Mapenzi nimeyanyooshea mikono

Mapenzi nimeyanyooshea mikono

INRI

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2017
Posts
1,324
Reaction score
2,319
Habari wana MMU.

Naomba nisimulie yaliyonipata siku ya jana Jumapili.

Nina mpenzi wangu tumekuwa kwenye mahusiano hata miezi minne haijafika. Kiukweli nilipenda haswa mpaka muda huu, naye nafahamu alinipenda sijajua baada ya hili tukio la jana.

Tukio lenyewe ni baada ya kuchukua simu yangu na kuperuzi baadhi ya apps. Sikupanick nikamuachia. Baada ya kumaliza, si nikashika ya kwake bhana wee, hapo ndio vagu lilipoanzia. Kawa mkali sikujali nikasoma normal texts, kuna mtu anapenda kuchat nae, nikaona jina lake.

Muda si mrefu akawa kanipora simu, nikaomba niangalie sms, akanionesha ila roho haikukubali nikajua tu kuna chats huwa anafuta. Bhasi na mimi nikapata hasira sana, kuona kwanini anakuwa mkali kushika simu yake. Mida ya jioni nikamjibu kwa hali ya kuonesha nimechoka. Nikatimuka zangu home.

Akaniandikia ujumbe wa jinsi ninavyotaka mtu perfect wakati ni ngumu. Akanitakia kila la kheri kwasababu nilimjibu kifupi. Sasa tangu natembea, nipo kwenye usafiri kurudi home, namuwaza yeye tu afu roho inauma nikikumbuka moments zetu. Yaani niliishiwa nguvu.

Nikapita duka la madawa nikanunua Valiums kwaajili ya kupata usingizi. Ndio nikalala. Nimeamka asubuhi nikiangalia juu chini ni yeye tu. Dah!

Uvumilivu umenishinda, yanini kuteseka hivi, nimemcheki muda si mrefu kwamba nilikosea nasubiria anijibu.

Kweli ukiona watu wanakunywa sumu, kujinyonga na kutoa uhai usishangae.

Mapenzi yana-run Dunia.

My take: Mliopo kwenye mahusiano, mjifunze kusikilizana na ku-reach resolutions kuliko kujiona wewe ndio upo sahihi.

Good Monday.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza pole. Hayo hutokea kwenye mapenzi ya kisasa.
Inaonesha umri wako bhado ni mdogo kiasi hicho kitu kidogo hivyo kikufanye umuache mtu wako. Umekurupuka. Japo kweli una mapenzi nae.

Ipo hivi, kama kweli mtu wako anakupenda kwa dhati atatafuta muda akujibu ( positive response) na ikiwezekana muonane kuzungumza upya hivyo Kurudi tena kwenye mahusiano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa dogo unataka kutufundisha sisi watu wazima? umelikoroga pambana na hali yako. Halafu nyie watoto wa sekondari siku hizi mmekuja na mitopiki ya kimama sana. Nataka kuacha kuingia JF mpaka shule zifunguliwe ndio narudi
 
Ha ha ha ha dawa haijakoea vzur Mkuu naona maana umeomba na msamaha juu ilhali ukijua kwamba yeye ndio kakosea aiseee.....................
Kama unajua wewe ni mdhaifu na jeuri ya kumuacha huna kaa mbali na simu ya mwenza wako utakipa presha unnecessary.
Nina miaka zaid ya mitano sasa sjawah kufanya huu mchezo wa kupekua simu na wala sina huo mpango
 
Sasa dogo unataka kutufundisha sisi watu wazima? umelikoroga pambana na hali yako. Halafu nyie watoto wa sekondari siku hizi mmekuja na mitopiki ya kimama sana. Nataka kuacha kuingia JF mpaka shule zifunguliwe ndio narudi
Mapenzi ni utoto wakati mwingine.

Hii kitu haina umri, rangi, dini, kabila, hadhi yako nk..

Mapovu hayajengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpenzi tu wa kawaida hali ni hiyo angekua ni mkeo wa ndoa s ndio ungekua ushakufa wewe??

Kama hukua na ujeuri wa kumuacha simu yake unapekua unataftanini?? Hujui ukitafta lisilokuhusu utakutana na litakalo kukera? Kibaya zaid kishajua hufui dafu kwake subiria hizo drama zake.

Pole.
 
Kwanza pole. Hayo hutokea kwenye mapenzi ya kisasa.
Inaonesha umri wako bhado ni mdogo kiasi hicho kitu kidogo hivyo kikufanye umuache mtu wako. Umekurupuka. Japo kweli una mapenzi nae.

Ipo hivi, kama kweli mtu wako anakupenda kwa dhati atatafuta muda akujibu ( positive response) na ikiwezekana muonane kuzungumza upya hivyo Kurudi tena kwenye mahusiano.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimejifunza kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndani ya miezi minne umependa mpaka umevuka mipaka, unaonaje ukaungana na muheshimiwa msukuma kwa kujitangaza rasmi una PHD ya kupenda
 
ndani ya miezi minne umependa mpaka umevuka mipaka, unaonaje ukaungana na muheshimiwa msukuma kwa kujitangaza rasmi una PHD ya kupenda
Love doesn't ask why, when, how, which, what person you love.

Nafikiri wengi mnadhani kupendana ni muishi miaka mingi.

Kuna kitu kinaitwa pia Love at first sight.

This shits happen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom