwa ni tofauti kabisa na unachokiongelea ww.
Huyu binti kaamua tu kuja kuvuruga kikao....
 
Karma amepumzika tu sio kwamba kaacha, ipo siku atajikuta tu kadumbukia katika uhusiano [emoji28][emoji28][emoji28]
Wa sampuli hii ndio huwa wanakuja kukutana na wanaume vilaza huko mbeleni.

Sasa wewe unakuta kabinti hakajafika hata 20 Kameanza kusema wanaume ni mbwa, hivi wanaume amewajulia wapi, anatembea na wavulana badala ya kusoma anasema wanaume mbwa.
 
Kwa kweli mimi kuliko kuwa kwenye mahusiano kama hayo ni bora nibaki single hadi nakufa! African men demand a lot from their women more than they can give!
Hebu tupatie mifano hai ya demand za wanaume ambazo wewe zinakuchosha na kukufanya uone wanaume wanademand a lot from women?!
 
Hio uomba omba haipendezi na wala haikubaliki. Ila kuna ile una hustle unaona kabisa leo bila bila.

Tajiri hajatoa hela kwa wakati uko pending unahitaji material kukamilisha kazi nyingine. Unavuta waya! Mama hembu naomba nsaidie laki 7 nikamilishe kazi nina kipengele kidogo ntakurudishia nikishakabidhi kazi. Dakika 10 tri..trii sms ya MPesa imeingia.

Sasa kwa demu mwenye roho ya kimaskini atakuwa anaona kama miujiza maana akiombwa hata elfu 50 anahisi akaunti yake inawaka moto. Ila hapo kama mke unakuta na kazi ulimfaitia wewe akapata.
Ha ha ha
 
Mwanamke akiwa na laki mbili na mimi laki tano, hapo ndani tuna laki saba ukijumlisha na ile laki mbili nitakopa kwa mshikaji wangu...

Kimsingi ni kulishana matango pori maisha hatlyataki fujo....
huna chako pale....
 
Back
Top Bottom