USIOGOPE KUOA MCHAGGA
Nimeona wanaume wengi mmeingiwa na hofu juu ya ndoa.
Watu wanasema "Usioe wa kabila fulani, WACHAGGA ni wauaji wa waume zao wakifanikiwa" na maneno mengine mengi. Maneno haya yamevunja ndoa nyingi kabla hata hazijaanza.
Nimekuandalia ujumbe huu ukutie moyo:
MSIKILIZE MUNGU, USISIKILIZE KELELE ZA WATU
Ndugu yangu,
Ndoa si kabila. Ndoa ni agano mbele za Mungu.
Ukioa kwa kusikiliza maneno ya watu, utaishi kwa hofu ya watu. Ukioa kwa kumsikiliza Mungu, utaishi kwa amani ya Mungu.
1. Kabila halimfanyi mtu kuwa mke mwema au mbaya.
Uovu na wema havina kabila. Mchagga mwema yupo, na wa kabila lingine mwovu yupo. Kila kabila lina malaika wake na lina wabaya wake. Usihukumu bustani nzima kwa sababu ya ua moja lililokwisha nyauka.
2. Mwanamke sahihi hutoka kwa Bwana, si kwa ukoo.
Biblia inasema: "Mke mwema hutoka kwa Bwana" Mithali 19:14.
Mungu haangalii kama ni Mchagga, Mhaya, Msukuma au Mpare. Mungu anaangalia moyo. Mtu akiwa na Mungu, Mungu humchorea mtu sahihi. Hata awe wa wapi, Mungu akisema huyu ndiye, ndiye.
3. Hofu si kutoka kwa Mungu.
Mungu hajakupa roho ya woga. Hofu ya kuoa kwa sababu ya porojo za mitandaoni na vijiwe vya kahawa itakuzuia usimkose yule Mungu aliyekuandalia. Usikubali shetani akutishe na hadithi za kusadikika.
Badala ya kuuliza "Ni kabila gani?" Anza kuuliza:
- Je, huyu mwanamke anampenda Mungu kuliko anavyonipenda mimi?
- Je, ana heshima, bidii na hekima ya kujenga nyumba?
- Je, nikiwa chini, atanivumilia na kuniombea?
- Je, amani yangu inathibitisha ndani yangu huyu ndiye?
Mke sahihi si yule asiye na mapungufu, ni yule Mungu aliyemkusudia awe safari yako ya kwenda mbinguni.
Kwa hiyo ndugu yangu, inuka. Omba. Fungua macho ya rohoni. Usioe kabila, oa mtu. Oa tabia, oa maombi, oa maono.
Mungu akiwa ndiye kiongozi wako, hatakuletea mwuaji, atakuletea msaidizi. Hatakuletea adui wa mafanikio yako, atakuletea mlinzi wa mafanikio yako.
Acha kuogopa. Anza kuamiini.
Tukutanekwamwamposa
#Pdidy