Mapenzi ya kweli ni adimu kama dhahabu na wengi tunayagundua baada ya kuyapoteza

Mapenzi ya kweli ni adimu kama dhahabu na wengi tunayagundua baada ya kuyapoteza

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Frank ni mtoto wa mwalimu na baba yake alimkazia sana kwenye elimu yeye na ndugu zake. Kwa miaka yote wakiwa shule ya msingi baba yao hakuwahi kwenda kunywa bia bar, alirudi nyumbani na kuoga na kuanza kuwa mwalimu wa watoto wake.

Topic za hesabu Frank alifundishwa mwezi mmoja kabla ya wenzake darasani. Kwa mshahara wa mwalimu, nyumbani kwa kina Frank hakukua na mbwembwe nyingi zaidi ya mahitaji muhimu. Baba yao alipenda mpira hivyo walikua na king’amuzi na timu anazo support msure zikishinda watoto wali kunywa soda.

Frank na ndugu zake masomo ya darasani yalikua rahisi kwao kutokana na msaada wa msure wao na imani waliyofundidhwa ni kuwa elimu pekee ndiyo itawapa maisha wanayoyataka wao.

Darasani kwa Frank alikuwepo Lilian, mama yake Lilian alikua Mkuu wa Wilaya. Lilian alivaa mavazi nadhifu yaliyo trend kipindi hicho. Frank alimpenda sana Lilia na alimuumiza sana ndotoni. Alipeleka maombi yote lakini Lilian alimdharau sana Frank mvaa Safari Boot zilizochongwa kwa Mchaga.

Baada ya Frank kwenda Chuo Kikuu na kuhitimu kama mhandisi sasa Lilian anamtafuta Frank. Frank anasema nilimpenda wakati ule angekubali tusote pamoja mimi ningemuoa sasahivi Lilian anamkaribisha Frank nyumbani akale chakula pia awaone ndugu zake wote.

Lilian anampenda Frank Mhandisi si Frank mvaa safari boot.
 
Ukubwa Jalala.

Mwanamke Majukumu.

Mwanaume Hela, vingine tutavumilia.
 
What women want?

What men want?

Power, Respect & Fame.

Fill the blanks.
 
Sky najua Ni mtu mzima wewe hivi Mimi siwezi kuwa km Frank kwako
 
🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️
 
Tukubali tukatae, hakuna lolote zuri lisilotegemea pesa.

Ukiwa na pesa utapata mapenzi ya kweli (kujihisi unapendwa tu ni ukweli tosha), utakuwa na nyumba nzuri na utamiliki kila kizuri.

Hata uchungu wa tajiri na kapuku una utofauti wake. Usiombe uugue/uguliwe halafu huna kitu (mfano wa uchungu)

Bottom line, tusilaumu wale wanaofuata neema baada ya yote, hakuna faraja katika umaskini.
 
Back
Top Bottom