Mapenzi yanapo waunganisha watu wawili na kupelekea mushkeri katika jamii

Mapenzi yanapo waunganisha watu wawili na kupelekea mushkeri katika jamii

Episode 4.

Wakati mwingine unajiuliza THABO BESTER ni mmoja au ni kundi la watu?Ikiwa THABO BESTER ni kati ya kundi la watu,
Je yeye ni nani katika kundi hilo.? Je! Yeye ndio master plan wa kundi hilo.?

Why ana endelea Kuushangaza ulimwengu, kwa matukio yake magumu.
na yasio dhaniwa kufanywa na mtu mmoja.

Katika chumba cha mahojiano yaliyovuja na Investigators hivi karibuni.
THABO BESTER alinukuliwa akisema.."If money is the life of people, justice will not exist in the world"..

Tk motsepe
Jina alilopenda kulitumia kwenye michongo, akiwa ndani ya chumba hicho cha mahojiano alisema tena...

don't need to talk any more, I want to take a break".

Alizungumza maneno hayo akiwa na hasira, huku akipigapiga meza, ilikuwa ni baada ya kukamatwa TANZANIA na kurudishwa SA.

Brigedia Jackson Mkhaulesi, moja ya wachunguzi wanao chunguza kesi ngumu ni makini na machachali kwenye miji ya Durban,
Cape Town, Johannesburg na miji mingine hapo South Africa, aliskiliza kwa makini maneno ya THABO BESTER katika chumba cha mahojiano.
na ndipo alipo gundua maneno machache kupitia thabo bester.
Ni maneno machache yaliyosema.."If money is the life of people, justice will not exist in the world

"Brigedia Jackson Mkhaulesi akiwa kama jasusi na mbobevu katika maswala ya uchunguzi.

Aliona thabo bester hayuko peke yake.

Mtuhumiwa namba moja aliyemuona ni Dr Nandipha magudumana.Crimes Committed by Dr NandiphaBrigedia.

Jackson alijiridhisha juu ya hilo kitokana na matukio ya maiti 3 kuingizwa ndani ya gereza, ni mpango uliofanywa na Dr Nandipha,
Lakini pia baada ya THABO BESTER kutoroka gerezani kwa kufake kifo cha moto,
DR NANDIPHA alimuhifadhi BESTER kwa kumficha kwenye jumba lake la kifahari na mwisho kutoroka naye nje ya nchi.
Mtuhumiwa wa pili ni baba Mzazi wa Dr Nandipha huyu ni mzee Zolile Cornelius Sekeleni.
Crimes Committed by Zolile Cornelius Sekeleni.Brigedia Jackson,
aliamini Mzee Zolile anajua kila kitu kuhusu mpango wa mwanaye, akiwa kama baba why hakutoa taarifa mapema .
Baba alijua mwanae anaishi wapi ivyo alikuwa na uwezo wa kuwaona watu wanaoingia na kutoka katika nyumba hiyo" .
Brigedia Jackson alisema..Pia aliamini hata magari yaliyokuwa yanatumika kusafirishia maiti mengine yalikuwa ya mzee Zolile Cornelius Sekeleni.

Brigedia Jackson baada ya kumtia hatiani baba mzazi wa Dr Nandipha.
Sasa akawaza ni nani aliyekuwa mkuu wa ulinzi wa getini hapo gerezani na ndipo anamfikia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la MOTANYANE MASUKELA.

Huyu alikuwa ni mkuu wa ulinzi getini, ana la kujibu bwana MOTANYANE MASUKELA akakamatwa mchana kweupee akaeleza.
Kwamba yeye na vijana wake walikuwa wanachati wakati THABO BESTER anapita hapo getini..
Kisha Brigedia JACKSON akawafikia watu wa3 ambao ni Tieho Makhotsa, Nastassja Jansen na Teboho Lipholo, huyu Teboho ni "CCTV installer" fundi wa mifumo ya Camera za ulinzi wa Gs4.

Wakati Tieho na Nastassja ni wasimamizi wa chumba cha kuongozea camera "Camera control room" wote wakakamatwa.
Lakini udadisi wa Brigedia JACKSON bado ulikuja lazima kuna mtu alikuwa anatumika kuingiza maiti gerezani.
Brigedia Jackson akawa mbwa anayenusa vikali ndani ya gereza la Mangaung.

Baada ya kunusanusa sana akamfikia SENOHE MATSOARA ambaye huyu alikuwa akifanya kazi katika gereza kama dereva.
Huyu SENOHE MATSOARA alianza kufanya kazi kama "Counselor".
Mtoa ushauri na mtatua changamoto za wafungwa, akaaminika akawa dereva mara akawa msimamizi mkuu wa magari yote yanayotoka na kuingia katika gereza hilo.

Ghafla SENOHE MATSOARA maisha yake yalianza kubadilika, akawa ni mtu wa bata na Mzee wa kumwagilia moyo, alipoingia club aliingia na wanawake warembo wanne wanne.

Alikuwa mtumiaji mzuri wa mtandao wa Facebook, alionyesha nyumba, mavazi, na alinunua gari yake ya kifahari huku akijinadi katika mtandao huo.

Crimes Committed by SENOHE MATSOARA.
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Katlego Bereng, alikuwa akikatiza mitaa ya kituo cha Tax cha Pretoria, mara anaonekana kuweweseka ghafla nguvu zinamuishia na kutafuta sehemu akae lakini hakufanikiwa kufanya ivyo badala yake akadondoka chini kwa kishindo kama kiroba.

Kisha gari inasogea eneo la tukio na kumchukua kijana huyo mpaka hospital, hakikupita kipindi kijana akafariki.

Majira ya jioni watu kadhaa wanafika hospitalni na kujitambulisha kama ni nduguze na marehemu ya kwamba wanautaka mwili.

Wakafuata taratibu zote na wakapatiwa mwili lakini watu hawa walikwenda mpaka gereji bubu na kuiacha gari yenye mwili huo humo,

Asubuhi na mapema katika gereza la Mangaung linaonekana lori la usafi likishusha madustbin makubwa ya kuifadhia uchafu.

Kisha lori hili linaondoka na kuyaacha madustbin hayo hapo gerezani kwa maana ya uchafu wote uendelee kuifadhiwa vyema.

Mtu mmoja anaoneka kulichukua dustbin moja na kulipeleka angle ambayo Hakuna CCTV camera na ilipofika usiku tukio la kuwaka moto likatokea kwenye selo aliyo fungwa bester.

Usimamizi wa magari kuingia na kutoka gerezani ulikuwa chini ya SENOHE MATSOARA,
Hivyo Brigedia Jackson akiwa kama mbobevu kazini alijua wazi maiti zote ziliingizwa gerezani na SENOHE MATSOARA.

Aling'amua hilo kupitia mtililiko wa CCTV camera na kila dustbin zilivyo kuwa zinaingizwa, mtu fulani alionekana kuchukua dustbin moja na kuipeleka kando.

Brigedia Jackson akapiga mstari na kuamini MATSOARA ni wakukamatwa tu.
Kwa maana hiyo!!

Dr Nandipha kazi yake ilikuwa kuandaa maiti na kuzitoa mahospitalni kwa njia aliyoijua yeye na kisha SENOHE MATSOARA kusafirisha maiti kuziingiza gerezani.

na hata mpango uliposhindikana MATSOARA alitoa tena maiti na kwenda kuzika kwa kushirikiana na DR NANDIPHA.

Tubaki hapahapa kwenye kuzika...Maiti iliyoleta matokeo chanya kwenye mpango huu wa kutoroka kwa Thabo bester ni maiti ya3 ambayo ni ya kijana Katlego Bereng.

Tubaki hapahapa kwenye kuzika...Maiti iliyoleta matokeo chanya kwenye mpango huu wa kutoroka kwa Thabo bester ni maiti ya3 ambayo ni ya kijana Katlego Bereng.

Sasa baada ya BESTER kufake kuwa amefariki kwa kuungua moto katika selo, watu Wakaaminishwa kuwa aliyeungua moto katika selo ile ni BESTER,
habari zikasambaa SA, na Dr Nandipha ndipo alipokuja na kuudai mabaki ya mwili ule kwamba ni ya Mume wake aliyefunga naye ndoa hivi karibuni.
Tuelewane vizuri hapaKabla ya DR NANDIPHA kupatiwa mabaki ya mwili, mwili wa mtu aliyedai ni Mume wake.

kama ilivyo sehemu ya mpango wazike mwili huo ili kupoteza ushahidi haraka kisha yeye na Bester wale kuku kwa mrija.

Sasa mabaki ya mwili huu yalichukuliwa na kupelekwa mortuary kisha akapewa na kwenda kuuzika.

Hili ndilo kosa alilolifanya DR NANDIPHA kuruhusu mabaki ya Mume fake yaingizwe mortuary kisha apewe..

Hakujua kuna JACKSON MKHAULESI jasusi mwenye tabia za kijasusi, mwenye kuzingatia zaidi matukio, akiamini matukio yanatabia ya kuendelea na kujirudia akiamini kukusanya matukio na kuyaweka katika file moja ni kufanya kazi yake kuwa nyepesi.

Ndicho alichokifanya brigedi JACKSON MKHAULESI baada ya tukio la moto kutokea na mabaki ya mwili kupelekwa mortuary alifanya mpango wa siri sana na madaktari watiifu na kupewa vipimo vya DNA kisha akavihifadhi katika data zake.

Ivyo siku zote hizo Brigedia JACKSON alikuwa anafuatilia nyendo za DR NANDIPHA, ila Dr Nandipha hakuwahi kujua kama anafuatiliwa na mpelelezi hatari zaidi hapo South AfricaLilikuwa ni swala la muda tu.

Na hata gari lake lilipo kamatwa mpakani ulikuwa ni mpango wa Brigedia JACKSON, na baada ya Dr Nandipha na Bester kuliacha gari lile pale mpakani Zimbabwe, watu waliokuja kumfuata DR Nandipha mgahawani na kumuhoji watu wale ni vijana wa Brigedia JACKSON.


Sasa hapa hata mimi naanza kuhisi kitu Kupitia picha walizopigwa Dr Nandipha na Thabo Bester wakinunua bidhaa dukani,
Ukiziangalia kwa umakini Picha hizo utagundua mtu aliyepiga alidhamilia hakupiga kwa bahati mbaya.

Inawezekama Thabo bester wakati anapigwa Picha alihisi kitu au kumuona aliyempiga Picha kutokana na muonekano katika Picha, perhaps aliyewapiga Picha ni kijana wa Brigedia Jackson.

Hii nime jaribu kuwaza Mimi!!

Sasa baada ya Dr Nandipha na Thabo Bester kukamatwa Tanzania na kurudishwa South Africa ndipo mambo yakaanza kuchemka, DNA ikapatikana kwa haraka na kubainika aliyeungua gerezani sio Thabo Bester bali ni kijana Katlego Bereng.

Ndugu wa Katlego Bereng, wakajitokeza na kudai mabaki ya mwili wa kijana wao wamzike lakini pia walilaani vikali matendo ya Thabo Bester ikiwa alihusika kwenye kifo cha kijana huyo.

Mabaki ya mwili yakafukuliwa, sababu yalisha zikwa na Dr Nandipha na sasa wakapewa Ndugu sahihi na kufanya mazishi..

Jioni ya tarehe 05-06-2023 Brigedia Jackson baada ya kutoka mahakamani kwenye kesi ya Thabo Bester na Dr Nandipha kisha kesi hiyo kuhailishwa mpaka June20,

Brigedia aling'aka akitaka kesi hiyo iishe haraka kwani ushahidi upo na unajitosheleza na akasema Dr Nandipha hapaswi kupewa dhamana.

Hii yote ni kwasababu Dr Nandipha alikuwa anaomba apatiwe dhamana, na pia alikuwa akilalamika juu ya ukamatwaji wao TANZANIA haukuwa wa haki bali ni kama walitekwa.

Brigedia Jackson akiwa mahakamani na kuvalia koti lake jeusi, sura yake aliikaza na kumtazama Judge aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo.Judge akatupilia mbali maombi hayo ya Dr Nandipha na kudai malalamiko yake hayana mashiko ni ujanjaujanja tu.

Sasa baada ya mjadala kufungwa mahakamani Brigedia Jackson akachukua mkoba wake wenye data muhimu za kesi hiyo na kuuweka kwenye gari yake.
hii ni kwa sababu yeye ndiye msimamizi mkuu wa kesi hiyo ivyo data zote muhimu huwa anabeba mwenyewe.

Akaingia kwenye gari yake na taratiibu akanza safari haijachukua muda katika makutano ya barabara kando kidogo gari ya Komredi Jackson Inaonekana kuegesha mara unasikika mlio mkubwa wa risasi uliopelekea mpaka kioo cha gari kuvunjika na damu nyingi kuruka njee ya gari.

Kisha Punde taarifa zinasambaa kuwa Brigedia JACKSON MKHAULESI afariki dunia kwa kujipiga risasi ndani ya gari yake.

Kama utani lakini ndio uhalisia Brigedia, mpelelezi na jasusi machachali ameenda.Kifo chake kinachunguzwa lakini taarifa za awali ni kwamba brigedia amejipiga risasi mwenyewe.
Stay safe kwa ground mambo ni mengi sana.
FyU6WASXsAAKYqs.jpeg

I mean no malice to nobody,
salute to wisdom.
 
Back
Top Bottom