Mapenzi yanapo waunganisha watu wawili na kupelekea mushkeri katika jamii

Mapenzi yanapo waunganisha watu wawili na kupelekea mushkeri katika jamii

dem nae mwehu tu, pisi Kali kumbe jambazi. Hahaha.
At first haukujua, kilichokuwepo kichwani make ni yule Bester wa mambo ya mitindo wakati yupo chuo kikuu. Aliyekuja kukutana nae baadae baada ya kudanganywa na mitandao ya kijamii iliyomjenga Bester ni tofauti kabisa hapo ndipo "Love leads the way" took place
Ila tujue kuwa technology ikikuacha nyuma, kuna mambo unaweza fikiria hayawezekani kumbe kwa walioko tayari kwenye level kubwa ya kiteknolojia wanaweza wakakuibia wewe kilakitu uliyopo nyuma ya hiyo technology.....
Asante Intelligent businessman
 
Episode 3.

Kisha akazungumza na Dr Nandipha akitaka amsaidie Jambompango muhimu aliokuja nao Bester
Ulikuwa ni huu hapa Alitaka afungiwe katika chumba chake mwenyewe.

Ni chumba ambacho mfungwa huwekwa ikiwa atakuwa ni tishio kwa wengine au kama maisha ya mfungwa huyo yako hatarini.

Pia akasema akiwa katika chumba hicho inatakiwa upatikane mwili wa mtu aliyekufa na uingizwe kwenye chumba kwa siri kubwa.

Na hapo ndipo yeye atakapofanya mpango wa kukichoma moto chumba hicho,
then atatoka na kuuacha mwili huo uteketee kwa moto, kisha baada ya tukio hilo.
Mpango kazi ulianza..Crimes Committed by Dr Nandipha.
Dr Nandipha alianza kudai mwili mmoja katika Mortuary ya Hospital ambayo alikuwa anaifahamu vizuri.

Aliijua vyema hospital hiyo na uongozi wake kutokana na kwamba aliwahi kufanya kazi katika hospital hiyo alitafuta mwili ambao hauna Ndugu kabisa.
Aliuchukua mwili huo Na kuupeleka gerezani.

mtu aliye sehemu ya mpango huo aliingiza mwili gerezani kwa njia ya kuonekana kama ni mfanya usafi katika gereza hilo.
Mwili uliwekwa kwenye dustbin kubwa kisha mtu huyo alisimamia dustbin hilo na kufuata maelekezo kama yalivyotolewa na Thabo Bester.

Kisha Thabo Bester aliomba kuwekwa kwenye chumba cha pekeake akidai kuwa kuna baadhi ya wafungwa wanataka kumuua.
Ombi hilo lilishindikana baada ya askari watiifu kuharibu mchongo.
Kwa kuwa mwili ulisha ingizwa katika gereza ilibidi kutolewa kwa njia hiyohiyo ya siri.
Lakini mara hii Thabo Bester alimuomba tena Dr Nandipha aingize mwili mwingine gerezani kwa kudai kuwa ameshaweka sawa mipango yake,
mwili wa pili uliingizwa na zoezi likashindikana tena, Bester alikataliwa kuingia kwenye chumba hicho.

Mwili ukatolewa.., bester hakuchoka ali andaa Tena mpango wa tatu.
Alimuomba Dr Nandipha tena alete mwili, na hawamu hii mpango ukakubalika.
Bester alikubaliwa kuingia katika chumba hicho cha pekeake kisha maiti ikaingizwa katika chumba hicho na kukichoma moto chumba kisha yeye kutoka akivaa mavazi ya askari wa gereza hilo.

Kisha akatoka Kama mfanyakazi- na kuishia zake!.

Baada ya Bester kutoroka gerezani kwa kufake kifo chake, habari zikatangazwa mfungwa anayetambulika kwa jina la Thabo Bester afariki gerezani kwa ajali ya moto.

Na ndipo Dr Nandipha alipokwenda kuudai mwili huo,alisema ni mume wake aliyefunga naye ndoa.
Naijua una jiuliza ili kuwaje, wakati nandipha Alikuwa na mumewe!?.
.Dr Nandipha aliachana na Mume wake mwaka 2017,
Hivyo wakati huo alikuwa mwenyewe that's why alifanya kila alichoambiwa na Bester.
Wakagushi ndoa ili ionekane walisha oana.

Kisha tukio la ajali ya moto litakapotokea Nandipha ataenda kumdai mtu huyo aliyeungua kwa kusema ni Mume wake aliyefunga naye ndoa hivi karibuni.
Na atakapopatiwa mwili huo atakwenda na kuuzika,
maana yao kubwa ni kwamba Mwili usichunguzwe na kutambulika kwamba mtu aliyeungua katika moto huo sio Thabo Bester.
Hilo lilifanikiwa na Dr Nandipha alipatiwa mabaki ya mwili huo, ila kabla ya kupatiwa mwili huo ulipelekwa mortuary kisha akapewa na kuuzika.

Dr Nandipha akaanza kuishi rasmi kwa siri na Thabo Bester,
alikuwa akiishi naye katika jumba lake la kifahari hapohapo South Africa.
Kubaki kwao South Africa Perhaps hili ndio kosa kubwa walilolifanya..
Siku moja Camera zilimnasa Dr Nandipha akifanya manunuzi na mwanaumeMmoja aliyevalia miwani na Nguo zenye mtindo wa kufanana chini na juu,

katika muonekano wa Picha nadharia inakuja mwanaume huyo hakutaka kuonekana mbele ya macho ya watu Alivalia miwani meusi na alikuwa makini sana.
Picha hii iliwafanya hata watu wenye uelewa Mdogo kudadisi na kutaka kufahamu huyo Mwanaume aliyeonekana na Dr nandipha ni nani??
FwktjJpWcAIWWJT.jpeg

Na hapo ndipo watu walipoanza kulinganisha sura ya mtu huyo na Thabo Bester,
uvumi ukazidi Picha ikasambaa mitandaoni kwamba Thabo Bester aliyesadikika kufariki Gerezani kwa ajali ya moto ameonekana na Dr Nandipha.

Ndipo walipoamua kufanya mpango wa siri Wa kutoroka nchi,
mpango wao wakwanza ulikwama baada ya kufika kwenye mpaka wa Zimbabwe na kuletewa noma.
Dr Nandipha na Thabo Bester waliamua kulitelekeza gari hapo mpakani na kurudi kwenye maficho.Wakati huu Dr Nandipha alikuwa akitoka pekeake huku Thabo Bester akiwa mafichoni.
Siku moja Dr Nandipha akiwa mgahawani,

alifuatwa na watu wa3 ambao walilazimika kuja hapo baada ya gari lililotelekezwa kwenye mpaka wa Zimbabwe kujulikana linamilikiwa na Dr Nandipha.
Mmoja wa watu hao alikuwa ni muuzaji wa Magari, ambaye alimuuzia Dr Nandipha gari hilo kwa pesa nusu huku akiwa anamdai baadhi ya pesa.
Na wawili ilisadikika ni makachero wa polisi, moja ya video iliyovuja hivi karibuni ilionyesha Dr Nandipha akiwajibu maswali watu hao bila hofu huku akiendelea kupata Chakula.

Ni mwanamke mwenye confidence ya hali ya juu.
Baada ya mahojiano na watu hao, Dr Nandipha na Thabo Bester waliona hili jambo liko serious,
maana tayari vyombo vya habari SA vilianza kuzungumzia juu ya mtu aliyefariki gerezani kwamba perhaps bado anaishi.

But ukweli ni kwamba.Jambo walilo kuwa wana lihisi ni ukweli mtupu.
Na ndipo Dr Nandipha na Thabo Bester walipofanya mpango mwingine wa kutoroka nchi.
Walifanikiwa na kukimbilia Tanzania ambako walikuwa na mpango wa kupitia Kenya na kwenda walikotaka kwenda.

Makachero wa Tanzania..Walianza kuitilia mashaka gari nyeusi tokea Dar es salama, wakaamua kuitilia mkazo wa kuichunguza gari hiyo.
ambayo ilionekana ikizagaazagaa katika Hotel fulani na raia wa kigeni.
Kisha siku iliyofuata gari ikatoka na kuelekea uelekeo wa morogoro road,Bado makachero hawakukosa kiu ya kuwadadisi watu haoSafari hii ilikuwa ni mtafutano wa kimyakimya mpaka jijini Arusha.

makachero baada ya kujiridhisha kuwa watu hao ndio wanaotafutwa huko south Africa ndipo walipoamua kuwaletea noma.
Dr Nandipha na Thabo Bester walitaka mazungumzo ya kirafikiKutoka kwa makachero, Lakini hali haikuwa kama walivyo tarajia,
Walipoona kuwa hawasikilizwi ndipo walipoamua kuongea Lugha ya dharau,
kisha kutelemka kwenye gari na kutaka kuwaletea fujo makachero.
Wakadakwa no discussion selo."Don't take pictures"Alisema Thabo Bester baada ya kufikishwa kituo cha polisi.
FwkuHhLXoAEqOaj.jpeg

Mtu mwingine aliye fahamika kwa jina la Zakaria Alberto raia wa Mozambique.
ambaye huyu alikuwa Kama tour guide.

Mawasiliano kati ya Tanzania na South Africa yakafuatwa vyema.Ndipo mpango wa kuwapeleka watu hao SA ulipofanyika sababu walikuwa wakitafutwa na walikuwa na mashtaka ya kujibu huko.
Thabo Bester alifake kifo na kutoroka kwenye gereza lenye ulinzi mkali tarehe 3 Mei 2022 Akaja kukamatwa nchini Tanzania tarehe 7 Aprili 2023 wakati wa weekend ya Pasaka,

hiyo inamaana Bester na Dr Nandipha walikula kuku kwa mrija takribani miezi1103-05-2022 mpaka 07-04-2023.
Thabo Bester & Dr Nandipha wamerudishwa South AfricaNi machache yanayowahusu ila Yapo mengi yaliyofanywa na watu hawa but mahakama ndio muamuzi wa mwisho.

What comes around goes around, Stay safe kwa ground mambo ni mengi sana.
FwkuK_gXsAQlmaV.jpeg

salute to wisdom.

I mean no malice to nobody,
 
At first haukujua, kilichokuwepo kichwani make ni yule Bester wa mambo ya mitindo wakati yupo chuo kikuu. Aliyekuja kukutana nae baadae baada ya kudanganywa na mitandao ya kijamii iliyomjenga Bester ni tofauti kabisa hapo ndipo "Love leads the way" took place
Ila tujue kuwa technology ikikuacha nyuma, kuna mambo unaweza fikiria hayawezekani kumbe kwa walioko tayari kwenye level kubwa ya kiteknolojia wanaweza wakakuibia wewe kilakitu uliyopo nyuma ya hiyo technology.....
Asante Intelligent businessman
Episode 3 tayari mkuu.
 
Back
Top Bottom