Ha ha ha ..Nimekupata..Ok ni hivi.

Kama nilivyowahi kusema, mapenzi ni maisha na ukiangalia sana mapenzi ni myth na pia ukichimba deep sana unaweza ukachanyikiwa na kuwashawishika hakuna mapenzi ila sehemu kubwa ni sacrifice. Ok, leo tusifungue mjadala huo..

Mimi naamini mapenzi ya dhati ni mchanganyiko wa vitu vingi kama ilivyo pilau au biriani na huwezi kuchagua kuhisi ladha kiungo kimoja tu na kuacha kingine. Unatakiwa kukubali ladha ya pilau na siyo ladha ya wali, mdalasini etc. Ndani ya mapenzi ya kweli kuna kujitoa muhanga, kusameheana, uwazi, ukweli, uongo kidogo, mateso, furaha, busara, heshima, kuvumiliana, historia, bahati etc. Ni mseto wa pilau ambao wote mnatakiwa msifie ladha yake. Sasa kama wewe hupendi kiungo cha mdalasini, utasema pilau tamu lakini mdalasini imezidi kidogo ..hivyo mdalasini itapungua na siyo kutoa kwani ukitoa mdalasini hilo silo plau tena..

Pia kumbuka Historia ina sehemu yake katika maisha yetu ya sasa. Mfano, binafsi kila nikimwona mwanamke yeyote hata binti zangu nashindwa niwalipe nini.. Kumbuka nimepishana umri wa miaka 16 na mama yangu ambaye anaamini yule aliyempa ujauzito alimlaghai kwa maneno matamu labda pia na hela, kumwoa na kumtelekeza baada ya kumwongeza watoto wengine. Kuishi kwa kushuhudia jinsi yule mama alivyoangaika hadi kuishia kupoteza maisha yake kwa ajili yetu na at the expense ya yule jamaa aliyemlaghai kwa lugha ya mapenzi ni picha ambayo siwezi kusahau..Anyway, kwa sasa nimeshapewa jukumu la kuwa baba, Je? Nifanye nini kwa mke na watoto wakati najua fika kitakachowakuta na kidonda ambacho kinanisumbua hadi leo? Je? Nitamuhenzi vipi yule mama aliyejitoa muhanga ambapo mara nyingi nasema kwanini asingesubiri kidogo? Je niendelee kudanganya na kubadili wanawake ni sawa na yule aliyemdanganya mama yangu na kumtundika mimba akiwa na miaka 15?, Kufanya mapenzi na mabinti wakati najua mimi na mama tumepishana miaka 16? Je? Niwachukie wanaume kwa sababu ni wakatili, lakini mbona nami ni mwanaume, tena baba? Its complicated..

Solution, Just to be what you wanna be, Sacrifice life kama wengi walivyofanya, kuweka malengo ya chini kwani utakubali na kutatua matatizo mengi, kujishusha utaweza kumwona mwenzako na kuheshimu kama alivyo, kubalance na jamii kwani kama alivyosema Nyumba kubwa jamii siyo 1+2 = 3..ni akili kichwani..Lakini inawezekana pia ukajumlisha bahati..kwani ni bahati kupata mtu ambaye ataweza kuchukua na kuthamini mchango wako kwa familia na siyo kufikiri its your weakness na ku-take advantage..