Mapenzi ni kazi kama kazi zingine

Mapenzi ni kazi kama kazi zingine

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Kazi yoyote lazima ifanywe kwa ufanisi ili ilete matokeo mazuri,na iwe endelevu ili iweze kuleta tija kwa wafanyakazi,,,hivi umeshawi kumsikia mtu amechoka kufanya kazi ikiwa hiyo kazi ndiyo inayo muweka mjini?

Kama hivyo ndivyo basi tambua mapenzi nayo ni kazi kama kazi nyingine yoyote ile,,wapendanao hawana budi kupambana kuhakikisha mapenzi na upendo unaendelea kuwepo kati yao.

Kila mmoja miongoni mwenu atambue ana wajibu mkubwa sana wa kuhakikisha mnaendelea kupendana na kuheshimiana kwa gharama yoyote ile ikiwemo kutoa muda wake,hisia zake, uaminifu wake na tabia njema iliyotukuka ili ilete faraja na amani katika nyumba yenu.

Tunachofeli wengi wetu tunayafanya haya wakati tunapoanza mahusiano lkn baada ya kuwa pamoja na kuzoeana huwa tunaona hatuna tena wajibu wa kujitoa kuonyesha upendo kwa mwenza wako

Hakuna tena maneno matamu na yenye kufurahisha masikioni mwetu,,hakuna maneno matamu yenye kugusa nyoyo zetu na hisia zetu,,,yaani kuambiwa unapendwa ni mara chache mno,,tena afadhali sisi wanaume walau mara moja moja tunaweza kuwaambia wenza wetu kuwa tunawapenda

Lakini madam zetu watakwambia wanakupenda ikiwa wanataka kitu toka kwa mwenza wake ndio utasikia anakwambia maneno mazuri lkn yakifuatiwa na shida yake,,,na kibaya zaidi wanaume tunalijua hilo,,,so maneno yako mazuri hayana athari yoyote katika nafsi ya mwanaume kwakuwa umeyasema kwa sababu unataka kitu fulani.

Lau ukimwambia maneno hayo mwenza wako kwa wakati sahihi,trust me yatamuathiri na kumfanya awe na furaha sana,,,lakini wengi wenu mnafeli,,ebu badilikeni basi

Mwanaume pia anahitaji kuambiwa anapendwa,mwambie ni kiasi gani yuko special kwako,,mwambie hutaki kummiss hata siku moja katika maisha yako,,halafu utaona jinsi atakavyo kujali na kukuthamini.

Bahati mbaya kazi hiyo mnawaachia michepo nao kwakujuwa madhaifu yenu basi huifanya kazi hiyo vizuri sana na kukamata nyoyo za wenza wenu

Guys hivi yale mambo ambayo huwa tunayafanya tunapoanza kuwinda windo jipya huwa tunayaacha wapi? Kwanini mambo yale tusiyaendeleze ili kuwafanya wenza wetu wawe na furaha na wazidi kutupenda wakati wote.

Ninachotaka kusema hapa,,kila mtu anawajibu mkubwa sana kuhakikisha mapenzi na upendo kati yenu yanafanyiwa kazi ili kuleta matokeo chanya kabisa,,sio jambo la wanaume kuwapenda wanawake na kuwaonyesha mahaba bali ni jambo la wanawake pia kuwainyesha upendo na mahaba wanaume wao.

Ewe madam mara ya mwisho lini kumnunulia mwenza wako zawadi? Kuna raha yake ya kununuliwa zawadi na madam wako,,,wifi yenu mashallah huninunulia vizawadi kama nguo,saa basi nikivaa huwa nakumbuka hivi vimetoka kwa kpnz changu na inatia raha kwakeli

Mnunulie mwenza wako vijizawadi tena wakati mwingine mnunulie kwa hela hiyo hiyo anayokupa wewe,,kwake yeye hizo ni zawadi na atadhithamini sana,,unajua kile kitendo cha kwenda kununua zawadi kinaonyesha unajali na umemfikiria na kuona umuhimu wake kwako

Sitokuja kusahau kipindi fulani nilinunuliwa zawadi ya kadi ambayo ni kubwa kama zile kadi za x-ray tena nahisi inazipita ,ilikuwa kipindi cha valentine day enzi hizo,,, my ex girlfriend SIA i won't forget that gift,,,it was amazing

Kwanini nimefungua hii code? Ni kuonyesha nguvu ya zawadi katika mapenzi,,,saa nyingine nunua hata pipi,chocolate, na vitu vingine vidogo vidogo trust me vinatupa athari kubwa katika nyoyo zetu,,hii ni kote kote kwa wanaume na wanawake

Isionekane kupenda ni tendo la jinsia fulani laa,,bali kupenda ni wajibu wa jinsia zote na tunawajibika kwa hilo.

Tuache ule ujinga wa kusema "nimetendwa sana kwahiyo siwezi penda tena mwanaume" mwanaume naye anasema hivyo hivyo,,,matokeo yake wote tunaishi katika mapenzi kwa hofu ya kutendwa na kutupelekea wote kutooneshana mapenzi

Kutendwa kwako huko ulikotoka sio tatizo langu ni wewe na huyo ex wako halinihusu the same to me,kama nilitendwa sio tatizo lako it's my problem,,sasa kwanini shida zangu zikuathiri wewe? Au za kwako ziniathiri mimi?

Kama tunaingia katika ulimwengu wa mapenzi we must grow up,tuachane na utoto,,mapenzi ni kazi hivyo tunahitaji kujifunza jinsi ya kupenda,kujali na kuheshimiana

Hakikisha kabla hujaingi katika mapenzi mengine au na mtu mwingine,malizana na hisia zako za past relatonship,maliza machungu yako,,kisha anza upya kama hujawahi kupenda kabla,,,maumivu yako ya zamani usimbambikie mwengine,hausiki nayo.

Tambua wakati mwingine tunakutana na machungu na kuumizwa ili tuwe bora zaidi kwa ajili ya mahusiano mapya ambayo yatabadilisha maisha yetu.

Mapenzi yenye furaha na upendo ni kwa ajili ya watu wanaojitambua.


Ni hayo tu!
 
Anhaa nitajaribu io kazi,,kama ina mshahara mzuri lakini
 
Back
Top Bottom