Mapenzi yalivyonibadilisha na kuwa mkatili na roho ya ajabu

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
7,683
Reaction score
15,128
Naam kama heading inavyosema kwakweli kwasasa nimeanza kujichukia hasa upande wa mahusiano ya kimapenzi. Nianze nyuma kidogo ili uelewe kwanini yamenifanya kua katili na pengine inaweza ikawa funzo kwa vijana wa leo. Hapa sitataja majina halisi ya wahusika na nitaeleza direct lengo tu.

"Wewe ni mtu usiyejali mkatili una roho mbaya sana nakuchukia huu ni moja ya ujumbe niliokutana nao leo asubuhi katika simu yangu kutoka kwa binti mmoja ,najua yupo humu atasoma aone kwanini nimekua hivi na wala sifanyi kusudi nimejikuta tu nimekua sina huruma tena na wanawake.

Nimepitia mahusiano mengi ila kuna mahusiano haya 5 ndo yameacha kumbukumbu mbaya sana za maisha yangu ,kiasi imebadilisha akili yangu na kwasasa naanza kuona sio sawa hata kidogo.

UHUSIANO WA KWANZA

Mwaka X Nikiwa nipo form 1 nilipata mpenzi wangu wa kwanza ambaye alikua amepanga kwetu. Mpenzi huyu ni mkuria wa huko mara alikua pisi kali na mpaka sasa ni miongoni mwa pisi kali ya kariba yake ambaye nimewahi kudate nae, kwasifa alikua mrefu wa wastani mweupe ,guu la bia ,shepu la maana kiasi alikua akiwatoa udenda pale mtaani. Binti huyu alikua mtoto wa kwanza katika familia ya Mzee Mazinde(code ila linafanana na hili) ambaye alijaaliwa kwa kipindi hiko kua na watoto wa 5 ambao wote ni mabinti.

Mzee huyu alikua anajiweza kifedha kiasi chake kwani alikuwa mfanya biashara huko mara ndipo akaamua kuhamishia makazi yeye na familia yake hapa Dar es salaam. Hapo ndipo alipokuja kupanga nyumbani kwetu huku akiweka mambo yake sawa ili ajenge mjengo wake na kuhamia.Kutokana na kua na watoto 5 akiwa pia na mfanyakazi wa ndani aliamua kuchukua vyumba vinne.

Tangu alipohamia pale binti yake mkubwa kwa jina la Deborah(code ila linafanana na hilo) aliwatoa sana udenda vijana wa mtaa ule. Bint huyu alikua na mikogo ulienda na uzuri na jambo la kupendeza alikua msafi sana na kuvaa mavazi yanayoendana na uzuri wake.

Alipata usumbufu sana hadi kwa kwa kaka zangu walimuinda sana bila mafanikio ndipo mpaka ikaja mimi nikahamia kwa mzee kutoka nilipokua nakaa kwa mama(mzee na mama wametengana). Kwa mara ya kwanza hisia za mapenzi zilianza baada ya kumuona Deborah ilifikia kiasi nilikua nisipomuona hata siku moja sina amani.

Basi kufupisha stori nikaanza harakati za kumtongoza mwishowe akakubali jambo ambalo hata mimi alinishangaza😁,nadhani kwakua nilikua nasoma Azania na yeye jitegemee na tulilingana vidato. Maisha ya mahusiano yakaanzia pale mabroo baada ya kuona hivyo wivu uliwajaa sana ila wakaachana na mchongo wa kumfukuzia tena. Mapenzi yetu yalikua ya wizi wizi sana kwasababu wote tulikua wanafunzi ,siku zilienda mpaka ikafika siku ya kula tunda kwa mara ya kwanza dah mpaka leo sijawahi sahau ile test aisee.

Kwakua yule bint alikua mzuri na mimi sina kitu na kuna watu walionizidi wanamfukuzia nilikua nina wivu sana kwake. Huyu bint yeye ndo alinipa zawadi kubwa nyingi kuliko mimi japo na mimi nilimpa sana zawadi ndogo ndogo.

TUKIO LA DEBORAH SASA.

Ikiwa imepita miezi 8 tangu uhusiane tarehe 25 December ya mwaka huo tulipanga baada ya chakula cha mchana cha X mass tutoke tukatembee. Basi bwana tuliletewa chakula na mama yake Deborah sasa bro alikuja na embe na kisu cha gheto alikua amechukua jamaa yake anaitwa Juma(code) ambaye alikua anakaa nyumba ya pili.

Hivyo aliniagiza nikachukue kisu ,nikiwa na spidi ya kuwahi ili nikale pilau nikawa nakimbia huku naita Kaka Juma Kaka Juma vuuu nikaingia ndani bila hodi DAH SIKUAMINI NILIPOMKUTA Deborah akiwa na juma wamekaa kitandani huku akiwa na chupi tu na juma akiwa na boksa na vest.Sikuweza kujua kama walikua wanaanza au wamemaliza niliduwaa na mate ya uchungu yakipita kooni.

Ngoja niwape wasifu wa Juma kidogo, huyu bwana yeye alikua anafanya kazi Halmashauri kwa hiyo alikua ana uwezo mzuri na alikua best yake mkubwa kaka yangu ninayemfuata.

Juma kwa hasira alifoka kwanini nimeingia bila hodi ,huku nikiwa bado nimeduwaa machozi yakinelenga bila ya kusema chochote nikataka kuondoka. Juma aliniambia subiri usiondoke akasimama akaja mpaka nilipo akarudishia mlango,akamuuliza Deborah leo lazima tukate mzizi wa fitna uniambie hapa hapa KATI YANGU MIMI NA FEYZAL NANI UNAMPENDA?.

Bila kufikiria mara mbili Deborah akasema anampenda Juma dah ule uchungu haukuelezeka,nikaamua kuondoka kwa uchungu sikusema chochote mpaka nafika kwa bro. Wakati naingia anafoka kwanini nimejichelewesha lakini ghafla aligundua nilikua nalia ndipo aliponiuliza mbona kama ulikua unalia? Ni kama alitonesha kidonda na kufugulia bomba la machozi nililia sana mfululizo kwa sauti na kwa uchungu sana hadi sasa bro anasemaga hakuwa kuniona nalia na kua na uchungu kama ile siku.

Huku kilio cha kwikwi nikilia nikamueleza bro ,Bro alipatwa na hasira sana pale pale akaondoka kwenda kwa Juma ulitokea ugomvi mkubwa sana kupelekea mpaka ishu ika link kwa wazazi wa Deborah na pale mtaani. Swala lile likafika mpaka kwa Baba kiasi cha kukasirika na kuamua kua niondoke pale nikaishi kwa mama na mimi baada ya tukio lile sikua tena na hamu hata ya kuishi pale hivyo nikaondoka.

Mawazo ,sonona na ukiwa vilinichukua kuanzia nyumbani hadi shuleni Mama mzazi alinisihi sana niachane na mapenzi nisome na ilinichukua muda mrefu sana mimi kuja kukaa sawa. Wakati napitia kipindi kigumu Juma alikimbia ule mtaa maana ilikua soo kutembea na mwanafunzi ila baadae alikuja pale kwa mama na kuniomba radhi yaliisha lakini Bro wangu hakutaka tena kua karibu nae.

Nikiri ilinichukua muda sana kukaa sawa kumbuka alikua mwanamke wangu wa kwanza kuvunja amri ya 6 na nilimpenda hasa na niliapa sitakuja tena kupenda na sitaki tena mapenzi.

Mambo mengi yalitokea baada ya hapo mimi na Deborah japo hatukuwahi kurudiana ila kuna mengi yalitukutanisha ambapo tukawa maadui wakubwa maana walikaa pale home kwa miaka 2 mbele kabla ya kuhama. Leo sitaandika hayo nitaishia hapa kwa huyu.

UHUSIANO WA PILI

Baada ya kuachana na Deborah nikiwa kidato cha pili na kurudi kwa mama,maisha yaliendelea mpaka kidato cha pili mwishoni nikiwa bado sina mpenzi mtaani pale akahamia bint mmoja akiwa anaishi na dada yake ambaye alikua askari wa barabarani. Bint huyu hakua mrembo alikua bint wa kawaida Muislam na kwa kabila alikua watu wa Mafia huko.

Huyu bint hakua na uzuri kihivyo ila alijaaliwa kalio na kiuno ,yaani kwa kipindi kile pale mtaani hakuna bint aliyefua dafu kwa upande huo. Huyu tumuite KAUTHARI basi bwana nikaanza harakati nikiwa na washikaji zangu wote tunafukuzia huyo manzi.

Binti alikuja kipindi ndo ametoka form 1 anataka kuingia form 2 na mimi natoka form 2 naenda form 3 hivyo kwasababu nilikua na uwezo ikabidi nimsogeze kwa triki ya kumfundisha MATH. Maisha yalienda nikawa natupia ndoano mdogo akachomoa kiasi hadi uhusiano wetu wa kimasomo ukafa, akatokea kunichukia ajabu hadi akiniona anatema mate duh basi nikapiga chini.

Siku moja nikiwa nimekaa mwenyewe kijiweni alimtuma mtoto aniletee kikaratasi kilisema hivi " SHEMEJI NA DADA LEO SAA 1 USIKU WANAENDA KWENYE HARUSI ,TUKUTANE PALE MWEMBENI SAA 3 BY KAU". Tabasam likachanua muda ule ule niliondoka kwenda home kuoga maana ilikua saa 11 jioni, piga mswaki nikajitayarisha kabisa nikiona masaa hayaendi. Saa 2 usiku juu ya alama nikawa nimefika eneo la tukio tena nilifanya siri sikumwambia mtu yeyote yule, nikiwa namsubiri akaja yule mtoto tena akaniambia dada yupo kule kaniambia nikufuate nami kwa shauku nikaelekea nikimfuata mtoto yule.

Kweli nilimkuta ananisubiri akanisalimia kisha akamwambia dogo aende nyumbani, akaniambia "FEYZAL TAFUTA SEHEMU YOYOTE TUKAONGEE NINAO MUDA HADI SAA 5 USIKU". Bila ajizi nikafikiria nikaona huyu nimpeleke kwa mwanangu ISIHAKA ,nikamuomba anisubiri kwa spidi ya juu nikakimbia mpaka kwa jamaa nikampa mkanda na jamaa kwasababu alikua mwanangu sana akaniruhusu. ISIHAKA huyu alikua mkubwa kwangu kwa zaidi ya miaka 4 ila alikua ananielewa sana so haikua ngumu kukubali. Nikarejea kwa KAUTHARI hao mpaka gheto ,ndipo aliponieleza amekubali ombi langu lakini nisimuumize kwani yeye ni bikra na hajawahi kua na mwanaume yeyote.

Nilifurahi mno basi stori zikazidi nikajikuta naomba gemu siku hiyo hiyo na kweli dogo alikua bikra ,nilipata ugumu mkubwa sana japo nilifanikiwa kwa nguvu kiasi baada ya hapo alikua analia kwanini nimemlazimisha,basi nikambembeleza sana akaelewa kutahamaki saa 7 usiku hii hapa haraka sana nikampeleka kwao kwa bahati dada yake hakua amerudi. Mapenzi moto moto yaliendelea huku tukivunja amri ya 6 mara kadhaa hatimae ikafika likizo akaniaga anaenda kwao Mafia hapo ikawa mara ya kwanza kutengana nae. Alipokua mafia tuliwasiliana kwa wizi wizi maana hakua na simu mpaka aliporudi lakini niligundua mabadiliko makubwa sana japo alikua akikataa.

Binti kwanza aliongezeka na pia hakua ana jali kama mwanzo baadae zikaanza rumanzi mtaani kua anatoka na jamaa mwingine mara yule,nikawa nafuatilia nakuuliza bint anakataa. Spidi ya kupewa tunda ikawa kwa nadra sana japo alibanwa ila bado alikua anajiiba na tulikuta lakini hapo akawa sio yule tena hali iliendelea vile alinitesa mno kwakweli na mimi kwakua binti nilimkuta bikra nikawa sielewi kwake. Ikaja likizo ndogo akaondoka tena kwenda mafia baada ya wiki na siku chache akarudi ,basi baada ya kama mwezi visa vikiwa vimezidi zaidi akaniita sehemu usiku tukakaa na akaanza kwa kufanya hivi.

Alichukua mkono wangu akaweka kwenye tumbo lake ishara kua yeye ni mjamzito ,nilishtuka sana kwani hapo tulikua na miezi 4 sijala tunda na ghafla ananiambia ana mimba. Kabla ya kuhoji akaniambia "nina mimba lakini sio yako nimekuja kukufahamisha tuachane na usije ukanisumbua tena ,mwenye huu ujauzito utamjua sio muda mrefu na dada ameshakubali hivyo nimekuja kuchukua vitu vyangu na kuondoka".

Aisee nilihisi kama kisu kinanipasua moyoni uchungu uliochanganyika na wivu ulinitawala kabla sijaongea bint akainuka aondoke nilimvuta mkono nikamuwamba kibao hapo ndo nilipoamsha moto ambao kuuzima ilikua ngumu alinijazia watu ikabidi niondoke tu kwa kukimbia kabla noma haijawa kubwa.

Baada ya siku chache mbele tangu ile siku nikapata taarifa alipewa mimba na binamu yake huko Mafia ,ila waliona wasipelekane popote maana wote ndugu. Sikujua tena kilichoendelea kutoka pale maana yule dada alihama mwezi mmoja tangu lile tukio na KAUTHARI aliondoka asubuhi yake baada ya kunipa ule ujumbe.

Maisha mtaani yalikua ya jau washikaji walinicheka kinoma yaani, ila nikaendelea na maisha.

Dah nitaendelea vidole vinauma aisee.
 
FB_IMG_1721294982956.jpg
 
Pole kwa kutendwa
 
NB:Wazee sitaki mtu yeyote anipe pole mimi naeleza hayo kumbuka kuna maisha ya kutoka uvulana kwenda uanaume kuna mambo unapitia ya kijinga na ya maana so STAKI POLE ZAIDI SHAURI TU NITAKAPOMALIZA WOTE WA TANO.
 
Nafurahia kuona oni lako ,hakika nahisi unaendelea vyema ,nikiuona uzi wa kwenda chumba maalum muda ukiwa umeenda Sana ila katika sala na Dua nilikukumbuka .

Pole kwa yote ,Allah aendelee kukurudhuku afya njema na maendeleo mema ya afya yako ,Insh'Allah .
Amen❤️🙏,.
Asante rafiki nimepona
 
Back
Top Bottom