Mapenzi yanamtatiza: Tumsaidie huyu Binti.............

Mapenzi yanamtatiza: Tumsaidie huyu Binti.............

platozoom

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
9,424
Reaction score
11,320
Ni binti mzuri kwa sura pia kichwani yuko vizuri........Ni rafiki yangu sasa yapata miezi saba. Tumekuwa tukipiga story mara kwa mara tunapokutana.

Kwa sababu ananiamini na kunichukulia kama kaka yake juzi amekuja kwangu na kunieleza tatizo lake ambalo hapo kabla hakuwa ameniambia...Ni kuhusu mahusiano yake.

Kwamba ana mpenzi wake anayempenda sana lakini miezi minne iliyopita alikuja kugundua kwamba anam-cheat, tena zaidi ya hayo akafikia kuzaa na huyo msichana.....Alivumilia na yakapita baada ya jamaa kumuomba msamaha. Mbaya zaidi baada ya kama mwezi alikuja kuona SMS ya mapenzi kutoka kwa msichana mwingine kwenye simu ya huyo jamaa.

Alifadhaika sana na kuamua kumuacha jamaa yake kwa hasira.....Na baada ya muda fulani akaja kumpata kijana mwingine ambaye ameonyesha kumpenda sana na anamjali...na inavyoonyesha mpenzi mpya anataka baadaye iwe ndoa kabisa.

Tatizo liko hapa: Anampenda sana jamaa yake wa kwanza...na yupo moyoni mwake hajafutika na kwamba anampigia simu kila wakati kumuomba msamaha warudiane. Kwake yeye anaona mtu wa future yake ni huyu mpezi mpya lakini anaona kama hayupo moyoni mwake na anashindwa namna gani amfute mawazoni jamaa wa awali ili ampende huyu mpya.

Sijamshauri mpaka sasa japo nimemuahidi kumpa ushauri wenye maana. Mimi "mbayuwayu" Naleta hapa JF nipate mchango wa mawazo ili nichanganye na zangu.
 
Ajifunze kumpenda mpenzi mpya; kwani wa zamani ataendelea kumsumbua, unless anataka mateso ya daima!

With time n devotion, atamsahau tu; l am talking from experience!
 
pole sana kwa matatizo yanayokukuta..wataalam wanajiandaa na week end subiri kidogo..wanakuja mda si mrefu watatoa ushauri mzuri tu..
 
Ajifunze kumpenda mpenzi mpya; kwani wa zamani ataendelea kumsumbua, unless anataka mateso ya daima!

With time n devotion, atamsahau tu; l am talking from experience!
Kaunga Ulikuwa kwenye mawazo yangu kabisa.........Sawasawa lakini na mimi nikawa najiuliza anaanzaje kujifunza
 
Last edited by a moderator:
Kwani huyo wa zamani kampa nini mpaka asisimsahau? Aache kuendekeza mapenzi bana.
 
mwambie aamue anataka kuishi maisha gani...

Kama ya kufumania kila siku na kukeletewa aina tofauti ya watoto wa nje aende kwa wa kwanza

kama kutulia na mumewe na kudhaminiwz awe na huyo wa pili(ingawa tabia za mwanaume wa pili hatujajua nimeassume ni mwenye staha loh....)
 
Maisha yako ni wewe unayaamua mwenyewe. Hivi ukishaona mpenzi hata mwenzi wako wa ndoa anatoka nje na ukamkamata kabisa kuna discussion hapo? Tena shukuru Mungu umegundua mapema kabla hujaingia kwenye ndoa ili uanze process za talaka na mengineyo. Just a mchumba or friend, piga chini songa mbele. Men/women are like buses, you miss one you catch the next one!!!! Tena wakati huu wa maradhi? Huyu hakupendi kabisa achana naye, ni mlafi m.a.l.a.y.a tu.
 
Watu wengine shida sana wamepewa akili na mungu lakini hawajui kuzitumia...mpe pole sana huyo binti :bounce:
 
Unafikiri unaweza kumsaidia mtu aliyepotea naye mwenyewe anajijuwa kuwa anapotea. Mwambie tu achaguwe kilicho cha uhakika yaani huyu anaetaka kumuowa au aingie kizani akingojea maudhi, magonjwa na kusaliti.
 
Hv huu ugonjwa wa wanawake kutokusahau waliowatenda unanikera thana,ninaweza mshaur zaid na ufumbuz kwan uzowefu n nao.kwa uchache n hv,kwanza afute mawasiliano hta km kakalili namb ya yule jamaa,2.ajaribu kuwa busy na mpenz wake mpya,atasahau.Mengneyo wasiliana nami nkupe.
 
Wanawake bana,akisharidhishwa kwenye niniliyu basi kosa.
 
2pa kule hajui thaman ya penz lake sa ye wanin tena,tena asithubu2 kumrudia kwan hajua km malaya hana likzo? Labda km yupo radh kushea io mal,na man akshajua dem mdhaif kiivo ndo atakua anajfanya kbolo-dinda akjua kua atasamehewa 2 lazma.kumsahau atamsahau 2 hakuna lenye mwanzo lkakosa mwsho mbn kabla ya kua nae alkua poa 2,tena naongeza iv mwambie akshkwa ashkamane
 
mwambie aamue anataka kuishi maisha gani...

Kama ya kufumania kila siku na kukeletewa aina tofauti ya watoto wa nje aende kwa wa kwanza

kama kutulia na mumewe na kudhaminiwz awe na huyo wa pili(ingawa tabia za mwanaume wa pili hatujajua nimeassume ni mwenye staha loh....)

Haya BADILI TABIA naongezea kwenye pwenti zangu za kumwambia
 
Last edited by a moderator:
Maisha yako ni wewe unayaamua mwenyewe. Hivi ukishaona mpenzi hata mwenzi wako wa ndoa anatoka nje na ukamkamata kabisa kuna discussion hapo? Tena shukuru Mungu umegundua mapema kabla hujaingia kwenye ndoa ili uanze process za talaka na mengineyo. Just a mchumba or friend, piga chini songa mbele. Men/women are like buses, you miss one you catch the next one!!!! Tena wakati huu wa maradhi? Huyu hakupendi kabisa achana naye, ni mlafi m.a.l.a.y.a tu.
Maane duh umempa maneno makavu straight.......nitayachuja na kumtupia mdogo wetu huyu ili asiharibikiwe
 
Last edited by a moderator:
Upendo what?Aaah sijui niseme nini!
 
Watu wengine shida sana wamepewa akili na mungu lakini hawajui kuzitumia...mpe pole sana huyo binti :bounce:

Haya fazaa lakini usisahau hili si jambo rahisi sana na tunatofautiana uwezo wa "kubeba"...by the way kama nimekuelewa apige ganzi moyo na akomaze akili yake
 
Last edited by a moderator:
Unafikiri unaweza kumsaidia mtu aliyepotea naye mwenyewe anajijuwa kuwa anapotea. Mwambie tu achaguwe kilicho cha uhakika yaani huyu anaetaka kumuowa au aingie kizani akingojea maudhi, magonjwa na kusaliti.
Ngekewa huyu ana tatizo lakini pia kitendo cha yeye kuliona ni hatua nzuri, la msingi tumsaidie atokeje hapa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom